The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Kwa nchi yetu kupuuza elimu inayohusiana na mambo ya kilimo lilikuwa kosa kubwa sana lisilosameheka.
Mikoa yote ya Tanzania ukiondoa dar salam msingi wao mkuu wa uchumi na ajira ni kilimo Kwa miaka yote.
Ukanda wetu wa majirani zetu na mataifa mengine duniani wanakabiliwa na changamoto za kiusalama, uhaba wa ardhi, ukame, hali mbaya ya hewa na kutokuwa eneo la kimkakati kama tulivyo sisi, yaani tupo mahali ambapo Kila njia ya usafiri ni rafiki.
Katika mazingira ya namna hiyo unashindwaje kukifanya kilimo kuwa ajenda kuu ya kujikomboa kiuchumi?
Ni kwa nini usikifanye kilimo kuwa ufumbuzi wa tatizo la ajira?
Ukishajijua hivyo unaondoaje somo la kilimo shuleni badala ya kuongeza uwekezaji huko ili lifundishwe kwa kina litengeneze wataalamu watakaoleta tija kwenye kilimo?
Mimi naamini katika nyakati hizi za changamoto za Russia vs Ukraine sisi tungepiga hela sana. Ni aibu sana kwa taifa kushindwa kustabilize kilimo ili kijibu maswali yote magumu ya kiuchumi.
Ndipo nadhani Iko haja ya kumtafuta mtu aliyeondoa somo la kilimo shuleni achunguzwe uraia wake na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.