Na lengo la elimu ni kujibu changamoto za wakati husika. Kwa taifa kama letu tulipaswa kuwa na maendeleo makubwa sana kwenye mambo ya kilimo ikiwa tungekuwa serious na kilimo.
Tulipaswa kufundisha kilamo na liwe somo la lazima kwa kila mwanafunzi tangia nursery hadi chuo kikuu tulipaswa watanzania wakisome kilimo kwa vitendo Tanzania ilipaswa agricultural transmissional center kwa subsahara region and the rest of the world.
Tuzalishe watafiti na wataalamu wa kutosha wa udongo, mbegu Bora, pembejeo, masoko ya ndani na nje, miundo mbinu ya kilimo cha kisasa na cha umwagiliaji, uhandisi wa mitambo na viwanda vya zana za kilimo nk. Haya yote yanatakiwa kufundishwa kwenye shule zetu zote.
Sio hivyo tu lakni serikali itenge fedha za kutosha kuifanya hii elimu kuwa ya vitendo zaidi badala ya nadharia.