Aliyefuta somo la kilimo shuleni achunguzwe uraia wake na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi

Nimesoma Agriculture Olevel bado sijaona faida yake,zaidi ya kutesa tu watoto mara kuchunga ng'ombe,bustani jembe la mkono na ujinga mwingine mwingi.
Ni somo gani ulilosima na unaweza kutuwekea faida zake hapa mkuu?
Ninachojua mimi ni kwamba lengo hasa la kusoma ni kujipatia maarifa ya kupambana na mazingira na kujiletea maendeleo kupitia hayo maarifa.
Sasa iweje wewe ukasoma bila kupata maarifa yoyote?
 
Mungai.

Miaka yetu, nyumbani na shule lazima use na kitalu cha bustani,iwe ni mboga au maua! Somo la Sayansi kilimo.

Ila kuna shule za sec watoto wanalima na kufuga

cc: weluwelu
Galanos
 
Mungai (Marehemu) japo alikuwa Mafinga ila inasemekana alitoka Kenya........ Agriculture ilikuwa somo zuri sana Kwa tuliosoma
Inauma na kuumiza sana kwani natafuta mantiki ya kufuta hili somo siioni kilimo kimetuajili kimetuzalishia chakula kimetupa malighafi za viwanda kimetupatia fedha nyingi za kigeni kwa miaka nenda rudi kwa nini uwazuie watanzania kujielimisha kuhusu kada hii muhimu?
 
Acha uongo na ujinga
2016 tangazo la kazi la maaafisa kilo, alafu kwenye kuajiriwa wakadhulumiwa?
2017 tangazo tena la kazi la maafisa kilimo, alafu kweye kuitwa kazini wakadhulumiwa?
2018 tangazo tena la kazi la maafisa kilimo, alafu kwenye kuitwa kazini wakadhulumiwa?
2019 tangazo tena la kazi alafu kwenye kuitwa kazini wakadhulumiwa?
2020 tangazo tena la kazi alafu kwenye kuitwa kazini wakadhulumiwa?
2021 February tangazo tena la kazi alaafu kwenye kuitwa kazini wakadhulumiwa?
Duhhh mkuu utakuwa uko vizuri sana kwenye kuona matangazo ya Ajira, sie wengine hatujawahi kuona hizo Ajira unazosema hapo zimetoka kila mwaka, anyway

Na pale juu umeweka picha za tangazo la 2019 lenye kuhitaji watu 3 na tangazo la January 2021 lenye kuhitaji mtu mmoja

Kwa ukubwa wa Tanzania na demand ya maofisa kilimo Kwahiyo hao watu 4 ndio wewe kwako unaita zilitoka Ajira nyingi?
 
Kwa nchi yetu kupuuza elimu inayohusiana na mambo ya kilimo lilikuwa kosa kubwa sana lisilosameheka.

Mikoa yote ya Tanzania ukiondoa dar salam msingi wao mkuu wa uchumi na ajira ni kilimo Kwa miaka yote.

Ukanda wetu wa majirani zetu na mataifa mengine duniani wanakabiliwa na changamoto za kiusalama, uhaba wa ardhi, ukame, hali mbaya ya hewa na kutokuwa eneo la kimkakati kama tulivyo sisi, yaani tupo mahali ambapo Kila njia ya usafiri ni rafiki.

Katika mazingira ya namna hiyo unashindwaje kukifanya kilimo kuwa ajenda kuu ya kujikomboa kiuchumi?

Ni kwa nini usikifanye kilimo kuwa ufumbuzi wa tatizo la ajira?
Ukishajijua hivyo unaondoaje somo la kilimo shuleni badala ya kuongeza uwekezaji huko ili lifundishwe kwa kina litengeneze wataalamu watakaoleta tija kwenye kilimo?

Mimi naamini katika nyakati hizi za changamoto za Russia vs Ukraine sisi tungepiga hela sana. Ni aibu sana kwa taifa kushindwa kustabilize kilimo ili kijibu maswali yote magumu ya kiuchumi.

Ndipo nadhani Iko haja ya kumtafuta mtu aliyeondoa somo la kilimo shuleni achunguzwe uraia wake na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.
Nakubaliana na hoja yako lakini nitofautiane na wewe kidogo kwenye muktadha wa kile unacholenga kukikafanikisha.

Kufundisha somo la kilimo mashuleni tu hakuwezi kuwa mwarobaini wa matatizo yetu ya kuhusu chakula. Vivyo hivyo kwenye mambo mengine. Mashuleni kunafundishwa masomo ya uvuvi, je uvuvi wetu umeweza kuleta tija kwenye uchumi wa taifa kama inavyostahili (ukizingatia maliasili ya uvuvi tuliyonayo)? Mashuleni kunafundishwa masomo ya kemia, je tumeweza kutengeneza madawa yetu wenyewe? Mashuleni kunafundishwa biolojia, je tulipokumbwa na janga la corona tuliweza kutengeneza kinga zetu wenyewe? Mashuleni tunafundisha somo la fizikia, ni majuzi tu kuna kabunge kamoja kaliweza hata kuhoji kwanini tunafundisha Physics wakati hata kwenye portal ya ajira ya serikali hakuna fursa za namna gania utaalamu wa shahada hiyo unaweza kutumika.

Mi nafikiri hapa tulipofikia inahitajika top down approach ili kuweza kuleta tija kwenye kwenye nyanja zetu mbalimbali. Mfano mdogo wa top-down ni jinsi ambavyo sekta ya tekonolojia ya mawasiliano ilivyoweza kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi hapa Tanzania. Hakuna aliyewahi kufundishwa somo la information technology mashuleni kabla ya miaka ya 2000. Ni mpaka pale akina Mobitel, Celtel na Vodacom walivyoingia Tanzania na mitaji yao (capital driven industries) ikachochea mabadiliko makubwa kwa namna vijana walivyoweza kujiingiza, kusoma na kujiendeleza kwenye kozi mbalimbali ili waweze kuajirika kwenye makampuni haya. Spin-off benefits za maendeleo hayo ni pamoja na hata mtandao wetu huu pendwa JF, teknolojia ya mawasiliano imweza kutengenenza fursa kibao za ajira na kujiajiri. Na ni vivyo hivyo inavyopaswa kuwa kwenye kilimo, uvuvi, ufugaji, n.k.

Top-down kwenye kilimo maana yake ni kwamba lazima wawepo watu wachache (makampuni) yatakayowekeza kwenye kilimo cha kisasa. Mkitaka tuendeshe kilimo chetu kama zamani, tutafanya hivyo: hata mimi mwaka jana nilijilimia eka zangu tano za mahindi, nikavuna, baadhi nilisaga unga na naendelea kula ugali nao, baadhi nilisaga nikauza voroba. Overall nilipata hasara maana nilijilimia kwa style ninayoijua mimi na kujitunzia kwa style niliyoiweza mimi, na nikauza kwa bei iliyokuwepo sokoni. Style hii haiwezi kumshawishi kijana aone somo la kilimo shuleni litamfaa kuliko kiuendesha bajaji. Na ni mara kumi kuendesha bajaji kuliko kulima kilimo cha namna hii. Kwani kilimo cha miwa kilombero na Kagera hakijatufundisha jambo lolote jinsi ya kuapproch kilimo chetu?
 
Hivi KIBAHA saivi CBA haipo!? Kibiti na Ruvu!?
 
Asante sana mkuu kwa huu mchango adhimu.
Naomba nikubaliane na ww kuhusu huu utaratibu unaoupendekeza isipokuwa bado nashawishika kwamba kama tungewekeza sana kwenye elimu ya mapinduzi ya kilimo kisha ikatengwa bajeti ya uhakika kuhusiana na mambo ya kilimo ilikuwa njia fupi sana ya kufikia ufumbuzi wa kudumu wa matatizo ya kiuchumi kwenye nchi yetu
 
Sasa hapa wanaosema halikuwepo, lirudishwe vipi tena?
Kuna shule maalumu za Kilimo,mfano Rungwe Secondary mkoani Mbeya kuna kaka yangu alisoma,ni shule maalumu ya kilimo,hapo kulikuwa hakuna mambo ya B/Keeping wala Commerce. Kwa sasa hiyo shule sijui kama wanaendelea na Agriculture ila kwa shule za msingi kulikuwa na somo la Sayansi Kilimo lakini kwa shule za Secondary kulikuwa na shule maalumu za Kulimo.
 
Kwa nchi yetu kupuuza elimu inayohusiana na mambo ya kilimo lilikuwa kosa kubwa sana lisilosameheka.

Mikoa yote ya Tanzania ukiondoa dar salam msingi wao mkuu wa uchumi na ajira ni kilimo Kwa miaka yote.

Ukanda wetu wa majirani zetu na mataifa mengine duniani wanakabiliwa na changamoto za kiusalama, uhaba wa ardhi, ukame, hali mbaya ya hewa na kutokuwa eneo la kimkakati kama tulivyo sisi, yaani tupo mahali ambapo Kila njia ya usafiri ni rafiki.

Katika mazingira ya namna hiyo unashindwaje kukifanya kilimo kuwa ajenda kuu ya kujikomboa kiuchumi?

Ni kwa nini usikifanye kilimo kuwa ufumbuzi wa tatizo la ajira?
Ukishajijua hivyo unaondoaje somo la kilimo shuleni badala ya kuongeza uwekezaji huko ili lifundishwe kwa kina litengeneze wataalamu watakaoleta tija kwenye kilimo?

Mimi naamini katika nyakati hizi za changamoto za Russia vs Ukraine sisi tungepiga hela sana. Ni aibu sana kwa taifa kushindwa kustabilize kilimo ili kijibu maswali yote magumu ya kiuchumi.

Ndipo nadhani Iko haja ya kumtafuta mtu aliyeondoa somo la kilimo shuleni achunguzwe uraia wake na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.
Viongozi wetu wa Afrika wanamuomba Putin asitishe vita kwasababu nchi za Afrika zinateseka kwa kukosa mahitaji muhimu kama vile chakula hasa ngano. What a shame to our Leaders?
 
Somo hili lilipaswa kuwa la lazima kwa ngazi za sekondari na msingi katika shule zote binafsi na za serikali
Ishu si kulazimisha watu.Tatizo la nchi hii tumekalili kila kitu ni kulazimishana. Muhimu ni kutengeneza "image" nzuri ya kilimo ili watu wakipende wenyewe. Mbona watu hawalazimishwi kubet,kuimba music au kucheza mpira?
 
Nakubaliana na hoja yako lakini nitofautiane na wewe kidogo kwenye muktadha wa kile unacholenga kukikafanikisha.

Kufundisha somo la kilimo mashuleni tu hakuwezi kuwa mwarobaini wa matatizo yetu ya kuhusu chakula. Vivyo hivyo kwenye mambo mengine. Mashuleni kunafundishwa masomo ya uvuvi, je uvuvi wetu umeweza kuleta tija kwenye uchumi wa taifa kama inavyostahili (ukizingatia maliasili ya uvuvi tuliyonayo)? Mashuleni kunafundishwa masomo ya kemia, je tumeweza kutengeneza madawa yetu wenyewe? Mashuleni kunafundishwa biolojia, je tulipokumbwa na janga la corona tuliweza kutengeneza kinga zetu wenyewe? Mashuleni tunafundisha somo la fizikia, ni majuzi tu kuna kabunge kamoja kaliweza hata kuhoji kwanini tunafundisha Physics wakati hata kwenye portal ya ajira ya serikali hakuna fursa za namna gania utaalamu wa shahada hiyo unaweza kutumika.

Mi nafikiri hapa tulipofikia inahitajika top down approach ili kuweza kuleta tija kwenye kwenye nyanja zetu mbalimbali. Mfano mdogo wa top-down ni jinsi ambavyo sekta ya tekonolojia ya mawasiliano ilivyoweza kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi hapa Tanzania. Hakuna aliyewahi kufundishwa somo la information technology mashuleni kabla ya miaka ya 2000. Ni mpaka pale akina Mobitel, Celtel na Vodacom walivyoingia Tanzania na mitaji yao (capital driven industries) ikachochea mabadiliko makubwa kwa namna vijana walivyoweza kujiingiza, kusoma na kujiendeleza kwenye kozi mbalimbali ili waweze kuajirika kwenye makampuni haya. Spin-off benefits za maendeleo hayo ni pamoja na hata mtandao wetu huu pendwa JF, teknolojia ya mawasiliano imweza kutengenenza fursa kibao za ajira na kujiajiri. Na ni vivyo hivyo inavyopaswa kuwa kwenye kilimo, uvuvi, ufugaji, n.k.

Top-down kwenye kilimo maana yake ni kwamba lazima wawepo watu wachache (makampuni) yatakayowekeza kwenye kilimo cha kisasa. Mkitaka tuendeshe kilimo chetu kama zamani, tutafanya hivyo: hata mimi mwaka jana nilijilimia eka zangu tano za mahindi, nikavuna, baadhi nilisaga unga na naendelea kula ugali nao, baadhi nilisaga nikauza voroba. Overall nilipata hasara maana nilijilimia kwa style ninayoijua mimi na kujitunzia kwa style niliyoiweza mimi, na nikauza kwa bei iliyokuwepo sokoni. Style hii haiwezi kumshawishi kijana aone somo la kilimo shuleni litamfaa kuliko kiuendesha bajaji. Na ni mara kumi kuendesha bajaji kuliko kulima kilimo cha namna hii. Kwani kilimo cha miwa kilombero na Kagera hakijatufundisha jambo lolote jinsi ya kuapproch kilimo chetu?
Ufahamu wako unaonekana ni mkubwa ila inashangaza kuona umeandika eti ulilima kwa staili unayojua wewe,ukauza mazao kwa style unayojua wewe,hv km unanania ya dhati na kilimo chako ulishindwa kuwatafta wataalamu wakakuelekeza kuhusu mbegu bora na kupanda kwa nafasi?

Au wewe ulikaa tu ili baadae upate cha kulaumu? Mbona hospitali huwa unajipeleka mwenyewe na hausubiri serikali ikupeleke? Hata kutafta soko baada ya kuvuna napo ulitaka serikali ikusaidie? Kila kitu serikali!! Kujiongeza hamna![emoji15][emoji15] Watanzania tunalaumu sana!
 
Back
Top Bottom