Aliyejaribu kumhonga baba mtu baada ya kumpa mimba binti yake, akana kosa hilo mahakamani

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Mchimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Erick Peter (39) amefikishwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi Simanjiro na kusomewa shitaka la kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari Tanzanite.

Peter amesomewa shitaka hilo na mwendesha mashitaka Mosses Hamilton mbele ya hakimu mkuu wa mahakama hiyo Charles Uiso.

Mwendesha mashtaka huyo amesema katika kesi hiyo namba 102 ya mwaka 2022 kuwa mstakiwa huyo ametenda kosa hilo kwa kumpa mimba mwanafunzi huyo wa kidato cha nne katika tarehe isiyotajwa kwenye mwezi Mei 2022.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo Erick alikana kutenda kosa hilo la kumpa mimba mwanafunzi huyo alipoulizwa mahakamani hapo na hakimu Uiso.

Mshtakiwa huyo aliachiwa kwa dhamana mara baada ya kudhaminiwa na watu wawili ya sh2 milioni kila mmoja.

Hakimu Uiso ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 4, 2022 itakapotajwa tena mahakamani hapo, kwani upelelezi wa kesi hiyo bado ujakamilika.

Upande wa upelelezi unapaswa kukamilisha vielelezo ikiwemo taarifa ya daktari na shuleni ili mshtakiwa asomewe maelezo ya awali mahakamani hapo.

Chanzo; Mwananchi
 
Acha KUTETEA UOVU.
wanawake walivyojaa humu mitaani kipi cha ajabu ambacho wanacho wanafunzi? matatizo mengine ni ya kujitakia.
Mwanafunzi na yeye ni mwanamke. Wana uhitaji wa lile jambo la wakubwa. Hivyo wakati mwingine kuwatia majaribuni wanaume. Kama una binti, ikishafikia hatua ya kulambishwa mimba, jibu siyo kumfunga mwenye mimba. dawa zuri ni kuwaweka pamoja wahisika na kujadili pamoja na kulea mtoto atakayezaliwa maana na huyo mtoto anahitaji kuwaona baba na mama.
 
Mchimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Erick Peter (39) amefikishwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi Simanjiro na kusomewa shitaka la kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari Tanzanite.

Peter amesomewa shitaka hilo na mwendesha mashitaka Mosses Hamilton mbele ya hakimu mkuu wa mahakama hiyo Charles Uiso.

Mwendesha mashtaka huyo amesema katika kesi hiyo namba 102 ya mwaka 2022 kuwa mstakiwa huyo ametenda kosa hilo kwa kumpa mimba mwanafunzi huyo wa kidato cha nne katika tarehe isiyotajwa kwenye mwezi Mei 2022.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo Erick alikana kutenda kosa hilo la kumpa mimba mwanafunzi huyo alipoulizwa mahakamani hapo na hakimu Uiso.

Mshtakiwa huyo aliachiwa kwa dhamana mara baada ya kudhaminiwa na watu wawili ya sh2 milioni kila mmoja.

Hakimu Uiso ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 4, 2022 itakapotajwa tena mahakamani hapo, kwani upelelezi wa kesi hiyo bado ujakamilika.

Upande wa upelelezi unapaswa kukamilisha vielelezo ikiwemo taarifa ya daktari na shuleni ili mshtakiwa asomewe maelezo ya awali mahakamani hapo.

Chanzo; Mwananchi
..Mbona Maelezo Hayakidhi Kichwa Cha Habari? Alitaka Kumhonga Shilingi Ngapi Mzee akatolea Nje?
 
Kuna toleo la kwanza, hebu lipitie ingawa hawakutaja kiasi cha Pesa taslimu alichotaka kuhonga mshtakiwa ila wameelezea kidogo
 
Back
Top Bottom