Alivyoifanya Mobutu Congo DR ndio wanavyoifanya CCM Tanzania. Ni suala la muda tu Tanzania itakuwa kama Congo


Utawala wa Mobutu Sese Seko wa Zaire unawiana sawa kabisa kiutendaji na Utawala wa CCM uliopo hapa Tanzania.
Jinsi Vibaraka wa Mobutu Sese Seko walivyokuwa wakisifu na kumwabudu. Mobutu ndivyo hali ilivyo kwa Vibaraka wa Watawala hapa nchini wanavyofanya, hakuna tofaufi hata kidogo.
Watu wenye akili nzuri waliokataa kumsifu na kumuabudu Mobutu Sese Seko walikumbana na Visa vya kutekwa na kuangamizwa sawasawa kabisa na hali inayoendelea hapa nchini.
 
Dah Congo huruma sana…nchi ina utajiri wa kulisha bara lote la Africa…
 
Hiyo mikoa muda si mrefu itakuwa sio yetu
tumeshaongea sana humu lakini Serikali inapuuza
waahamiaji haramu ni wengi sana huku!
Hao Wahamiaji endapo kama wangeweza kusimamiwa vizuri naamini kwa dhati kabisa kwamba hawawezi kuwa tishio. Nchi ya Marekani ina Wahamiaji wengi sana, lakini kutokana na kuwepo kwa utaratibu mzuri wa utambuzi wa Watu na Mifumo mizuri ya Utawala wa nchi hiyo Wahamiaji hao wengi wao wamekuwa faida kwa nchi hiyo. Kumbuka: Hata Rais Barack Obama chimbuko lake ni Mhamiaji kutoka nchini Kenya, Rais Joseph Biden chimbuko lake ni Mhamiaji kutoka nchini Poland, Rais Donald Trump chimbuko lake ni Mhamiaji kutoka nchini Ujerumani, tajiri mkubwa zaidi duniani kwa Sasa Bw. Elon Musk pia ni Mhamiaji kutoka nchini Afrika Kusini.
 
Andiko bora la 2025. Utasakamwa lakini huo ndiyo ukweli.
 
Mnavyo iombea mabaya Tz, halafu ndio kwanza Mungu anaibariki CCM inazidi kutawala nchi, hakuna maandamano hakuna kelele wapinzani wote wameufyata wamebaki kutukanana wenyewe kwa wenyewe kisa uenyekit πŸ€£πŸ’©
Kwani kwa Mobutu ulisikia upinzani ? Kongo ilikuwa amani, miziki, mpira na starehe ya kufa mtu. Lakini watu makini, wazalendo ziro. Ndiyo maana M23 hawana upinzani wowote. Hakuna mtu wa kuionea uchungu Congo. Wababe wanamiliki misitu, migodi na raia wanakimbia na magodoro kuepuka vita.
 
This is Africa usifananishe na marekani
Sisi bado tunajitafuta!
 
Baelesee bachawa ba mama
 
N
ashukuru kumbe unafahamu mambo haya mabaya yalianzia awamu ya Nne na hayakuanzia awamu ya tano βœ…πŸ™ŒπŸ«‘
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…