Hii nchi ina mijitu ya ajabu sana. Halafu imepewa dhamana kubwa kwa Taifa.
Kwa vitendo vya hovyo kiasi hiki, hii nchi haitakuja kuwa na upendo kati ya watawala na wananchi.
Huko kwenye nchi za wenzetu, Rais akifanya mambo ya kukera, watu huweza kumrushia kiongozi wa nchi mpaka mayai, lakini Serikali haihangaiki nao. Fikiria tukio kama hilo litokee Tanzania, huyo aliyerusha yai, si watamkatakata vipande vipande!!
Bush akiwa Rais aliwahi kurushiwa kiatu na mwananchi, alikikwepa, halafu akawaambia walinzi wake wasihangaike na huyo aliyerusha hicho kiatu.
Wenzetu wanaangalia tu kama tendo lililofanywa lililenga kumjeruhi au kuonesha tu hisia? Matendo ya kuonesha hisia, hawana muda nayo. Ni yale tu yanayolenga kumjeruhi au kumwua kiongozi, hapo watapambana hasa na huyo mwovu.
Sasa huyo wa kuchoma picha ya Rais, kwani kwa kuichoma hiyo picha, Rais Samia alijeruhiwa mahali popote katika mwili wake? Au kwa kuchomwa picha yake, uhai wake utaondoka?
Ni vizuri Rais Samia akakemea mambo ya kijinga au ya kipuuzi yanayofanywa na vyombo vya dola, ambayo hayana msaada wowote kwa Taifa. Tuna mambo mengi sana ya msingi ambayo vyombo vya dola vinatakiwa kuyafanya kuliko kujihangaisha na petty issues.