Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu unaota ,akimsaidia ni kwa mtaji upi?Kuna mambo mawili hapa ambayo watoa maoni wengi naona kama wanayachanganya,
1) Kwanza ni je urudiane naye ama la?
Hili ni juu yako, usikilizie moyo wako unasemaje, umelalamika kwamba ulimpenda sana, lakini amekusaliti na ukaamua ku move on, uamuzi hapa ni juu yako ukiamua kurudiana naye ni sawa, kwakuwa unapaswa kuusikiliza moyo wako, (Usihofu hatutakucheka!)na ukiamua kuachana naye pia ni sawa. Wakati mwingine maishani kuna kipindi cha 'kujaribu maisha' hii ni pamoja na kuingia kwenye mahusiano ukitaka kuona 'kuna nini hapa na pale' kabla hujafanya maamuzi ya mwisho ya kuwa na mtu wako maisha wa kufa na kuzikana. Ndiomaa utakuta mtu mwanzoni anaringa anakuwa haeleweki lakini ukimpa muda, baada ya miezi au miaka kadhaa, mtu anarudi kwamba yuko tayari. Sina hakika kama yeye alikuwa na mawazo haya.
Umesema umemsamehe na unaendelea na mambo yako, Ila usiwe mnafiki, kama kweli umeamua kuendelea na maisha yako, basi achana naye na wala usitake kujua au kufuatilia mambo yake.
2) Pili amekuomba msaada, je umsaidie ama usimsaidie?
Umetangaza hapa kwamba UMEMSAMEHE, kama kweli umesamehe, na kama ombi lake la msaada liko ndani ya uwezo wako, unapaswa kumsaidia. Kumsaidia hapa haina maana kumrudia, yaani unamsaidia na baadaye unaendelea na maisha yako. Usimpomsaidia na kama kweli ipo ndani ya uwezo wako, maana yake bado hujamsamehe, na unataka kumkomoa, kulipiza kisasi ili naye apate shida.
Wakati mwingine Mungu anatufundisha mambo kupitia changamoto hizi za maisha tunazokabiliana nazo katika maisha yetu. Kupitia wewe kumsaidia utakuwa umemfundisha jambo muhimu sana maishani, kwamba kwasababu zozote zile usimdharau mtu, na pia kuwa mkweli kwa watu. Usipomsaidia na ukaendelea na mambo yako wewe na yeye hamtakuwa tofauti.
on nimekuelewaMapenzi yaliyo ya ajabu huyo Mwanamke utamrudia kimwili mmeachana ila kiroho bado msamehe maisha yaendelee.
mmhMkuu unaota ,akimsaidia ni kwa mtaji upi?
Dont confuse love na sympthy kama ambavyo wengi wanaingia huo mtego.
okUnyama unyama tu.
SUKAH
nimekuelewaJamani,huyu jamaa bado anampenda huyu mwanamke na atamsaidia na atatupwa tena,muacheni apambane na hali yake..ila kwa maelezo yake inaonekana mwanamke hakumpenda jamaa,alikuwa tu hajakutana na mtu wake!
Ok nimekuelewaMzee wewe kaa kimya wala usijbu na jiangalie sana maana mtu uliyempenda anachance kubwa sana ya kuweza kukushawishi na kukuingiza tena kwenye mambo ya hoyo halafu unajuta baadae
2, Mjibu sina uwezo wa kukusaidia kwisha kazi
Sijamaanisha kuwa amsamehe na warudiane bali amsamehe na yeye aendelee na maisha yake lakini aondoe vinyongo moyoni mwake......kama yupo kwenye nafasi ya kumsaidia amsaidie kibinadamu....KWENYE MASUALA HAYO HAKUNAGA MSAMAHA...
KESHO KUTWA AKIRUDI TUKIO LITAJIRUDIA
WATAKUJA TIANA KIBIRITI
HUYO MWANAMKE KAPIGIKA NDY ANATAKA KURUDI
HUYU MLETA MADA ASONGE MBELEEE TU
OVA
Ushauri gani unautaka? Una akili kweli wewe? Hilo sio la kuomba ushauri. Achana naye [emoji817]%. Yeye wakati anakuacha na maneno na dharau juu alikuonea huruma? Wewe ni mjinga, acha ujinga.Jina lake linaanzia na M ni binti wa kaskazini mwa Tanzania mwenye level ya diploma katika upande wa elimu.
Ni binti nilie mpenda kutoka moyoni, shida zake zote zilikuwa zangu niliakikisha anakuwa happy muda wote.
Nikaenda kujitambulisha kwa wazazi wake ndugu na jamaa zake, nikaanza kuweka mikakati ya kutaka kumuoa.
Mwaka jana binti akadai anataka kwenda kusoma (kuongeza elimu) nikakubali kwa shingo upande sana sana sana (maana ada sikuwa nalipa mimi, ni wazazi wake), nilikubali uku nikiwa naona penzi na mipango ya ndoa ndio inaingia mchanga (kwa waliopita vyuoni nadhani mnaelewa ofu iliyokuwa inanitawala),
Binti akafika chuo mwaka wa kwanza hapa hapa jijini DASILAMU mabadiliko yakaanza kwenye semieter ya kwanza katikati, kiburi kikaanza, binti hakawa tena hataki mawasiliano na mimi, nikaanza kupata wakati mgumu sana maumivu ya kichwa juu ya penzi ilo yakaanza, ikabidi niingie chimbo kuanza kuchunguza ili niwe na majibu ya uhakika, loh salaaalee...binti kumbe alishapata mtu mpya chuoni, binti nikawa simuambii kitu tena akanisikiliza, binti nikawa simpigii simu akapokea, simtumii sms ikajibiwa, siku ya tarehe 14/02/2021 aliniambi ivi "WEWE NINI UMESAHAU KWANGU MBONA UJIONGEZI, EBU SEMA KUNA ULICHO ACHA NIKUPATIE ILI USIWE UNANITUMIA SMS NA KUNITAFUTA KWA SIMU ZAKO, NAOMBA NISEME IVI SIKUTAKI ILI UELEWE KAMA UMESHINDWA KUJIONGEZA NA WAAMBIE WOTE WANAOJUA MAHUSIANO YETU ITS OVER NOW NA WAAMBIE NDUGU ZAKO WASINISUMBUE PIA" nilibaki nimebung"aaa kama nimepigwa na shoti za umeme, nikatamka neno moja tu moyoni "mungu najua ntapita kwenye tanuru ili, na kila kitu juu ya aya maisha yangu unayo wewe, nashukuru umenibariki sana kufika hapa ngoja nifanye kazi kwa bidii ntapata wa kunifaa" Mawasiliano yakaishia hapo japo kwa maumivu makali mnooo.
Ilipita miezi kadhaa....Napokea simu kutoka kwa M akidai anataka tuongee, nikamsikiliza ilikuwa ni simu ya kutaka kuniomba msamaa kwa kilicho tokea, anadai ata yeye haelewi nini kilimpata (nikaona izi ni soud tu za mabinti wa kileo) nikamuambia tu sawa nilisha kusamehe muda tu na nakutakia kila lenye heri kwenye maisha yako na mtu wako mpya..
Ni binti ambaye maumivu yake bado yanaishi kwenye kumbukumbu ya maisha yangu mpaka ivi sasa,
Nadahani mnaelewa dunia ya sasa bila connection mambo yanakuwa magumu sana, nashukuru mungu mimi naishi vizuri sana na watu tofauti tofauti kwenye sector nyingi nina watu ambao kama ikitokea changamoto falani naweza wafata wakanisaidia kwa uharaka zaidi, na uyo binti analielewa ilo kabisa ameshapata changamoto nyingi uko nyuma ila nilikuwa natumia connection za watu nilio nao kusolve kwa uharaka kabisa.
Sasa uyu binti kwa sasa anasumbuliwa na changamoto flani flani amabyo anadai kama isipokuwa solved kuendelea kwakwe kwa shule kutakuwa na changamoto kubwa sana, iyo changamoto yake kwangu haitachukua ata siku mbili kuisolve kama nikichukua jukumu ilo la kumsaidia,
Baada ya kupata changamoto iyo kwa sasa ndio amekuwa akinitafuta na kuniomba niwe msaada wake.... sijawai kujibu sms zake ambazo kila akituma lazima aniombe nimsaidie kwenye ilo tatizo, sijawai pokea simu zake maana najua ataanza tu kunielezea ilo tatizo na mimi sikutaka kushughulika na mambo yake kwa sasa maana yupo kwenye mahusiano mengine.
Je wangwana wana jamiiforum wenzangu, watu wangu wa nguvu ambao tumeshawai kupitia changamoto za kuumizwa na walio tuumiza kesho wanataka msaada wetu mnashaurije kwenye ili maana bado nina kidonda moyoni
Note: nilikaa nae kwenye mahusiano miaka 4.
Karibuni kwa mawazo yenu wana JF.
Mkuu pale hakuna penzi, kama ni kumsaidia heri msomeshe dada yako, atakushukuru zaidi maishani.
wanawake mnapenda sana hurumaMsaidie tu ka unatoa sadaka ila usirudiane, haya maisha tu you never know one day atakuja kukusaidia na wewe
Mkuu sawaSijamaanisha kuwa amsamehe na warudiane bali amsamehe na yeye aendelee na maisha yake lakini aondoe vinyongo moyoni mwake......kama yupo kwenye nafasi ya kumsaidia amsaidie kibinadamu....
Kweli kabisahawa viumbe hawasomekangi kabisa, mpotezee tu, atakuletea mabalaa mengine.
Kweli kabisaUshauri gani unautaka? Una akili kweli wewe? Hilo sio la kuomba ushauri. Achana naye [emoji817]%. Yeye wakati anakuacha na maneno na dharau juu alikuonea huruma? Wewe ni mjinga, acha ujinga.
Jamani,huyu jamaa bado anampenda huyu mwanamke na atamsaidia na atatupwa tena,muacheni apambane na hali yake..ila kwa maelezo yake inaonekana mwanamke hakumpenda jamaa,alikuwa tu hajakutana na mtu wake!
Jambo la mahusiano ni jambo endelevu kwenye mzunguko wa maisha ya mwanadamu.......Mkuu sawa
Ila hata kumsaidia kiubinadam aachane nayeee
Mtego huooo
Ova