Alivyoifanya Mobutu Congo DR ndio wanavyoifanya CCM Tanzania. Ni suala la muda tu Tanzania itakuwa kama Congo

Mkuu nimekuelewa vizuri sana ila kuna kitu naona hapa nadhani hamnielewi au mnanielewa kutokunielewa ninachokisema mimi ni kwamba kule Congo M23 sio kikundi cha raia wa kawaida wenye silaha M23 ni Jeshi lenye mafunzo ya kijeshi, unanielewa sijui hapo wamejifunzia wapi hayo mafunzo mpaka wanawatia jamba jamba kila wanaosogea kuongilia mgogoro wao hilo swali usiniulize, tuje upande wetu hapa twende taratibu hivi unahisi kuna Jeshi la Tanzania ambalo litaenda kinyume na Serikali na kutaka kuipindua Serikali? Ndio maana nawaambia nyinyi mnaota sababu mnaongea na hamsemi kwanini mnaongea mnasema tu subiri subiri utaona siku sio mbali kutoka sasa hicho ndicho kitakacho waangusha mtatumia Jeshi gani kuwaangusha?
 
Unakosea sana kuifananisha serikali ya Tanzania na ile ya Mobutu. Wakati Mobutu anapendelea kijijini kwao hapa Tanzania miradi ya maendeleo imetapakaa Tanzania nzima. Kila mtanzania kafikiwa na mradi fulani huko aliko. Lucas Mwashambwa husema "Mama katufikia". Hakuna sekta iliyoachwa bila kuguswa na maendeleo.

Wakati wa utawala wa Mobutu, mwanae Kongolu "Saddam Hussein" alikuwa na nguvu karibia sawa na Rais. Koffi Olomide akiwa kwenye ubora wake alishawahi shushwa kwenye gari na kucharazwa viboko kama mwanafunzi wa shule ya msingi. Mobutu alichinja wanafunzi wengi sana ndani ya usiku mmoja huko Lubumbashi kisa kikiwa kuandamana mchana wake.

Jitahidi kutokuwa mpumbavu kwa kufananisha shetani Mobutu na Tanzania.
 
Ulikuwa unaona yanayofanyika Chato kipindi cha awamu ya 5? Unaona yanayofanyika saivi kizimkazi kipindi hiki cha awamu ya 6?

Alafu nani kakwambia Mobutu hakuendeleza maeneo mengine ya Congo?

Mwisho kuna tofauti gani kati ya huyo mtoto wa Mobutu uliyemtaja hapo na Abdul mtoto wa Mama Samia?
 
Mkuu hata DRC haikuamka siku moja na kujikuta hapo. Think nje ya box
Hizo sala zenu za kutaka TZ iwe kama DRC mngejiombea wenyewe na vizazi vyenu. Serikali ya CCM ipo imara na haiwezi kuruhusu wahuni kuleta taharuki.
 
Maendeleo yanafanyika nchi nzima ikiwemo Kizimkazi. Mobutu angeendeleza maeneo mengine angalau DRC kungekuwa na barabara zinazopitika. Abdul alishawahi shusha mtu kwenye gari na kuamuru achapwe viboko? Acha upumbavu wa kufananisha giza na nuru. Hizo dua zako za kutaka TZ iwe kama DRC hazitafanikiwa.
 
Ndiyo maana nakuita Tahira. Msuya alianza kazi lini? Alikua waziri wa biashara na viwanda na baadaye akawa Waziri Mkuu mara mbili wakati wa Nyerere na Mwinyi.

Uchumi wa Tanzania uliporomoka kikubwa zaidi baada ya Vita ya Uganda- 1978/ baada ya hapo ndiyo kukawa Hakuna pesa na baadaye shillingi kuporomoka.

Sasa Mwinyi alifanya nini? Mwaka 1992 nchi ilifirisika. Aliyeanza kuinua nchi alikua Mkapa.

Wewe unamsikiliza Zitto? Soma vitabu
 
Unaongelea maendeleo gani wakati vijijini na hadi maeneo ya mjini huko barabara ni kizungumkuti hadi watu wanapata shida kusafirisha mazao yao na bidhaa zao?

Unaongelea maendeleo gani wakati kuna shule hazina hata vyoo? Na mnajengewa hadi vyoo na wafadhili kakika karne hii huku hao mabwana zenu wa CCM wakiiba fedha za walipakodi?

Unaongelea maendeleo gani wakati ma hospitalising huko dawa ni kizungumkuti huku watu wakijinunulia ma V8 kila siku?



Unaongelea mae
 
Uzi umejieleza kwa mifano iliyoshiba. Endeleeni na hizo tabia za uchawa. Yakitimia tutakumbushana.
Chawa bibi yako

Nchi hizi mbili hazina chochote kinachofanana kwenye historia

Hatukua na mapinduzi, diktesa puppet wala division ya ukabila wala ethnicity

Our roots to stability lies on the system ambayo ni hybrid ya mkoloni pamoja na ujamaa… rarely hizo systems kucollapse

Umeangalia incidences chache ambazo if we want to equate basi hata dini, mataifa na kanda zingeshakufq because of sifa

Up your game my sister
 
Ukweli mtupu aisee! Watu wanasifu na kuabudu km mazombies!
 
Mosongo ya mfumo wa utawala ni tofauti sana

Tabia za wapambe ndio zinafanana

Who told you chawa kama akina steve Nyerere wana nguvu ya kushtua mifumo yetu?
 
Mosongo ya mfumo wa utawala ni tofauti sana

Tabia za wapambe ndio zinafanana

Who told you chawa kama akina steve Nyerere wana nguvu ya kushtua mifumo yetu?
Kwani shida ni uchawa au shinda ni nini? Kwa nini tuwe na machawa? Kwa nini watu wapewe nafasi na vyeo kwa sababu ya uchawa?
 

..Somalia dini moja, kabila moja, lakini walisambaratika.

..Tanzania tuna bahati hatujapata mpumbavu anayeamini ktk mapambano ya silaha ambaye ana wafuasi wa kutosha.

..anahitajika Mtanzania mjinga anayeamini katika vita, na atakayeungwa mkono na moja ya nchi jirani.

..M23 wangekuwa hawaungwi mkono na Rwanda wasingekuwa na nguvu kiasi hicho.

..RPF wasingeungwa mkono na Uganda wasingemletea shida Habyarimana.

..UNITA na Savimbi wasingeungwa mkono na makaburu wa Afrika Kusini vita vya Angola visingedumu kwa muda mrefu.

..Binafsi nachukia sana vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kuna mambo mengi ya msingi ya kufanya ktk ulimwengu tunaoishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…