- Thread starter
- #161
NotedWatu tunatofautiana sana.
Mtu alikuacha Kwa nyodo hivyo halafu bado una muda hata wa kusoma SMS zake?
Hujui ku-BLOCK?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
NotedWatu tunatofautiana sana.
Mtu alikuacha Kwa nyodo hivyo halafu bado una muda hata wa kusoma SMS zake?
Hujui ku-BLOCK?
NotedMkuu me sikushauri chochote ila naligeuzia upande wangu mimi ningefanya hivi
1.kama nilifanikiwa kumsamehe hata kama sijamsahau namsaidia shida yake kama iko ndani ya uwezo wangu, kisha nafunga vioo achukue 50 zake sina muda wa kumbloku wala nini
Itabidi niishi kwa nidhamu sana mazoea nae sitaki(mazoea hasa ya mapenzi nitamuuliza pia kama kuna kitu kasahau kwangu mbona ajiongezi kama sina muda nae), atakua mshikaji tu kama washikaji wengine
2.kama sijasamehe [emoji23][emoji23] hakuna rangi ataacha iona aisee tena kajileta mwenyewe, siku zote ndege mjanja huangukia tundu bovu na hakikisha haji kunisahau kamwe
Mwendo wa kupiga pale panapouma mpaka akimbie mwenyewe asilete mazoea tena
Jino kwa jino [emoji23][emoji23][emoji23]
Msaidie kama mtu mwingine wa kawaida but usirudishe uhusianoJina lake linaanzia na M ni binti wa kaskazini mwa Tanzania mwenye level ya diploma katika upande wa elimu.
Ni binti nilie mpenda kutoka moyoni, shida zake zote zilikuwa zangu niliakikisha anakuwa happy muda wote.
Kweli, amsaidie halafu asimkumbushe chochote kwamba hoo nilikupenda sana, mara unanikumbuka kwa shida, toa msaada halafu kausha. Kwa kumfanyia mtu wema aliyekufanyia ubaya unapata thawabu mara dufu.Kwahiyo anakukumbuka katika shida tu? Zikisha tatulika mambo yakiwa sawa anarudia matapishi. Hawa viumbe bana, sasa kama alileta dharau kabla akijua wazi wewe una msaada mkubwa kwanini alifanya vile?
Lakini kama umewiwa kumsaidia kibinadamu tu fanya ila siyo urudishe habari za kusameheana msaidie kumfanikishia Jambo lake kisha songa mbele.
Umesema wa mkoa gani? 😀
Mpe block moja ya hatariNimepokea kwa mikono miwili, shukrani.
Ataleta mazoeaKweli, amsaidie halafu asimkumbushe chochote kwamba hoo nilikupenda sana, mara unanikumbuka kwa shida, toa msaada halafu kausha. Kwa kumfanyia mtu wema aliyekufanyia ubaya unapata thawabu mara dufu.
Sasa huyo si utoto mie na jamaa yangu kanifanyia mambo worse but we chat na nimesamehe na nimemtendea wema yeye ndo anaumia wakati Nina amani. Mpenzi wako hata ka numeachana kumkomoa kisa misunderstood huwa naona lack of maturity.Ila kusema ukweli inataka moyo Sana. Mtu kama humtaki kwa nini usimuambie tu kistaarabu akaelewa kuliko kuvurumisha maneno namna hiyo.
Kama wangeachana kwa wema unafikir jamaa hata angekuja kuomba ushauri amsaidie au laa.
Lakini unaona tatizo ni approach ya binti kumuacha jamaa ilikuwa kama vile hakuna siku atamuhitaji tena kitu ambacho kiubinadamu jamaa imemgusa Sana.
Bro mimi nahisi nina kisasi cha upendo, mtu kama huyo nitamsaidia sana, lkn mwisho wasiku nitamwachia deni la maumivu akijiadhibu mwenyewe na sio mimiKAMA UNACHOSEMA KINA UKWELI!!!
BASI ACHANA NAYE MKATIE LINE
ACHANA NAYE WALA USIPOKEEE
SIM YAKE AU KUJIBU SMS ZAKE
ova
Yes! Kibinadamu tu!Kwahiyo anakukumbuka katika shida tu? Zikisha tatulika mambo yakiwa sawa anarudia matapishi. Hawa viumbe bana, sasa kama alileta dharau kabla akijua wazi wewe una msaada mkubwa kwanini alifanya vile?
Lakini kama umewiwa kumsaidia kibinadamu tu fanya ila siyo urudishe habari za kusameheana msaidie kumfanikishia Jambo lake kisha songa mbele.
Sijakuelewa unaposema Bongo bila connection ni ngumu, kwenye issue gani sasa? Kwani huyo binti anahitaji msaada wa kiuchumi au ni issue nyingine tu muhimu?Jina lake linaanzia na M ni binti wa kaskazini mwa Tanzania mwenye level ya diploma katika upande wa elimu.
Ni binti nilie mpenda kutoka moyoni, shida zake zote zilikuwa zangu niliakikisha anakuwa happy muda wote.
Nikaenda kujitambulisha kwa wazazi wake ndugu na jamaa zake, nikaanza kuweka mikakati ya kutaka kumuoa.
Mwaka jana binti akadai anataka kwenda kusoma (kuongeza elimu) nikakubali kwa shingo upande sana sana sana (maana ada sikuwa nalipa mimi, ni wazazi wake), nilikubali uku nikiwa naona penzi na mipango ya ndoa ndio inaingia mchanga (kwa waliopita vyuoni nadhani mnaelewa ofu iliyokuwa inanitawala),
Binti akafika chuo mwaka wa kwanza hapa hapa jijini DASILAMU mabadiliko yakaanza kwenye semieter ya kwanza katikati, kiburi kikaanza, binti hakawa tena hataki mawasiliano na mimi, nikaanza kupata wakati mgumu sana maumivu ya kichwa juu ya penzi ilo yakaanza, ikabidi niingie chimbo kuanza kuchunguza ili niwe na majibu ya uhakika.
Kumbe alishapata mtu mpya chuoni, binti nikawa simuambii kitu tena akanisikiliza, binti nikawa simpigii simu akapokea, simtumii sms ikajibiwa, siku ya tarehe 14/02/2021 aliniambi ivi "Wewe nini umesahau kwangu mbona ujiongezi, ebu sema kuna ulicho acha nikupatie ili usiwe unanitumia sms na kunitafuta kwa simu zako, naomba niseme ivi sikutaki ili uelewe kama umeshindwa kujiongeza na waambie wote wanaojua mahusiano yetu its over now na waambie ndugu zako wasinisumbue pia" nilibaki nimebungaa kama nimepigwa na shoti za umeme.
Nikatamka neno moja tu moyoni "mungu najua ntapita kwenye tanuru ili, na kila kitu juu ya aya maisha yangu unayo wewe, nashukuru umenibariki sana kufika hapa ngoja nifanye kazi kwa bidii ntapata wa kunifaa" Mawasiliano yakaishia hapo japo kwa maumivu makali mnooo.
Ilipita miezi kadhaa.
Napokea simu kutoka kwa M akidai anataka tuongee, nikamsikiliza ilikuwa ni simu ya kutaka kuniomba msamaa kwa kilicho tokea, anadai ata yeye haelewi nini kilimpata (nikaona izi ni soud tu za mabinti wa kileo) nikamuambia tu sawa nilisha kusamehe muda tu na nakutakia kila lenye heri kwenye maisha yako na mtu wako mpya..
Ni binti ambaye maumivu yake bado yanaishi kwenye kumbukumbu ya maisha yangu mpaka ivi sasa,
Nadahani mnaelewa dunia ya sasa bila connection mambo yanakuwa magumu sana, nashukuru mungu mimi naishi vizuri sana na watu tofauti tofauti kwenye sector nyingi nina watu ambao kama ikitokea changamoto falani naweza wafata wakanisaidia kwa uharaka zaidi, na uyo binti analielewa ilo kabisa ameshapata changamoto nyingi uko nyuma ila nilikuwa natumia connection za watu nilio nao kusolve kwa uharaka kabisa.
Sasa uyu binti kwa sasa anasumbuliwa na changamoto flani flani amabyo anadai kama isipokuwa solved kuendelea kwakwe kwa shule kutakuwa na changamoto kubwa sana, iyo changamoto yake kwangu haitachukua ata siku mbili kuisolve kama nikichukua jukumu ilo la kumsaidia,
Baada ya kupata changamoto iyo kwa sasa ndio amekuwa akinitafuta na kuniomba niwe msaada wake.... sijawai kujibu sms zake ambazo kila akituma lazima aniombe nimsaidie kwenye ilo tatizo, sijawai pokea simu zake maana najua ataanza tu kunielezea ilo tatizo na mimi sikutaka kushughulika na mambo yake kwa sasa maana yupo kwenye mahusiano mengine.
Je wangwana wana Jamiiforum wenzangu, watu wangu wa nguvu ambao tumeshawai kupitia changamoto za kuumizwa na walio tuumiza kesho wanataka msaada wetu mnashaurije kwenye ili maana bado nina kidonda moyoni
Note: nilikaa nae kwenye mahusiano miaka 4.
Karibuni kwa mawazo yenu wana JF.
Yes!Isafishe nafsi yako kwa kuachia msamaha na alama ya mtu aliyesamehe ni kuwatendea wema wale waliotukosea......
Wanadamu ni viumbe wenye kubadilika badilika ndio maana hata Mungu anatuasa kuwa tunakubaliana jambo basi kuwe na mashahidi kwa kuwa kiumbe mwanadamu ana kawaida ya kubadili maamuzi......
Kama yeye amekubadilikia ndivyo ambavyo pengine na wewe ungembadilikia.....
Kama umeamua kumsamehe na kuendelea na maisha mengine basi hupaswi kumuwekea kinyongo na kama jambo lipo ndani ya uwezo wako wewe msaidie kwani Mungu pekee ndiye anayelipa wema na sio mwanadamu........
Kukubali kumsaidia kutatoa tafsiri kuwa umesamehe na kumsahau na umeamua kuendelea na maisha yako bila ya yeye na uwepo wako mbele ya macho yako haukupi shida...
Kukataa kumsaidia kunakutafsiri kuwa bado una kinyongo na upo kwenye mateso makali baada ya kuvunjika kwa mahusiano yenu...........
Vaa uanaume, jitoe kwenye tope la visasi na chuki achia upendo na ubinadamu na hiyo ndio fimbo na funzo kwa watesi wako.......
Yes! Nafurahi kukutana na comment zenye akili kama hizi.fata hii njia toa msaada kama mtu ambae hamjuani ili usikumbuke maumivu yyte then usifate yale atakayo yeye wanawake wana
self defense yao ya kugawa penzi ili kukusaulisha yale magumu aliyokueleza tambua bado anamegwa na huyo jamaa ake
wa chuo ila ww kama kijana smart msaaidie then pita hiviiiii...bila kukubali tena rushwa yake ya ngono...utanishukuru baadae