Alikubamiza miezi nane gerezani, leo mmekuwa marafiki wa kufa na kuzikana

Alikubamiza miezi nane gerezani, leo mmekuwa marafiki wa kufa na kuzikana

Baada ya gia angani 2015 naona kazi ya kumtetea Mbowe ngumu sana.
Kaja kujimaliza mwenyewe kwa kutowashauri vema wafuasi wake akina Musa Mwalimu, Yericko, n.k.
Katika uchaguzi wa 2015, Chadema ilipata wabunge 73, nyongeza ya 25. CUF walipata 42, nyongeza ya 8. CCM ilipata 260 ikiwa ni nyongeza ya viti 6. Lowassa alipata 40% ya kura zote na JPM 58.5%. Chadema ilipata 32% ya kura zote na CCM 55%. Sasa niambie Mbowe aliwaangusha vipi? Ugumu wa kumtetea utatoka wapi?

Matokeo hayo ndio yaliwatia hofu CCM dhidi ya Chadema ya Mbowe maana walijua kuwa wangeruhusu iendelee wangeweza kushindwa 2020. CCM haitaweza kuruhusu Mbowe apate uongozi Chadema maana wanajua uwezo wake.

Amandla...
 
Ndugu ,you have nailed it... Mbowe ni mwanasiasa halisi sio mwanaharakati kwa aslimia ata 20% .Waliochukua chama kwasasa wao ni harakati,payuka,tukana,beza nk.. CHADEMA kwasasa aiwezi kufanya operation yenye maana kama enzi za Mbowe-OPERATION SANGARA
Sahihi
 
Mimi nilipoteza imani kwa Dj baada ya kubadili gia angani kwa kumpokea Lowassa na kumpa tiketi ya kugombea uraisi, kila nikijiuliza sipati jibu, pia nilipoteza imani kwa mheshimiwa sana Dj baada ya msaidizi wake ben kupotea na akauchuna kama aliyepotea si msaidizi wake wa karibu na mwisho kwa Mzee Kibao na sasa kaonyesha wazi tabia yake, kuna wakati kwa mtu kama yeye alitakiwa atumie busara na hekima ya kukaa mbali na hao waliokuwa watesi wake, kama hao waliomfunga miezi 8 anaweza kufurahi na kusikitika nao iweje leo isiwe hivyo kwa wenzake ambao amekuwa nao miaka kibao na ambao walikuwa wanashinda mahakamani na kupaza sauti ya kuachiliwa kwake yeye anashindwa kurudisha mkono?
Kama.hufahamu siasa usiwe unachangia mada za kisiasa mkuu. Hakuna asiyejua influence ya lowasa na hakuna kipindi ambacho Chadema imefanikiwa kwenye Siasa kama kipindi ambacho lowasa ameenda Chadema. Nenda uka comment mada zingine mkuu
 
Katika uchaguzi wa 2015, Chadema ilipata wabunge 73, nyongeza ya 25. CUF walipata 42, nyongeza ya 8. CCM ilipata 260 ikiwa ni nyongeza ya viti 6. Lowassa alipata 40% ya kura zote na JPM 58.5%. Chadema ilipata 32% ya kura zote na CCM 55%. Sasa niambie Mbowe aliwaangusha vipi? Ugumu wa kumtetea utatoka wapi?

Matokeo hayo ndio yaliwatia hofu CCM dhidi ya Chadema ya Mbowe maana walijua kuwa wangeruhusu iendelee wangeweza kushindwa 2020. CCM haitaweza kuruhusu Mbowe apate uongozi Chadema maana wanajua uwezo wake.

Amandla...
Kitendo cha kuachana na itikadi ya chama tayari ilikuwa hasara kubwa isiyoweza kufidiwa na idadi yeyote ya madiwani na wabunge ambao baadhi walikikimbia chama na kurudi CCM.
Nguvu ya kuwa na itikadi umeiona maandamano ya 2025. Kabla ya Lowassa walikuwa watu wakiitwa kuandamana wanajitokeza, baada ya Lowassa walikuwa hawajtokezi. Baada ya kuondoka Mbowe umeona Ile Oktoba 29.
 
Ninachokiona mimi ni kuwa CCM wanamhofia Mbowe zaidi ya wanavyo mhofia Lissu. Wanajua Mbowe ana uwezo mkubwa wa kujenga na kuongoza chama chake. Ndio maana zinafanyika kila aina ya mbinu kumuharibia. Mimi mwenyewe nilistuka nilipoona wafuasi wakuu wa CCM wakimpigia debe la wazi Mbowe wakati wa uchaguzi wa Chadema. Walijua watu wataamini kuwa CCM wanamkubali kuliko Lissu na hivyo watampigia Lissu ambae alikuwa ndio chaguo lao. Na kweli, zaidi ya mwaka umepita na tunachokiona ni matamko tu ya jukwaani, presa na posts kwenye social media.

Mimi naamini Mbowe amesoma huo mchezo na anaenda nao hivyo akiangalia picha kubwa. Mbowe ni kama Michael Corleone katika Godfather. Yeye sio Sonny.
Ndio maana watu wake wengi nao wako kimya. Atawastua wengi atakapo rudi katika siasa.

Amandla...

..jinsi serikali wanavyomtesa Lissu ndivyo wanavyozidi kuikabidhi Chadema kwa wanaharakati.

..mazingira ya Mbowe kurudi kwenye siasa yanazidi kuwa magumu kama moderates hawana nafasi ktk political space.

..siasa zinazoendelea sasa hivi hazina " afya " kwa Mbowe, wala Lissu. Na asitokee mmoja wao akajiona yeye ana afadhali machoni mwa Ccm.
 
Mnaopenda gutter politics lazma mtaumiza mioyo yenu tu bure. Mh.Mbowe anajua maana halisi ya uongozi,upinzani na siasa kuliko wengi asa upande wa upinzani. Kinacho kosekana kwa sasa ndani ya CHADEMA hamna mtu mwenye hulka ya hivyo. Pamoja na yote Mh.Mbowe akuwai kuwataka wananchi na wafuasi wa CHADEMA waichome nchi...UKWELI NI KUA LISSU atoshi kwenye siasa zenye ustaarabu na utaifa..Kinachowagharim ndiyo hicho
Wewe bado unasumbuliwa ni mzimu wa ushabiki wa kikabila, ambao ndo uliponza wengi wakiamini ni mtu ana ufahamu. Huyu hana ufahamu. ni kama taka tu!
 
If it is politics, Yes! However, the kind of CCM behaviour is not politics. It is enmity!
Ukipatana na CCM kwa sababu za kisiaza, ni sawa na kusema Idd Amin angerudi kujenga Uganda, Which is fallacy!
gentleman,
you can perceive CCM as you wish, but in politics anything can happen at any given time 🐒
 
Pamoja na yote Mh.Mbowe akuwai kuwataka wananchi na wafuasi wa CHADEMA waichome nchi...
Acha uongo, si alifunguliwa kesi ya ugaidi na kutaka kuua viongozi wa kitaifa au DPP alidanganya?

Ni hivi Freeman akiwa mwanadiplomasia mnamchekea ila siku alipodai katiba mpya akaitwa Gaidi!! Hata Lissu leo akianza maridhiano mtaanza kumsifia hapa!!

Unafiki hauwezi kulisaidia hili taifa
 
Wewe bado unasumbuliwa ni mzimu wa ushabiki wa kikabila, ambao ndo uliponza wengi wakiamini ni mtu ana ufahamu. Huyu hana ufahamu. ni kama taka tu!
Hili ni nshomile la Bugandika
 
Acha uongo, si alifunguliwa kesi ya ugaidi na kutaka kuua viongozi wa kitaifa au DPP alidanganya?

Ni hivi Freeman akiwa mwanadiplomasia mnamchekea ila siku alipodai katiba mpya akaitwa Gaidi!! Hata Lissu leo akianza maridhiano mtaanza kumsifia hapa!!

Unafiki hauwezi kulisaidia hili taifa
Unafiki unakuumiza..kumbe Lissu ndiye anadai Katiba Mpya.. nilijua ni watanzania wote.
 
Wewe bado unasumbuliwa ni mzimu wa ushabiki wa kikabila, ambao ndo uliponza wengi wakiamini ni mtu ana ufahamu. Huyu hana ufahamu. ni kama taka tu!
Nikisoma comments za makamanda ,najiuliza hivi awa eti ndiyo wanataka kweli twende Ikulu? Hapana,tubaki tu kundi la harakati.
 
Back
Top Bottom