John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Ndiyo, Rais anapaswa kulaumiwa kwa kufanya Maamuzi yasiyofaa kama haya. Kwa nini kila wakati anapokea na kukubali ushauri mbovu kwa kuwateua Watu wasiofaa kwenye nafasi za Uongozi? Endapo kama hafurahishwi na suala la kupewa ushauri mbovu, Je, ametoa adhabu gani kwa hao Watu ambao wamekuwa wakimpatia ushauri mbovu??Usimlaumu Rais kutenguwa baadhi alio wachaguwa na kuwateuwa wengine hiyo ndio kazi yake Rais. Walaumu wale wanaompa ushauri mbovu wa kuwachaguwa hao anawao teuwa kuwapa uongozi halafu baada ya muda mfupi tu anawatenguwa na kuwateuwa wapya.
Hmm….ingekuwa ni suala limetokea moja tu, si ishu.
Lakini ni suala linalojirudia rudia….
Kuna tatizo mahali.
Mara hii hamzungumzii Tena kuwa Urais ni TAASISI. Yaani kubadili maneno tu ili mkidhi Nia zenu ambazo sina hakika kama ni njema.She is showing how incompetent and confused she is now. She need Loyal people's to her,no more no less
Duh hii iko kwenye Physics, Chemistry au Biology. Definitely haiko kwenye Maths, ila ina sound vizuri.The more things change, the more they stay the same...
Yule alitolewa kwa visasi vya makundi.Late jpm, alikuwa na watendaji wazuri kwa kiasi fulani, mf. Kalemani, huyu akirudishwa hakuna ubaya wowote, tena akapewa wizara/shirika pasua kichwa kama TTCL,endapo aliimudu Tanesco mbovu ya wakati ule, kipi kitamshinda?
Kipindi kile wakipewa ukiranja kuwasimamia mawaziri, "aliwavuta" Ikulu. Ni kama vile walipandishwa vyeo.Palagamagamba Kabudi aliteuliwa [na Rais Samia] kuwa waziri wa sheria na katiba Aprili 2021.
2022 akaondolewa kutoka kwenye hiyo Wizara.
Leo/ jana, huyo Palamagamba Kabudi kateuliwa tena kuwa waziri wa katiba na sheria.
Hivi nyie mnamuelewa kweli huyu Rais tuliyenaye?
Kama Kabudi aliondolewa kwenye hiyo wizara hiyo 2022, maana yake ni kwamba hakufaa.
Nini kilichobadilika toka hiyo 2022 mpaka kupelekea yeye kurudishwa tena?
Oh well, labda ni mimi tu na hii elimu yangu ya fom foo ndo sielewi kinachoendelea.
Mnaoelewa, nielewesheni.
Pia soma:News Alert: - Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya
Uhusiano kati ya Mwabukusi kuwa Rais wa TLS na Kabudi kuwa waziri wa sheria, ni upi?Unakuwa na rais wa TLS Kama mwabukusi au Lisu utafanyaje? Kabudi nguli wa sheria unamuwekaje pembeni
Mawaziri wapo hapo kama formality tu na Signatories ila behind the scene sio decision makers wala advisors mana Nao wanatamani Kiti Kikuu, Leo uwafanye washauri watu wanaotamani nafasi yako si hatari hio mkuu? Mtu kama Mwigulu au January wanakesha kuwaza kiti chako leo uwafanye washauri wako,Tuliambiwa anapewa kazi maalumu ya ushauri ikulu, yaani alinyang'anywa uwaziri ili kuwa mshauri maana yake hawa mawaziri siyo washauri wa rais.
Afadhali BITEKO amepunguza kero za umeme kuliko January Makamba.Biteko tanesco kaimudu
Yule jamaa sio tanesco tu unakumbuka kwe mafuta kila mwisho wa mwezi sheli zote zinaishiwa mafutaAfadhali BITEKO amepunguza kero za umeme kuliko January Makamba.
Since Prof. Muhongo my best perfomer, the guy (Makamba) performed worst like never before.
Palagamagamba Kabudi aliteuliwa [na Rais Samia] kuwa waziri wa sheria na katiba Aprili 2021.
2022 akaondolewa kutoka kwenye hiyo Wizara.
Leo/ jana, huyo Palamagamba Kabudi kateuliwa tena kuwa waziri wa katiba na sheria.
Hivi nyie mnamuelewa kweli huyu Rais tuliyenaye?
Kama Kabudi aliondolewa kwenye hiyo wizara hiyo 2022, maana yake ni kwamba hakufaa.
Nini kilichobadilika toka hiyo 2022 mpaka kupelekea yeye kurudishwa tena?
Oh well, labda ni mimi tu na hii elimu yangu ya fom foo ndo sielewi kinachoendelea.
Mnaoelewa, nielewesheni.
Pia soma:News Alert: - Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya
Hii nchi Rais alikuwepo mmoja tu nae ni Marehemu Nyerere labda na Marehemu Mwinyi hawa waliofuata ni majizi tu na machumia tumbo na hayanaga akili yanaona wengine ni viwete wa ubongo.Sio Kabudi tuu wapo kibao, Akina Makonda, Hapi, Lukuvi nk nk
Hawa viongozi wetu sijui ubongo wao huwa unawaza nn...yaani mtu aliyeonekana hafai miaka michache nyuma na kuwekwa kando leo anarudishwa tena kwenye uongozi utadhani hakuna watanzania wengine smart wa kuhudumu ktk nafasi hizo?!.
Huwa tunaongozwa na kikundi kidoogo cha watu wajinga kbs tunaowaita WAHESHIMIWA!!.