Mbowe bado ana wafuasi wengi ndani ya Chadema. Akirudi tu kwenye siasa wataungana nae. Chadema ya Mbowe ilipambana kuliko ya hivi sasa. Na wengi wanakumbuka hilo.
Mbowe hapendwi na CCM. Wanamkumbatia ili kumharibia machoni mwa Chadema. Wanajua
ana uwezo wa kukijenga chama chake na kuibua watu wenye uwezo mkubwa. Chadema ya Lissu ni one trick pony. Sasa hivi wameelekeza nguvu zao karibu ya zote kwenye kesi ya Lissu. Wakati wa kesi ya Mbowe, Chadema iliendeleza mpambano nje ya Mahakama. Ingawa wanaharakati na wanamtandao walimpigania sana lakini hawakuwa peke yao.
Bawacha, Bavita, Bazecha waliendelea kumpigania na kukipigania chama bila uoga. Waliwekwa ndani lakini kesho yake walikuwa mtaani.
Amandla...