Wenye akili huzingatia kila tahadhari na kuchukua hatua stahiki kufanya marekebisho. Walio shiba kodi za Wadanganyika kupuuza kila ushauri. Kuna serikali zimewahi kuanguka na zilikuwa imara kuliko Tanganyika mara 10. Uzalendo haupo tena. Wananchi wanaofukuzwa na askari, mgambo nk no kwa kuuza bidhaa zao na hawana ajira ni rahisi mno kumuunga mkono mvamizi. Wahitimu mamilioni wasio na ajira hawana uzalendo tena ni rahisi kutumika. Naiogopa vita, nilikuwepo vita ya Uganda na Tz 1978-1980. Simpendi Kagame kama ukoma, but Tanzania ilipofikia Mungu tu apishe mbali. Mmasai aliyefukuzwa Loliondo anapata wapi uzalendo. Ndugu wa aliyepotezwa,, kupigwa risasi au kufungwa kisiasa anapata wapi uzalendo. Watoto genius wako mtaani hawana ajira, na watoto wa Viongozi wamejazana TRA na BOT, uzalendo utoke wapi ?