Alikuwa anaenda kuolewa akamtumia ujumbe Ex eti waagane, imefanya niwaze sana kuhusu suala la kuoa

Alikuwa anaenda kuolewa akamtumia ujumbe Ex eti waagane, imefanya niwaze sana kuhusu suala la kuoa

Juzi niliudhuria send-off Moja mkoa X, Huyu Binti ni mwenyeji wa huo mkoa, sasa alipata mchumba mkoa mwingine na alikubali kuolewa, aliyekuja kumuoa alimwambia direct kwamba nataka kukuoa, yule mwanamke hakukataa licha ya kua na mahusiano yake ya mwanzo (alikubali kwa sababu mtu wake wa mwanzo alikua aeleweki kuhusu ndoa), huyo mtu wa mwanzo wa bibi harusi ni rafiki yangu,

Send off imefanyika jumapili, leo yupo safarini kwenda kwenye sherehe ya ndoa mkoa mwingine alipo bwana wake mpya, lakini cha kushangaza Jana huyu bibi harusi mtarajiwa alikua anamlazimisha mshikaji wangu ambaye ni ex wa Huyo Bibi harusi, aende wakaagane (sms nilisoma), Tena bibi harusi akasema "usipokuja nitakuchukia maisha yangu yotee, nataka unipe show ya nguvu tuagane"

Nilivyosoma hiyo sms nikajikuta namuonea huruma bwana harusi, huko alipo amepambana kuunda kamati, amekopa ili kufanikisha sherehe, anajua mke wake mtarajiwa yuko kwenye send-off kumbe mke mtarajiwa analilia dudu la yuyu.

Imenifanya niwaze sana na kuona ugumu uliopo kwa vijana wa kipindi hiki kuoa, sometimes nawaelewa wanaosema ni bora uoe bikra, kwa sababu utakua na assuarance kwamba hiyo kitu haijachakazwaaa.

Kuchakazwa sio shida, shida ni bond waliyokua nayo na mchakazaji, nipo karibu na chuo cha NIT mabibo hapa, naona watoto wanavyochakazana, Yani wanasuguana haswaa mpaka na kufungana kamba, lakini kumbuka huyo ni mke wa mtu mwingine wa baadae.

Kizazi hiki ukiona mtu ameoa, ujue amekubaliana kujivika mabomu, Tena akiwa ni msomi, yaani umekutana nae baada ya kumaliza chuo sijui kama atakuheshimu, na ukimkuta yupo kazini basi wewe vidonge vya pressure jitahidi uanze kuvijua mapema.
Kuna haja ya kufanya research ili kubaini kwanini Bond ya Ma X huwa ni Strong kuliko Ionic Bond
 
huku kwetu kwa watu ambao hatujaelimika,binti kwenye Harusi anasindikizwa na kikosi kazi cha familia.Huko kwenu binti anakwenda kwenye sherehe ya Arusi yake akiwa peke yake na anaweza akalala popote.
Nawapongeza kwakuwa na akili kubwa za namna hiyo
 
Back
Top Bottom