Alivyoifanya Mobutu Congo DR ndio wanavyoifanya CCM Tanzania. Ni suala la muda tu Tanzania itakuwa kama Congo

Mkuu nikwambie kitu kidogo tu kwanza heshima haiuzwi popote heshima haimbwi na heshima hupewa mtu bure haina gharama yoyote naweza nikawa mtoto mdogo sana ila nikakuzidi maarifa hapo tu ndipo tunapotofautiana kwa kiasi chake na uzuri ni kwamba ninachokwambia unakielewa vizuri sana ila unakwepa kutoa jibu linaibeba hoja yako, nimekuuliza Jeshi la kuiondoa CCM linatoka wapi ambalo litaifanya Tanzania kua km Congo? Km huna jibu sema sina jibu sio unakuja na majibu ya utoto mdogo mtoto mdogo ninaekuuliza maswali yanayokuumiza kichwa hivi unafikiri historia ya Mobutu unaijua peke yako na hao wenye hio Documentary yao uchwara?
Wewe unasemea CCM itatawala miaka 200,000 ndo unizidi maarifa mimi?🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Haya kakojoe ukalale dogo
 
Mwaka 2020 niliandika uzi humu jamvini kuhusu tofauti ndogo iliyokuwepo baina ya Congo ya Mobutu na Tanzania!

Niliandika uzi ule kwa sababu kuna vitu vingi sana vilivyokuwa vinatokea wakati ule havikuwa na tofauti na mambo yaliyokuwa yanatokea nchini Congo kipindi cha Mobutu. Niliweka na Documentary waliyoiandaa wazungu inayoonesha namna Congo ya Mobutu ilivyokuwa (Nashauri wanabodi muiangalie hadi mwisho bila kuchoka na mtajifunza kitu hakika).

Labda watu hawafahamu.

Congo tunayoiona leo ya vijana kuwasifia watu wenye hela na kuwaabudu badala ya kujikita kwenye kupata maarifa ya kuisaidia nchi yao kwenda mbele iliasisiwa na aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo Mobutu Seseko Kuku wa Zebanga.

Baada ya kushika madaraka, Mobutu alitengeneza Congo ya machawa. Ilikuwa huwezi kupata cheo au nafasi Serikalini bila kuonesha unyenyekevu wako na kujipendekeza kwako kwake.

Chama chake alikiita chama dola na kuwatengeneza wa Congo kukisifu chama chake na yeye binafsi. Zilitungwa nyimbo za kumsifu, zilitengenezwa nguo zenye picha zake pamoja na kofia ambazo vijana, wamama na watu wa Congo walitengenezewa utaratibu wa kuzivaa ili kumsifu na kuonesha kuwa maendeleo ya Congo ni yeye na hakuna Congo bila yeye.

Badala ya wananchi wa Congo kutengenezwa kufikiri vizuri kwa fikra huru kwa ajili ya maendeleo yao kwa miaka mingi ijayo, walitengenezwa kuwaza maendeleo ni mtu na bila kumsifu huyo mtu mkono hauwezi kwenda kinywani.

Matokeo ya hayo ni kwamba badala ya kutengeneza vijana na watu wenye akili kwa faida ya nchi yao, walitengeneza mapooza kichwani ambao ndo walipewa madaraka na Mobutu, hivyo nchi ya Congo alishindwa kustawi na kuhimili maadui wa ndani na nje maana walioshika uongozi hawakushika kwa merit ila kwa kujipendekeza kwao kwa Mobutu na chama chake.

Hali hii ndo yanayotokea sasa nchini Tanzania, kwetu Mobutu wetu ni CCM.

Kuanzia mwaka 2012, CCM walianza kutengeneza mfumo wa siasa zilizoshika hatamu leo hii. Walitengeneza mfumo wa vijana wanaoonesha kuwapigania, kuwatetea na kuwasemea vizuri viongozi wao kupewa madaraka makubwa ya uongozi kwenye utumishi wa Umma. Hii ilianza kwa Nape baada ya kumtukana Lowasa na kuonesha kuwa chawa wa JK alikabidhiwa Ukuu wa Wilaya na baadae cheo ndani ya CCM.

Ilifuata kwa Makonda ambaye nae baada ya kuonesha kuwa chawa wa JK kwa kumsema vibaya Lowassa akazawadiwa ukuu wa wilaya.

Kubwa zaidi ni Magufuli ambaye kwenye kila hotuba za kuzindua miradi ya ujenzi alikuwa anamsifia JK mwishowe JK akaona ndo awe Rais wa Tz.

Kipindi cha JK, vijana waliokuwa vyuoni waliotengenezwa na siasa za namna hiyo walianza kuzawadiwa nafasi ya uongozi na utumishi Serikalini kama DAS, DED, DC na nyinginezo.

Alipokuja Magufuli ndo alilifanya suala hili zaidi ya alivyofanya Kikwete. Magufuli alikuwa akikuona leo umemuongelea vizuri kwenye chombo cha habari kesho yake unasikia Msigwa kakutangaza wewe kuwa DC/DED/DAS/RAS/KM au Mwenyekiti wa Bodi au Mjumbe wa Bodi. Watu waliacha kupewa vyeo kwa uwezo wao ila kutokana na uchawa wao kwa Rais na chama chake.

Matokeo yake hali hii imeendelea na kukua hadi kwenye maisha ya kawaida. Mitaani machawa ndo wanqpewa fursa, kwa wasanii wanaotunga nyimbo za kuwasifia viongozi ndo wanapewa tenda za kufanya kazi na Taasisi za Umma ili wapige hela.

Sasa hali hii imefika climax. Siku hizi fedha za umma (kodi za wananchi) zinazotengwa kwenye bajeti ya Serikali kutekeleza miradi mbalimbali zinahusishwa na mtu kusifiwa binafsi kuwa anafanya yeye. Utasikia Magufuli kafanya haya, hakuna kama Magufuli, mara Samia kafanya haya, hakuna kama Samia.

Sasaivi huko CCM kama huvai kofia yenye nembo ya SSH au Samia au nguo yenye picha ya Samia unaonekana kama sio mwenzao.

Kwa wasio na akili wanaweza kuona jambo hili ni la kawaida sana ila kwa wenye akili napenda kuwaambia hizi ni dalili rasmi kuwa Tanzaniartunaenda kuwa kama Congo.

Suala hili linaenda kudumaza sana akili za Watanzania, suala hili linaenda kututengenezea jamii iliyopo Congo leo nchini Tanzania ambayo inaamini kwenye kujipendekeza, kutukuza wenye hela hali iliyofanya Taifa lile leo kufa na kuwa shamba la bibi kwa watu wenye akili (Mataifa mbalimbali ambayo yanaliibia ikiwemo Rwanda na Uganda)

Leo hii Tanzania, Vijana ambao wanashika nafasi zinazopaswa kushikwa na watu smart na intelligent ni vijana ambao wanaamini bila kujipendekeza kwao kwa CCM na Viongozi wao wakuu wasingefika hapo. Vijana hawa hawataweza kuifanya nchi yetu kuhimili hila za maadui wa ndani na nje ambao nchi zao zinawatengeneza kwa kuwapa exposure na kuwatengeneza kuwa smart isivyo kawaida.

Vijana hawa hawataweza kutengeneza Tanzania Dream ambayo inapaswa kutengenezwa na watu wanaoshika nafasi za maamuzi kwa merit na sio uchawa. Watu wanaofanya research na kuandika mambo makubwa na kuyasimamia yawe kweli.

Naionea huruma Tanzania. Kama Vyombo vya dola havitaisaidia kuiondoa CCM madarakani. Sisi ni Congo tunaofuata.
CCM ni Adui wa tanzania
 
Wewe unasemea CCM itatawala miaka 200,000 ndo unizidi maarifa mimi?🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Haya kakojoe ukalale dogo
Kwa akili zenu hizi za kijinga jinga basi CCM itatawala na kuongoza sio miaka 200,000 hata miaka Million na zaidi mpaka akili ziwarudi yaan unakaa unaifananisha Tanzania na Congo we una akili kweli?
 
Mfano usio hai.....

Mobutu aliipindua serikali halali....

Serikali ya CCM si serikali ya mapinduzi ya kijeshi.....

Utter nonsense.
 
Mkuu kabla hujamaliza kusema kuna kitu umekisahau nikukumbushe tu

Nyuma ya Serikali ya CCM kuna Jeshi linaloilinda Serikali

Elewa maana usipotoshe maana
 
Hata. kabla ya Mobutu kupindua serikali kulikuwa na jeshi linaloilinda SERIKALI.....

CCM si zao la mapinduzi ya kijeshi....hapa ndipo ninaposimamia!
 
Tutofauti sana na kongo, walivyonavyo hatuna, na tulivyonavyo hawana,
Kongo ni kongo na Tanzania ni Tanzania,
Ccm daima
 
Hata. kabla ya Mobutu kupindua serikali kulikuwa na jeshi linaloilinda SERIKALI.....

CCM si zao la mapinduzi ya kijeshi....hapa ndipo ninaposimamia!
Mkuu Nazi...

Narudia kusema ulisahau kusema nyuma ya Serikali kuna Jeshi linaloilinda Serikali yaan hapo fanya vyovyote huruki hio ipo wazi ndio maana mwenyekiti wa CCM ndio Mkuu wa Majeshi yote Nchini maana yake unaelewa au hauelewi nikueleweshe?
 
Anawaunga Mkono M23 sababu ni Watu wa Jamii yake ni Watutsi wenzake na wanaongea Kitutsi hio ni hoja moja wapo ila mara nyinyi amekua akitetea kua sio watu wa Rwanda ni watu wa Congo

Na bado unasema sio Ukabila?
Kama ni watu wa Congo yeye kinamuwasha nini?
 
Wako bukavu soon wataingia kwa wakata mauno na kujichubua
Wawanyoooshe,na wale wakishika nchi wataibadili mindset ya wakongo

Ova

Hatari Sana Mkuu.
Kama Jeshi la Congo litasalimu Amri itawarahisishia Sana. Lakini tofauti na hapo patachafuka vibaya.
 
Anawaunga Mkono M23 sababu ni Watu wa Jamii yake ni Watutsi wenzake na wanaongea Kitutsi hio ni hoja moja wapo ila mara nyinyi amekua akitetea kua sio watu wa Rwanda ni watu wa Congo
Wanaongea Kitutsti? Ndiyo kilugha gani hicho?
 
Kwa akili zenu hizi za kijinga jinga basi CCM itatawala na kuongoza sio miaka 200,000 hata miaka Million na zaidi mpaka akili ziwarudi yaan unakaa unaifananisha Tanzania na Congo we una akili kweli?
Katika kuzalisha Chawa mleta mada yuko sahihi kabisa, Tanzania haina tofauti na DRC katika hilo. Kama haulioni hilo it means hauna akili hata kidogo.
 
Muda upi wewe acha ndoto zako za Mchana umeshakula kwanza au njaa inakusumbua?
Watu Kama wewe wapo/ walikuwepo tangu enzi za mitume wa Mungu ndio walio kua watesi wa YESU KRISTO na Mtume Muhammad.

So unaweza fanya unacho fanya Ila moyoni kumbuka hivi vitu.

* Maternich system.
Kama kwa bahati mbaya ungezaliwa mwaka 1821_1848 Austria.

Mtawala akiwa chancellor Clemens von Metternich. AMBAE for three decades alikalia kiti Kama chancellor of Austria. He was a conservative statesman alikua very conservative.

Matternich alikua na mfumo Dola na aliweza kuanzisha his spying system "matternich system" watu waliogopa hata kuongea UOVU wa serikali yao hata wakiwa peke yao chooni.

Hawa watu waliogopa,/ na ingekua enzi za matternich era baadhi humu tusinge kua tunaandika hata Kama ni anonymous identity

Watu ambao walizaliwa kwenye matternich era ilikua ukiwa ambia Kuna siku SERIKALI dhalimu ya matternich itaangushwa wangekukatalia kabisa ni kama wangekwambia upo kwenye nightmare.

Kwa CCM yenu kuto kusoma alama za nyakati na mahitaji ya jamii kwa Sasa ndicho kitakacho waangusha na sio mbali kutoka Sasa.
 
Back
Top Bottom