taira la mirembe
Senior Member
- May 29, 2015
- 188
- 63
Wakuu habari zenu,
Kuna swala limenishangaza kidogo! Kuna mdogo wangu amefariki juzi Ijumaa ya tar 24/7/2015 kwa ugonjwa wa kansa ya utumbo mpana. Siku mbili nyuma kabla hajafa alikuwa anaongea vitu vya ajabu ajabu na akili inakuwa sawa, ila siku ile ambayo alikuwa anakata roho alikuwa anaongea kiarabu si kiarabu yaani alikuwa anaongea lugha isiyoeleweka na kabla ya kukata roho aliniambia nipige magoti na akanishika kichwani huku akitaja jina langu. Na pia alifanya hivyo kwa watu wote tuliokuwa tunamuhudumia kwa ukaribu sana.
Ila kilichonishangaza zaidi ni kitendo cha kufa tarehe aliyozaliwa na zote zikiwa ni siku ya ijumaa! Alizaliwa 24/7/92 na amekufa 24/7/2015 zote zikiwa ni ijumaa.
Swali langu ni kwamba hii inaweza kuwa na maana yoyote?