Aliyehukumiwa kwenda jela miaka 2 kwa kuchoma picha ya Rais amechukuliwa na watu wasiyojulika, mpaka sasa hajulikani alipo

Aliyehukumiwa kwenda jela miaka 2 kwa kuchoma picha ya Rais amechukuliwa na watu wasiyojulika, mpaka sasa hajulikani alipo


Taarifa kutoka Mbeya ni kuwa kijana Chaula aliyefungwa miaka miwili jela kwa kosa la kuchoma picha ya Rais Samia, na baadaye kuachiwa baada ya kuhangiwa na wananchi amechukuliwa na watu wasiyojulikana toka jana Agosti 1, 2024.

Pia soma: Shadrack Chaula, aliyechoma picha ya Rais Samia aachiwa kutoka Gerezani

Mpaka muda huu hakuna mtu ambae anajua amepelekwa wapi na simu zake zote hazipatikani!

Pia soma: Aliyekamatwa kwa kuchoma picha ya Rais Samia ahukumiwa faini Tsh. Milioni 5 au miaka miwili jela

UPDATE:
Baada ya kusambaa kwa taarifa mitandaoni ikidaiwa kuwa kijana Shadrack Chaula ambaye ni Msanii wa Sanaa ya Uchoraji amepotea katika mazingira ya kutatanisha huku baadhi wakidai amechukuliwa na Watu ambao utambulisho wao haujajulikana, baba mzazi wa Shadrack, mzee Yusuph Chaula amesema ni kweli mwanaye hajulikani alipom Mkoani Mbeya.

Akizungumza na JamiiForums, mzee Yusuph amesema “Hatujui alipo mpaka sasa (Saa mbili Usiku Agosti 2, 2024), majira ya asubuhi nilijulishwa kuna watu ambao bado hatuwajui wamemchukua na kuondoka naye, namba zake hazipatikani tangu wakati huo.”

Ameongeza “Tumeshafika Polisi kutoa taarifa, tunasubiri mrejesho kutoka kwa Polisi, kesho tutafutilia zaidi. Sikuona kama ana tatizo na mtu yeyote tangu yale matatizo ya wakati ule yalipomalizika.”

Alipoulizwa kama naweza kuhusisha kilichotokea na kile kilichomtokea wiki chache zilizopita amesema “Sijui kama kuna uhusiano kwa kuwa, baada ya ile kesi aliendelea kuishi maisha yake ya kawaida.”

Julai 8, 2024, Shadrack Chaula aliachiwa huru kutoka gerezani baada ya kulipa faini ya Tsh. Milioni 5 ikiwa ni siku chache tangu alipohukumiwa kifungo cha Miaka Miwili jela au kulipa Faini hiyo kwa kosa la kutoa taarifa za uongo Mtandaoni.

Chaula ambaye ni Msanii wa Sanaa ya Uchoraji, Julai 2, 2024 alionekana kupitia kipande cha video akichoma moto picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya, alishindwa kulipa faini na kwenda jela, Wadau mbalimbali walianza kumchangia fedha kupitia Mtandao kwa nia ya kumlipia faini
inafikirisha ngoja tuone
 
Screenshot_20240707-171955.jpg
 
Kama kuna mwingine achome akiwa peke yake sio achome anajirekodi na kubandika katika mitandao ya kijamii lazima ataambia Jamhuri alikua na lengo gani Kufanya hivyo.
 
Halafu mambo kama haya wenye kimbelembele ni vinabo tu ambao hata hawajatumwa na mwenye picha kumtesa kijana wa watu.

Kuna vinuka mbupu havina kazi za kufanya vinajipa majukumu yasiokuwa yao ili tu waonekane wapo kazini na wao.

Chura Kiziwi anaweza kuwa na mapungufu mengi lakini nina hakika hawezi amrisha mateso kwa mtu kwa ajili ya maswala ya kipumbavu kama picha.
Ndugu Ngurukia , hata mimi pia naamini kuwa pamoja na mapungufu mengi ya mh. kule juu, hawezi kuamrisha hili, lakini ukimya wake juu ya haya ya utekaji na hasa ile kauli yake ya "drama za utekaji" zinanifanya akili ya kawaida kukataa.

Kwa nini asikemee haya matukio na kuamrisha wasaidizi wake au vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa wahusika na wachukuliwe hatua!!???
 
Hii gari mbona haimilikiwi na Jamhuri yetu kwa kuangalua No tuu..

Labda kibao kiwe cha kubandika na kutoa.
We jamaa utakuwa sio Mtanzania.

Hii gari ya nchi yako na inamilikiwa na Shirika la Reli Tanzania.
 
Wanaweza kumfanya chochote lakini wasisahau hapa duniani ni mapito huyu ndugu watamtesa lakini Mungu atampa haki yake.
 
Hapo ingelikuwa china au korea tusnge zungumza kihiv yaan jamaa angesha jongwa ila n Tz kwa sababu alikuwa anataka kick tumuombe awesalama tu
China hawabagui wa kunyonga, mafisadi yote yananyongwa ila huku mafisadi yanatamba tu
 
Back
Top Bottom