Asante kwa concern yako. Ndugu yangu watu tunatofautiana sana. Ni kweli mi nina kaufahamu kidogo kwenye mambo mengine lakini kwenye suala la kilimo ninakiri kwamba uzoefu wangu ni mdogo. Ukiniuliza kwa nini nilijilimia kivile nitakujibu kwamba I was "experimenting" with kulima lakini nilijifunza mambo mtambuka kuhusu kilimo kupitia uzoefu huu.
Jambo la kwanza nililojifunza, hata kama ningekuwa mzoefu kivipi ni vigumu sana kwa mkulima wa kawaida mmoja mmoja kuweza kunufaika na kilimo reja reja namna ile.
Jambo la pili nililojifunza, inawezekana ningeconsult wataalamu wa kilimo kungenisaidia kuchagua mbegu sahihi ya kulima, kuchagua na kutumia mbolea kwa usahihi, na kupata ushauri wa nitunze mavuno yangu kwa namna gani ili yakae muda mrefu kidogo bila kubunguliwa.
Lakini kwa bei ilivyokuwa inatembea sokoni (gunia la mahindi Tshs 40000) isingewezekana kabisa nikakiona kilimo kuwa na faida. Tayari nilishaona kwa nini kilimo chetu hakiwezi kuwavutia vijana wa leo.
La muhimu zaidi nililojifunza: only kilimo kinaweza kuleta tija iwapo kitaendeshwa ubepari zalendo: yaani makampuni machache ya kilimo yatakayowekeza kwenye vilimo mbalimbali (pengine kampuni moja kila mkoa) yatakayokuwa trusted na guaranteed na serikali kulisha watu wote wa nchi hii kupitia agricultural value chain production. Haya yanaweza kukifanya kilimo kiwe na tija (wanaweza kuregulate profitable price, kuajiri watu wengi kupitia value chain industries za kilimo husika, na hata elimu ya mashuleni kuhusu kilimo itakuwa na end goal in mind, mtoto atasoma kulimo huku akiwa ana motisha na wapi anaweza kufit kwenye maeneo mtambuka yanayohusu kilimo chetu kipya "fikirika").