Aliyeanzisha usafiri wa mwendokasi sidhani kama alikuwa na mpango wa kuwatesa watanzania kiasi hiki

Aliyeanzisha usafiri wa mwendokasi sidhani kama alikuwa na mpango wa kuwatesa watanzania kiasi hiki

Hatuna uwezo wowote wa kuendesha na kusimamia miradi mikubwa kwa ufanisi wapewe wazawa wa sekta binafsi wanaweza kufanya kazi angalau kwa ufanisi wa wastani wa kawaida!
 
Mardi unaokufa kwa kuzidiwa na wateja!
Hawana mabasi au wanabana kupata faida kubwa.
Watu wanakaa vituoni masaa 2, linakuja basi 1 au 3. Kimara to kariakoo au kivukoni ni Dakika ngapi?
Kimara kwenda Moroco nafikiri wana basi 2, moja linatoka Moroco na liningine Kimara, yanapishana.
 
Waafrika turudishwe enzi za mawe!, tukale mizizi upyaa halafu uchi kitu ana kwa ana tukikimbiza mikia yetu huku tukiwatisha wanyama wengine! nafikiri hicho ndo kipaji chetu!
Kabisa, mchakato wetu wa kuwa binadamu kamili bado haujakamilika.
 
Watanzania wengi ukiwapa ajira, kitu cha kwanza wanachowaza ni jinsi gani ataiba apate utajiri aishi maisha ya kifahari, ili nae atupie picha kwenye mitandao ya kijamii atambie wenzake.

We jiulize, waziri mzima tena wa wizara nyeti, anaenda kwenye sherehe yeye na familia yake, anapiga picha chakula anachokula na mke wake, alafu anatupia kwenye mitandao ya jamii. Hiyo ni akili kweli? mbona alivyokua raia wa kawaida hakuwa anafanya hivyo?

Alafu ukiajiriwa kwenye kampuni iliyojaa wezi hapa Tanzania, ukaanza kufanya kazi kwa kunyoosha mstari, wenzako wanaona unawaharibia ulaji, wanaamua kukupiga fitna, alafu unafukuzwa, au wanakupiga sumu una rest in peace. Alafu kwenye msiba wanasema, pengo lako halitazibika.
Tanzania watu wanatafutia utajiri makazini😁 sasa ukileta kauzibe lazma unyooshwe. Watu wanapenda maisha ya kifahari ila kwa kutumia shortcuts. Utu hakuna kabisa sikuhizi watu wanapenda show offs na ni gharama kufanya show offs kwa mshahara wa laki 6 lazma ujiongeze uibe million 2 ya ziada kila mwezi
 
Ukichunguza sana unaweza kukuta aliyeanzisha mwendokasi hakuwa na lengo la kuwasaidia watanzania 🐼
Feasibility studies na objectives za miradi mingi ya kibongo huwa malengo ni kuwanufaisha watoa tender na bidders katika kila stage hadi utakapokamilika. Hapo mchakato lazima uzingatie 10% za migao watu wajenge na kununua magari ya kifahari. We unadhani watu wanawezaje kuporomosha mijengo ya aina ile Mbweni kule wakiwa ni staff tu wa serikali kama procurement officers ama Tax officers.
 
unaambiwa mradi wa mwendokasi ndio biashara ya kwanza duniani kufa kisa imezidiwa na wateja

ila mimi ninachokiona, mradi ulipoanzishwa, alipewa mtu asiye na uzoefu wa biashara ya usafiri kusimamia, halafu mate yakawatoka kwa yale manilionibya nauli yaliyokusanywa wakaona mradi ndio pa kupigia pesa

wakasahau ama hawakujua kiwa biashara ya magari japo pea inaingia lazima ulete mabasi mapya karibu kila miaka miwili walau

oneni akina abood, kila baada ya muda mfupi tu wanashisha mabasi mapya ndio maana standard yake ya huduma haishuki

serikali isihangaike kutafuta msimamizi wa huduma ya mwendokasi watafute watu toka makampuni makubwa ya mabasi huko watapata watu watakao wafundisha namna gania biashara ya usafiri inaendeshwa
 
Kabla ya kulalamika nionyeshe mradi wowote wa serikali ulio fanikiwa
 
Amani iwe nanyi watanzania

Sina uhakika huyu aliyeanzisha huu mradi wa mwendokas kama alikuwa na lengo na kutesa watanzania kiasi hiki

Na kama angejua watu watakuja kuteseka namna hii hakika asingeuanzisha

Utawala uliopo madarakani umeshindwa hata kusimamia huu mradi halafu wanataka tuwachague tena

Inauma sana kuongozwa kibabe namna hii na watu wasio na uwezo kuwa viongozi wa darasa la tano B

Mwendokas ni mateso jamani

MWENYEZI MUNGU mwenyewe aingilie huu ugomvi

LONDON BOY
Soon Mambo yatakuwa mazuri! Subira
 
Amani iwe nanyi watanzania

Sina uhakika huyu aliyeanzisha huu mradi wa mwendokas kama alikuwa na lengo na kutesa watanzania kiasi hiki

Na kama angejua watu watakuja kuteseka namna hii hakika asingeuanzisha

Utawala uliopo madarakani umeshindwa hata kusimamia huu mradi halafu wanataka tuwachague tena

Inauma sana kuongozwa kibabe namna hii na watu wasio na uwezo kuwa viongozi wa darasa la tano B

Mwendokas ni mateso jamani

MWENYEZI MUNGU mwenyewe aingilie huu ugomvi

LONDON BOY
Kumbe mnateseka nunueni yakwenu
 
Hawana mabasi au wanabana kupata faida kubwa.
Watu wanakaa vituoni masaa 2, linakuja basi 1 au 3. Kimara to kariakoo au kivukoni ni Dakika ngapi?
Kimara kwenda Moroco nafikiri wana basi 2, moja linatoka Moroco na liningine Kimara, yanapishana.
Wanawafanyia hivyo ili kupata maximum returns. Wakitumia basi moja moja kuwalundika maana diesel inatumika kidogo ila hela wanapata nyingi.
 
Nimeona mmoja huko juu kasema kaamka saa kumi na moja alfajiri, kapanda hiyo city bus saa moja tena si kupanda ni kudandia kama nyani, yaani unaamka saa kumi au Tisa Sasa unalala saa ngapi?, halafu ni ratiba ya mwaka mzima.
 
Poleni,huu USAFIRI ni mateso kwakweli.Siku hizi walau naona kuna option sio lazima upande kwa wale wanaotokea mbezi Luis.Unaweza panda zile za mwananyamala Hadi magomeni then pale ukachukua ya Posta au kariakoo.Kuna bajaji pia.
 
Ili kuondoa mgongano wa maslahi ilitakiwa serikali itoe tenda kwa watu binafsi kutoa huduma ya usafirishaji na yenyewe ipate chake na kusimamia tu waliopewa tenda kutoa huduma bora
 
Back
Top Bottom