Alinikataa kaja kunikubali baada ya kupata mtoto

Alinikataa kaja kunikubali baada ya kupata mtoto

Huyu jamaa ananikumbusha dem nltongoza mwaka 2018...nltongoza dem amenizid umri..kipindi hiko ana miaka 29...!!akanikatalia....!!nikapotezea...!!mwaka huu nkasema nitest naona kila nisemacho ni Ndiioo...ndiiooo...!!hapo ujue ana miaka kama 34...!!
 
ahahaha... mkuu haujaoaa
 
Ndugu yangu kuoa ni mtihani...kukaa na binadam ndan inahitaji Moyo saaana
ahaha... halafu mkuu nilichogundua.. hawa viumbe wakishaitwa mama ndo wanajipendekeza.. maraa my... baby... baba watoto.. Sweetbert ..
na huku mtot hata si wa kwako..
wakiwa hawajazaa wanajiona keki.. ila baada ya kuzaa sis pia tunasema hatutumii vitafunwa..
 
Mwaka 2012-2015 nilikuwa nchi jirani kwa mjomba wang (yaani kwao mamaangu) nikiendelea na masomo yangu..

Kulikuwepo dada mmoja.. kwa jina ngoja nimpe jina la fatuma .. for privacy.
huy mdada nilitokea kumpenda ghafla.. ilibidi nimwambie ukweli kuhusu hilo. ila alinikatalia na kunipotezea. pindi nilipomwambia kuhusu hilo swala ananichikia na kuniambia maneno yasiyofaa.. alikua mature enough.

Nilijizatiti kwa kipindi cha miaka miwili lakini sikufanikiwa kumpat.
mwaka 2015 nilimuacha huko nchini kwao nikarudi huku chini Tanzania na kuendelea na masomo yangu..
2016-2018 nilikuw nimemaliza elimu ya sekondari..o levo.

Siku moja ndani ya mwaka 2019 mwezi wa tatu. mama alikuwa ameenda katika biashara zake na bahati nzuri hakufanikiwa kurudi nyumbani .. muda ulienda ikabidi alale huko ajiandae na safari ya kurudi nyumbani kesho yake..

Alipokuwa kwenye ule mji.. alimkuta mdada mmoja mrefu mwembamba mweupe akiwa na mtoto mchanga akiwa pale anamnyonyeaha katoto kake keupe kazuri.. mama akamuulizia baba na mama wa familia ile(mji ule).. mama alizoea kuenda pale kupereka bidhaa zake pale..

Maongezi ya kujuana yaliendelea kwa dakika kadhaa.yule mdada alijitambulisha na kusema mimi naitwa fatuma .. natoka Nchi jirani.. kabila fulani..
mama akamuuliza tena.. '"unakaa wapi pale ......(mama alimuuliza sehemu ya mtaani kwao huku alikotoka).. kumbuka huko ndiko kwao mamaangu.

Mama akamuuliza tena.. umesoma shule gani pale (St Joseph's.. fatuma alijibu).. ""mmmmm.... jamani popote pale pana ndugu'" mama alisema maneno hayo baada ya kujua fatuma ni jirani yake kwa kule nchini kwao..

"" vip unamfahamu ngotho??"" mamaangu alimuuliza maana shule niliopelekwa ndo alisomea pia huyo fatuma..(yaani tumesoma shule moja)
"" ndiyo namfahamu, yeye ndo alikuwa akiongoza darasani kila mara, alikuwa mtulivu sana yule mkaka"" fatuma alijibu.
""mimi ndo mamaake ngotho""
mshangao ulikuw mkubwa sana baada ya fatuma kusikia swala hilo (mimi ndo maaamake)

Kesho yake kwenye saa nne asubuhi.. mama akanipigiia simu.. akaniuliza kama namfahamu fatuma. Nikamuuliza (fatuma gani unaongelea mama??) mama akampa simu .. sikuamini mpaka pale nilipoisikia sauti yake na kunikumbusha mambo ya nyuma ikiwemo kuhusu ..nilivokuwa naongoza darasani.

Kuanzia hapo mazungumzo yalipamba moto, kwan nilikuwa nikikumbuka uzuri wake kipindi tunasom, nikijua bado yupo vilevile. siku baada ya siku tuliwasiliana .

Ulipofika mwezi wa saba 2019 . nilisitisha mawasiliano kwa sababu niliingia shuleni na kuanza elimu ya advance.. naye akarudi kwao.. nchini kwao. .hapo tayari nishajua ana mtoto .. tena ni wa kike ndani ya miaka miwili hatuongei wala nini..
mwaka huu mwezi wa tano baada ya kumaliza shule.. kidato cha sita ..
nikaja huku dareselam kwa mjomba..

Tarehe 22/7/2021. ilikuwa saa moja jioni. nikaona namba ngeni ikipiga..
nilipokea ile simu na kutulia bila kuongea.. naye alitulia bila kupiga ""ellow"" kwa sekunde kama kumi na tano.
nikakata samu.. akapiga tena .. nilivopokea akaanza kufkoka..( we mbona unapokea simu ya halafu huongei??) daah.. nikasikia sauti ta kike.. nikasema..
samahani dada.. namba ngeni naomba ujitambulishe..

Alijibu kwaakasema ""Mungu akipanga binadamu hawezi kupangua"" alijibu kwa maneno hayo akataj jina lake kwa kuhesabu herufi za jina lake.. ""FA
TU MA""

Ndugu zangu nilifirahi hasa pale aliponiambia et yupo dareselam. .. kuna shule ya mtu binafsi amepata fursa ya kufundisha hapo...

Huyu mdada ananipenda kweli .. yaan kweli..
cha kushangaza ananiambia kuhusu uchumba .. et ananiomba msamaha kwa kunikatalia miaka ya(2012-2014) akijitetea eti bado hakuwa mature to engage kwenye mahusiano..

Lakini kwa sasa ana mtoto mmoja japo amemuacha huko kwao ana bibi yake..
wiki iliyopita aliniuliza kuhusu mamaang.. (vip my, mama hajambo? Naomba namba zake nimsalimie mamaang huyo.) bila shaka nilimpa na waliongea.
juzi jumamosi akaniuliza..
( vip mpenzi wangu.. mama anajua nini kuhusu mimi na wewe??)?

Wakuu.. huyu mdada yupo tayari kukutana na mimi muda wowote.. maana kilani ninachomwambiA hajawahi kukataa..
wiki iliyopita nilimwambia tukutane weekend, alikubali kwa roho safi ila cha ajabu pesa ilinipiga chenga maana tunakaa mbali kidogo hapa dareselam..

Ukiangalia, ndo kwanza naingia chuo mwezi wa kumi mwaka huu.. najiuliza vip baada ya miaka mitatu c atakuwa mmama kabisa??

Yeye anasema tuvumiliane maana amekubali kunivumilia mpaka nimalize chuo.. yaani mpaka 2024.
anasema et nimwambie mamaangu et yule mtoto ni wangu ili ikitokea tumeoana.. taarifa isijulikane mno.
wakuu naombeni ushauri juu ya huyu mdada..
natanguliza shukran..
Iyo nchi jirani nahisi ni Mambasa, anyway acha utoto huyo mwanamke hakufai, kaliona bwege lakulikamatisha ni wewe na kwel ww ni bwege tena bwege sio pole pole.
 
mwaka 2018 alikuwa na miaka 29 alafu leo ni mwaka 2021 ana miaka 34 [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Huyu jamaa ananikumbusha dem nltongoza mwaka 2018...nltongoza dem amenizid umri..kipindi hiko ana miaka 29...!!akanikatalia....!!nikapotezea...!!mwaka huu nkasema nitest naona kila nisemacho ni Ndiioo...ndiiooo...!!hapo ujue ana miaka kama 34...!!
 
Hadi namaliza kusoma nimegundua huyo dada amekuzidi uwezo wa kufikiri mara mbili au tatu zaidi yako. Shida yako ni kumuoa huyo dada au shida yako ni kuloweka utambi wako?

Unaambiwa ukubali kuwa mtoto ni wako unajua madhara yake kwenye familia yako siku ikija kubainika uliwadanganya, utaonekana wazi kuwa UMEOLEWA wewe.

Unataka kuloweka utambi au KUOA?
Muoe tu lakini ni ujinga kuwadanganya ndugu zako kuwa yule mtoto ni wako siku wakijua ukweli manake lazima watajua tu utakuja kuonekana bwege wa kiwango cha lami.
 
Muoe tu lakini ni ujinga kuwadanganya ndugu zako kuwa yule mtoto ni wako siku wakijua ukweli manake lazima watajua tu utakuja kuonekana bwege wa kiwango cha lami.
Nani bwege? Unajua uliyem-qoute au umedhamiria?
 
Hadi namaliza kusoma nimegundua huyo dada amekuzidi uwezo wa kufikiri mara mbili au tatu zaidi yako. Shida yako ni kumuoa huyo dada au shida yako ni kuloweka utambi wako?

Unaambiwa ukubali kuwa mtoto ni wako unajua madhara yake kwenye familia yako siku ikija kubainika uliwadanganya, utaonekana wazi kuwa UMEOLEWA wewe.

Unataka kuloweka utambi au KUOA?
Yani dogo ndo kamaliza A level, wenzake wako bize na maandalizi ya kwenda vyuoni yeye yuko bize na mke wa Mtu...

Dunia inaenda kwa kasi sana
 
we nenda pima oil ila kuoa hapana. Ni nafasi yako.pia kulipiza.
 
Yani dogo ndo kamaliza A level, wenzake wako bize na maandalizi ya kwenda vyuoni yeye yuko bize na mke wa Mtu...

Dunia inaenda kwa kasi sana
ahahhhhhaha.... mkuu ahahhaha... sio kwamba nipo busy na mke wa mtu...
yaan huyu mdada ametoka kenya na kuja hapa bongo .. dareselam a.. ananiletea mapenzi ambayo sijui hata yametokea wapi..
yaani kila mara ananiita mara mume wangu... baby wangu... mara ooo nakupenda....
ila kinachonishangaza ananiita et baba watoto...
ahhha.. yaani
 
Wakenya wamemla 0712 huyo ndio maana anamihemko sana.
 
Back
Top Bottom