Kwangu huwa naagiza mchele kutoka katavi, logistics zake ni ngumu mpaka unifikie, sasa nikiishiwa mchele before sijatumiwa mwingine naanza kuhangaika na huu wa masokoni, nanunua kidogo walau 5kg nisikilizie mzigo wangu ufike.
Kwa muda nikitumia huu mchele wa masokoni nikagundua kuna kitu hakiko sawa, Kupika wali ni jambo rahisi sana, ila huu nimejitahidi kupika kila namna lakini wapi! [emoji23] Wali mbayaaa kama mahindi, kwanza bora hata mahindi yana ladha, haushiki mafuta, unasumbua kuiva, ukipoa unakuwa kama mbichi [emoji1787]
Watu wa nyumbani kwangu hawajali sana wao ilimradi ubwabwa, nimeteseka peke yangu until last sunday walikuja mashost kwangu, huwa wanakuja jumapili tunapika pilau ndio nikawaambia kuhusu namna gani nateseka na huu mchele ndio wakaniambia kuna mchele unaitwa mchele wa Samia, upo kila mahali na wafanyabiashara hata ukitaka mchele tofauti wanakuwa wameuchanganya na huo. Ndio nikapata kuelewa kinachoendelea aiseee nimetesekaaa! Now sipiki ubwabwa hadi mchele wangu ufike, au lah bora nipikie basmat nijue moja!