Aliye mfano wa mwanadamu aketiye katika Kiti cha enzi Mbinguni ni nani?

Nimeuliza swali kwenye thread, pia unaniuliza swali🤔

Sasa hii ni ELIMU Gani!!
Kujibu swali kwa swali ni Socratic method. Hata Yesu alijibu swali kwa swali.

Unaweza kuthibitisha mbingu ipo?
 
Enoko...

.. Kutembea na Mungu ...
Habari za Enoko kutembea na Mungu ni mfululizo wa visa-asili vya 'mbari chotara' za wanadamu na 'Wana wa Miungu'...


View: https://www.youtube.com/watch?v=ztJOt9W56cI
Metatroni...

Habari za Metatroni ni kisa-asili cha 'Mageuzi' na 'kupaa mbinguni' kufika kwenye 'kiti cha enzi' na kuwa mshirika wa Ukuu na Utukufu-mhifadhi wa 'Uwepo' katika mapana yote dhahiri na nyakati... Halafu kutoka kwenye simulizi la kitabu cha Enoko, Ishmaeli kupaa mbingu sita--kufanya 'sala' katika mbingu ya sita ili astahili fadhili na rehema za 'mbingu ya Saba' ya utukufu wote...


View: https://www.youtube.com/watch?v=jt5AKyj5kWI
Hivi ni visa 'ILIMU'... Si kwamba ni matukio yalitokea huku ama kule; ila kwa namna ya ajabu, ni kama vile matukio 'yanaoendelea' daima kuwa 'SASA'.

Yantra Dhamma ni ufunguo wa ufunuo wa 'ILIMU'...

Alama za 'chakra ajna' na 'swastika katika 'Hash'--ndani ya makatizano mistari wima na ulali ndiyo muktadha wa habari za 'Malaika'--malaika na umalaika ndani ya mtu yeyote aliyekatika rizayati ya Elimu 3.0: Kwesti...


Mistari miwili miwili ya wima na ulali kukatizana, kufungamanisha na 'nyota ya Daudi' katikati ya Yantra Dhamma ni asili ya 'Torati'...

Torati maana yake ni miongozo...

Yantra Dhamma ni mkusanyiko wa 'funguo za hekima na ufunuo' wa dini zote kuu duniani hivi sasa Juni 2024.

Kwa namna hii 'Rizayati ya Elimu 3.0' ni maandalizi ya 'Kiutamaduni' kwa wanadamu wote ili wapate kujinasibu na ILIMU.

Kutumia Uono na Ufikirifu Mifumo, ILIMU ni metafizikia ya 'Elimu'... Ni matayarisho, nidhamu na vitendo kwa ajili ya 'Ufunuo' kwa mtu mmoja mmoja; si tena habari za 'dini za kimakundi' na 'ibilisi wa kujitenga'...

Katika 'uwepo' ni 'ugani usio na mwanzo wala mwisho--ugani wa kikwantumu'; nilipo mimi ndipo ulipo wewe, walipo wao ndipo nilipo mimi, nilipo mimi ndipo wao-ulipo wewe...

Kuinuka 'Mbingu Sita' ndiyo basi habari za 'vitovu sita vya mizunguruko ya unishati uwepo'; chakra ni neno la kihindi, kisanskriti lenye kumaanisha 'kujizungurusha kinishati' kama tuseme ilivyo kwenye 'kimbunga'... Kwenye kisa cha Ishmaeli ndiyo topografu ya 'jicho na pete zinazojizungurusha' kumshuhudia 'Ishmaeli' akikwea na kupaa mbingu moja hadi ingine...

Mer-Ka-Ba ya Enoko, Ishmaeli na Malaika wengine ni mambo ya 'Swastika' na 'Chakra Ajna' kwa 'Nyoka wawili wenye kujisokotea Juu' hadi kuishia kwenye kitovu cha Sita na 'kukazia macho' kitovu cha 'kumbukumbu la Uzima, Dhahiri na Mbingu zote zenye kutangulia 'mbingu ya Saba'...

Kwenye Yantra Dhamma, mambo haya ya 'malaika' ndiyo huwasilishwa na alama ya 'chakra ajna' na 'swastika' kuwa katika mstari ulali wa 'Torati'; torati ambayo ni usambamba wa 'Mbingu na Nchi'. Nchi yawa na 'Ujazi na Liberti' pale ambapo 'Nia ya UTU' ina 'U-Moja na Utangamano'...

Utimilifu wa Torati ni 'Dhamma'.

Yantra maana yake 'chombo'--instrumenti; Dhamma ni 'Utamaduni katika Utaamuliko'; Yantra Dhamma ni ufunguo wa rizayati ya Elimu 3.0 kwa ajili ya 'Utamaduni katika Utaamuliko'.

Utamaduni katika Utaamuliko ndilo kwa hapa duniani, ni ahadi ya 'Mbingu Mpya, Nchi Mpya'...

Ni katika 'Uwepo' ndivyo watu wa 'Ufunuko' walipata kufahamu 'Mambo ya Nyakati' na hata kusema 'Watarudi'...

Kiufundi unabii na ufunuo ni mambo ya Elimu 3.0; habari zake zinatafsiri na mapelekeo tofauti kwa akili na ufahamu wa kawaida wa 'akili ya nyama'... Kwa mfano, mtu wa akili ya nyama ana ile asili ya 'kudhani anajengwa na matukio'; hivi sivyo kwa ILIMU -- katika vilele vya ufunuo 'mtu hupotea' na kutamka yeye ni 'Mungu'... Kwa kuwa katika 'Uwepo' ni 'Roho ya Ufahamu wa Yote' -- kikomo ni ulinganifu wa ufahamu wa kawaida wa mtu 'asiyeinuliwa katika ufunuo kamili'.

Mambo ya Elimu 3.0 daima yamekuwa ni faragha ya wachache... Hii ni kwa kuwa ulimwengu kwa mapana yake ni hasimu kwa 'Nuru na Utukufu wa Kweli' wa 'Roho ya Uzima wote'--japo ni kwa juu juu tu. Kwa mfano, kumekuwa na miiko na kula yamini kwamba baadhi ya kweli zinzopatikana katika 'Rizati ya Elimu 3.0' zisisemwe hadharani na tena kwa hadhira isiyo na 'maandalizi'.

Hili bado lina 'hekima yake'; lakini kuna yale ambayo sasa, katika wakati na zama, siyo lazima yabakie ni 'siri' za 'Wandani' wa mambo ya intrigi za ufahamu...

kitovu cha katikati cha Yantra Dhamma ni kigoda cha mageuzi ya kiutu--kutoka kuwa 'mtu wa nchi' kuja kufanyika 'mtu wa mbingu'. Kwa kadiri ya 'Pumzi Takatifu' mtu 'huinuliwa' katika 'Utukufu' na 'Daraja' kupitia 'Fanusi Malaika'... Fanusi Malaika ndiyo habari za 'NENO' ama 'Majina 99 ya Allah'. Mtu yeyote mwenye 'Hekima' akichunguza majina 99 ya Allah atabaini ni mafumbo imani ya 'UTUKUFU' na tena yanakadirisha 'Unyoofu na Mapenzi Mema' katika 'UTU timilifu katika wongofu'.

Siri ya NENO na Majina ya UTUKUFU ni 'Uwepo' na 'Malaika'... Kristu ni 'NENO'; neno la Uzima...

Kristu ni NENO -- ni ufahamu; mtu yeyote katika rizayati sahihi anakuwa 'Kristu' -- Kristu kwa kadiri ya uweza wake kushikilia 'chaji' ya utukufu na uweza katika 'uwepo'. Siku za mbele, haya ndiyo mambo yatakayokuwa yakiendelea kwenye vituo vyetu vya Utamaduni--kujengea wanajamii uweza wa 'kushikilia chaji' ya utukufu na uweza.

Kwa hivi, kiufundi mambo kama vile Hijja na Kuzunguka Ka'aba ni rizayati ya Elimu 3.0 kwa 'daraja fulani'. Kuzunguka Ka'aba ni jambo lenye asili ya 'kuishinda KUBU ya ulimwengu wa madhahiri'.

Kuzunguruka Ka'aba ni topografu ya 'kujitia chaji' ya ajili ya 'kupaa mbinguni'. Ni 'ibada' ya 'kumshinda Shetani'; katika ILIMU moja ya mashauri ya siri sana ni ukweli wa dhahiri yote ya mwanadamu kuwa ni ulimwengu wa maanguko--himaya ya Shetani.

Kupaa Mbinguni ni mambo ya 'kumshinda Shetani'--ulimwengu wa majaribu ambavyo mwanadamu hujichagulia fahari ya nchi ama mbingu...

Kutwaa miili na kuwa mwanadamu pia yaweza kutafsiriwa kama 'Malaika' kushuka chini na kupambana na 'mfitini' wa 'mbingu na nchi'--Shetani.

Ni kupitia rizayati ya Elimu 3.0 ndiyo 'Vita/Mapambano' haya 'hufunuka' ukweli wake--visa vyote vya masimulizi na mapokeo, ya kiimani na maandiko ni 'utundu wa sanaa' ili kutia chachu ya mwanadamu kuutafuta ukweli--ukweli kwenye kumuweka mtu huru kweli kweli--Liberti.

Kwa hivyo, Ka'aba, kwa uono na ufikirifu mifumo, hushahibiana habari na mapelekeo ya falektori ya 'Musa' kwa wana wa Israeli... Walioagizwa na Marabbi kuzivaa mikononi na kujifunga kwenye mapaji ya nyuso zao...


View: https://www.youtube.com/watch?v=__ww6x0Rq8M
Karne ya 21, sasa 'Trizaniamu' na 'Yantra Dhamma' vinarudia drama ile ile 'Musa' na 'Wanaisraeli' kadiri ya 'mila, desturi na utamaduni' wa nyakati--simulizi la 'Kutoka 13'--kimahususi Kutoka 13:1-10 tena 13:10-16... Vile vile 'Kumbukumbu la Torati 6:4-9' na 11:13-21...

'Kutoka' na 'Kumbukumbu' ndiyo mambo hasa ya 'KUBU ya Mageuzi' katikati pa 'Yantra Dhamma'--Mageuzi ya Kijamii katika watu waiishio 'Miongozo'; ni 'Utamaduni' na 'Mihimili ya Mageuzi'... Kiufundi, mihimili ya mageuzi ndiyo siri ya 'Malaika'... Maisha ni 'Kumbukumbu' katika fanusi ya 'Malaika'.

SASA haya yanahusika vipi na jamii yetu ya 'Mtanzania'?

Kwa mtu wa uono na ufikirifu mifumo ni rahisi kubaini kwa nini misingi ya utaifa huafata mashauri, misingi na miongozo ya waasisi wa taifa--Tanzania, misingi ya utamaduni na maisha ina mbegu ya UHURU, UDUGU, HAKI na AMANI... Mambo haya manne ndiyo hufanya mraba wa ndani wa 'Mageuzi' jamii...

Ikiwa haya yanafanya anzio la 'chaji ya mageuzi' basi kuiishi miongozo wa haya manne kupitia (1) Dhamira Sahihi, (2) Vina vya Tafsiri, na (3) Uono na Ufikirifu Mifumo basi jamii inaweza kuinuka hadi kwenye sifa na utukufu wa 'Yantra Dhamma'--Sovereini Jumuifu...

Sifa na Utukufu wa Tanzania 2.0 na 3.0 ni 'Nchi Mpya, Mbingu Mpya'

Hili linawezekana...

Tukumbuke, Tujikumbuke ili Tukumbukwe...

Hmmm
 
 
 
Biblia ni lugha ya picha, ukishindwa kuielewa, hautaelewa chochote kile ulimwenguni..
Ndio nafahamu sna tu ,kama tu hadithi ya fikiri kabla ya kutenda ilivyo na mafundisho kwa lugha ya picha
 
Usichanganye Occasion 4 Ya Story ya Ufufuko kwenye Sehemu Moja..
Kwangu Mimi wale waandishi hawajitegemei. Wanashirikiana pamoja kuelezea maisha ya Yesu duniani na ufalme wa Mungu alikuja kuueneza. Yohane amemuelezea Yesu kwenye nyanja ya neno la Mungu zaidi. Mitume wawili wameelezea matukio waliyoyaona na Kuna sehemu wanafanana. Kwa Luka yeye alikua msomi zaidi ya hao, alifanya research kuhusu maisha ya Yesu ndo akayaandika. Wote kwangu wanategemeana kuunda Injili Moja.
 
Injili Zilo Tofauti sana Mkuu..
Jaribu kuchukua Muda wako na Usome tena..
Ila kama Utahitaji Nikuelezee Occasion Zote Nitakuelezea
 
MUNGU aliufanyia ujasusi, nimecheka sana hio kauli mkuu.
 
Usidhani halijui aliloandika, anajua fika, ila anafanya Ile KAZI ya kupindisha Kweli,

Ili watu wasiijue Kweli wakatubu na kuokolewa!!

Mungu ni Mwema, anasema na mioyo ya watu direct na wataijua tu Kweli.
sijakuelewa hapa.
 
MUNGU aliufanyia ujasusi, nimecheka sana hio kauli mkuu.
Ni Ujasusi Hasa,

Neno linasema, Alikuja Kwa Walio wake, lakini Walio wake hawakumtambua.

Kwa wasiopewa uwezo wa kufungua codes, wanasema Kuna mkanganyiko!!

Huoni kuwa Yohana kumwona aliyeketi katika KITI Cha enzi Mbinguni ana mwonekano wa mwanadamu ni Ujasusi huo?

Kwamba kumbe Mungu alishuka mwenyewe katika mwili wa mwanadamu Kwa KAZI maalum Kisha akarejea kule alikokuwako mwanzo🤔
 
Kama shetani aliweza kuishawishi theluthi fulani ya malaika na wakamuasi MUNGU ten waliyekuwa nae karibu na wanamuona, je atashindwa vipi kumpoteza mwanadamu kupitia maandiko ?, anway shetani alishacheza karata zake tangu mwanzo kuwapoteza kupitia hayo maandiko, na ataenda na wengi.
 
sijakuelewa hapa.
Ukifuatilia mjadala, Kuna watu wanatumia maandiko haya haya kuwapotosha watu wasiijue Kweli,

Imagine, mtu anadai ni mkristo na haamini kufa na kufufuka Kwa Yesu, haamini uwepo na uweza wa Roho mtakatifu ambavyo vyote vimeelezwa vyema katika maandiko na anadai ni mkristo,

Unalionaje Hilo?
 
Kuna yule Mchungaji aliyetuhumiwa Kwa ulevi, Lusekelo,

Akisoma Uzi huu naamini upofu wake utamtoka kujua kuwa Yesu ndiye Mungu 🤔
 
Yesu Kristo
Wakamwambia, mama Yako na ndugu zako wako nje wanakuita,

Akawajibu mama na ndugu zangu ni akina nani? Ni Hawa wanaolisikiliza neno la Mungu.

Yeye ndiye aliyemwumba Mariam, hivyo UKWELI unabaki pale pale kuwa,

Yesu ni Mungu, Hana mwanzo Wala mwisho. Na Ufalme wake Hauna mwisho, ni WA milele.
 
Mbona swali jepesi sana hilo kama unasoma biblia

Mwanzo 1;26

"Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia"
 
Mbona swali jepesi sana hilo kama unasoma biblia

Mwanzo 1;26

"Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia"
Sasa kumbe wasiomwamini Yesu kuwa BWANA na Mwokozi wa MAISHA Yao, Wana HASARA kubwa🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…