Aliondolewa 2022, karudishwa tena 2024! I’m confused

Aliondolewa 2022, karudishwa tena 2024! I’m confused

Usimlaumu Rais kutenguwa baadhi alio wachaguwa na kuwateuwa wengine hiyo ndio kazi yake Rais. Walaumu wale wanaompa ushauri mbovu wa kuwachaguwa hao anawao teuwa kuwapa uongozi halafu baada ya muda mfupi tu anawatenguwa na kuwateuwa wapya.
Ndiyo, Rais anapaswa kulaumiwa kwa kufanya Maamuzi yasiyofaa kama haya. Kwa nini kila wakati anapokea na kukubali ushauri mbovu kwa kuwateua Watu wasiofaa kwenye nafasi za Uongozi? Endapo kama hafurahishwi na suala la kupewa ushauri mbovu, Je, ametoa adhabu gani kwa hao Watu ambao wamekuwa wakimpatia ushauri mbovu??
 
Late jpm, alikuwa na watendaji wazuri kwa kiasi fulani, mf. Kalemani, huyu akirudishwa hakuna ubaya wowote, tena akapewa wizara/shirika pasua kichwa kama TTCL,endapo aliimudu Tanesco mbovu ya wakati ule, kipi kitamshinda?
Yule alitolewa kwa visasi vya makundi.
 
Palagamagamba Kabudi aliteuliwa [na Rais Samia] kuwa waziri wa sheria na katiba Aprili 2021.

2022 akaondolewa kutoka kwenye hiyo Wizara.

Leo/ jana, huyo Palamagamba Kabudi kateuliwa tena kuwa waziri wa katiba na sheria.

Hivi nyie mnamuelewa kweli huyu Rais tuliyenaye?

Kama Kabudi aliondolewa kwenye hiyo wizara hiyo 2022, maana yake ni kwamba hakufaa.

Nini kilichobadilika toka hiyo 2022 mpaka kupelekea yeye kurudishwa tena?

Oh well, labda ni mimi tu na hii elimu yangu ya fom foo ndo sielewi kinachoendelea.

Mnaoelewa, nielewesheni.

Pia soma:News Alert: - Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya
Kipindi kile wakipewa ukiranja kuwasimamia mawaziri, "aliwavuta" Ikulu. Ni kama vile walipandishwa vyeo.

Huu uteuzi wa sasa ndiyo sijauelewa kama wamepandishwa au wameshushwa vyeo.
 
Tuliambiwa anapewa kazi maalumu ya ushauri ikulu, yaani alinyang'anywa uwaziri ili kuwa mshauri maana yake hawa mawaziri siyo washauri wa rais.
Mawaziri wapo hapo kama formality tu na Signatories ila behind the scene sio decision makers wala advisors mana Nao wanatamani Kiti Kikuu, Leo uwafanye washauri watu wanaotamani nafasi yako si hatari hio mkuu? Mtu kama Mwigulu au January wanakesha kuwaza kiti chako leo uwafanye washauri wako,
Watu wanaomshauri Rais hawapo hata kwenye Political space, they are there quietly
 
Kwanza TANZANIA TUNA WASOMI WASIO KUWA NA AKILI KICHWANI HATA KIDGO HYO KABUDI KWAO KILOSA HOVYO WATU HAWAMKUBALI SANA
 
Wale wazee walikengeuka, tukawaweka pembeni kwa muda ili wajitafakari. Baada ya kujiridhisha wamejirekebisha basi tukawarudisha.
Katiba yetu haizuii hili.
 
Biteko tanesco kaimudu
Afadhali BITEKO amepunguza kero za umeme kuliko January Makamba.
Since Prof. Muhongo my best perfomer, the guy (Makamba) performed worst like never before.
 
Afadhali BITEKO amepunguza kero za umeme kuliko January Makamba.
Since Prof. Muhongo my best perfomer, the guy (Makamba) performed worst like never before.
Yule jamaa sio tanesco tu unakumbuka kwe mafuta kila mwisho wa mwezi sheli zote zinaishiwa mafuta
 
Sio Kabudi tuu wapo kibao, Akina Makonda, Hapi, Lukuvi nk nk
Hawa viongozi wetu sijui ubongo wao huwa unawaza nn...yaani mtu aliyeonekana hafai miaka michache nyuma na kuwekwa kando leo anarudishwa tena kwenye uongozi utadhani hakuna watanzania wengine smart wa kuhudumu ktk nafasi hizo?!.
Huwa tunaongozwa na kikundi kidoogo cha watu wajinga kbs tunaowaita WAHESHIMIWA!!.
 
Akifanya uteuz anasikia rahaa iyo wizara ya sheria afute tz hakuna haki utapeli mtupu
 
Palagamagamba Kabudi aliteuliwa [na Rais Samia] kuwa waziri wa sheria na katiba Aprili 2021.

2022 akaondolewa kutoka kwenye hiyo Wizara.

Leo/ jana, huyo Palamagamba Kabudi kateuliwa tena kuwa waziri wa katiba na sheria.

Hivi nyie mnamuelewa kweli huyu Rais tuliyenaye?

Kama Kabudi aliondolewa kwenye hiyo wizara hiyo 2022, maana yake ni kwamba hakufaa.

Nini kilichobadilika toka hiyo 2022 mpaka kupelekea yeye kurudishwa tena?

Oh well, labda ni mimi tu na hii elimu yangu ya fom foo ndo sielewi kinachoendelea.

Mnaoelewa, nielewesheni.

Pia soma:News Alert: - Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya

Amehamishwa leo
 
Sio Kabudi tuu wapo kibao, Akina Makonda, Hapi, Lukuvi nk nk
Hawa viongozi wetu sijui ubongo wao huwa unawaza nn...yaani mtu aliyeonekana hafai miaka michache nyuma na kuwekwa kando leo anarudishwa tena kwenye uongozi utadhani hakuna watanzania wengine smart wa kuhudumu ktk nafasi hizo?!.
Huwa tunaongozwa na kikundi kidoogo cha watu wajinga kbs tunaowaita WAHESHIMIWA!!.
Hii nchi Rais alikuwepo mmoja tu nae ni Marehemu Nyerere labda na Marehemu Mwinyi hawa waliofuata ni majizi tu na machumia tumbo na hayanaga akili yanaona wengine ni viwete wa ubongo.
Tanzania tuko zaidi ya 60m, wasomi wako wa kutosha sasa kinachowafanya wateuane wao kwa wao na familia zao ni nini.
Ni ushetani tu huo
 
Kwa UTEUZI wa leo atatufundisha utamaduni na michezo. Hapo vipi?
 
Back
Top Bottom