Aliniacha kwa fedheha, lakini leo anahitaji msaada wangu

Toa msaada wema hauozi bana, duniani tuliletwa tusaidie watu, pia huyu kakufundisha mahusiano yalivo. Na dunia ilivo ya ajabu IPO siku aweza kuja kukuokoa. Wewe msaidie ila kata mazoea naye utashangaa utapata armani moyoni
ok
 

Mkuu Msaidie huyo Mdudu,hiyo ni fursa adhim ya kufanya Closure na yeye.Msaidie kisha mfungie ukurasa.Asikutafute mpaka kiyama.Yeye ndiye kapoteza,kwa nini umshikilie rohoni mwako mjinga mmoja tu huyo.
 
Mkuu Msaidie huyo Mdudu,hiyo ni fursa adhim ya kufanya Closure na yeye.Msaidie kisha mfungie ukurasa.Asikutafute mpaka kiyama.Yeye ndiye kapoteza,kwa nini umshikilie rohoni mwako mjinga mmoja tu huyo.
ok
 
Mkuu pole sana kwa yaliyokupata.
Yaliwahi kunipata na mimi kwa mtindo huo huo.
Usije ingia mtego wa kusolve economic problems za huyo binti, maana tatizo likiisha atayeyuka tu kama barafu kwenye jua.

Narudia usijeingia mtego huo, wamekula wengine sasa wewe ndio wa kupangusa makali.
 
Kuna mambo mawili hapa ambayo watoa maoni wengi naona kama wanayachanganya,
1) Kwanza ni je urudiane naye ama la?

Hili ni juu yako, usikilizie moyo wako unasemaje, umelalamika kwamba ulimpenda sana, lakini amekusaliti na ukaamua ku move on, uamuzi hapa ni juu yako ukiamua kurudiana naye ni sawa, kwakuwa unapaswa kuusikiliza moyo wako, (Usihofu hatutakucheka!)na ukiamua kuachana naye pia ni sawa.

Wakati mwingine maishani kuna kipindi cha 'kujaribu maisha' hii ni pamoja na kuingia kwenye mahusiano ukitaka kuona 'kuna nini hapa na pale' kabla hujafanya maamuzi ya mwisho ya kuwa na mtu wako maisha wa kufa na kuzikana.

Ndiomaa utakuta mtu mwanzoni anaringa anakuwa haeleweki lakini ukimpa muda, baada ya miezi au miaka kadhaa, mtu anarudi kwamba yuko tayari. Sina hakika kama yeye alikuwa na mawazo haya.

Umesema umemsamehe na unaendelea na mambo yako, Ila usiwe mnafiki, kama kweli umeamua kuendelea na maisha yako, basi achana naye na wala usitake kujua au kufuatilia mambo yake.

2) Pili amekuomba msaada, je umsaidie ama usimsaidie?
Umetangaza hapa kwamba UMEMSAMEHE, kama kweli umesamehe, na kama ombi lake la msaada liko ndani ya uwezo wako, unapaswa kumsaidia. Kumsaidia hapa haina maana kumrudia, yaani unamsaidia na baadaye unaendelea na maisha yako. Usimpomsaidia na kama kweli ipo ndani ya uwezo wako, maana yake bado hujamsamehe, na unataka kumkomoa, kulipiza kisasi ili naye apate shida.

Wakati mwingine Mungu anatufundisha mambo kupitia changamoto hizi za maisha tunazokabiliana nazo katika maisha yetu. Kupitia wewe kumsaidia utakuwa umemfundisha jambo muhimu sana maishani, kwamba kwasababu zozote zile usimdharau mtu, na pia kuwa mkweli kwa watu. Usipomsaidia na ukaendelea na mambo yako wewe na yeye hamtakuwa tofauti.
 
KWENYE MASUALA HAYO HAKUNAGA MSAMAHA...
KESHO KUTWA AKIRUDI TUKIO LITAJIRUDIA
WATAKUJA TIANA KIBIRITI
HUYO MWANAMKE KAPIGIKA NDY ANATAKA KURUDI
HUYU MLETA MADA ASONGE MBELEEE TU

OVA
 
Kwa kuwa amekutafuta kwasababu ana shida na anaomba msamaha ili tu umsaidie. Ushauri wangu ni Achana nae tena mwambie kabisa siwezi kukusaidia kwasababu ulitupa jongoo na mti wake.
 
Mzee wewe kaa kimya wala usijbu na jiangalie sana maana mtu uliyempenda anachance kubwa sana ya kuweza kukushawishi na kukuingiza tena kwenye mambo ya hoyo halafu unajuta baadae
2, Mjibu sina uwezo wa kukusaidia kwisha kazi
 
Jamani,huyu jamaa bado anampenda huyu mwanamke na atamsaidia na atatupwa tena,muacheni apambane na hali yake..ila kwa maelezo yake inaonekana mwanamke hakumpenda jamaa,alikuwa tu hajakutana na mtu wake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…