Uchaguzi 2020 Aliyejipanga kupora uchaguzi tunamjua, Wananchi tukapige kura kwa wingi kumkataa!

Uchaguzi 2020 Aliyejipanga kupora uchaguzi tunamjua, Wananchi tukapige kura kwa wingi kumkataa!

RockCarnegie

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2019
Posts
963
Reaction score
1,927
Kwa wananchi wote ambao miaka mitano wameathirika kwa utawala mbovu wa Rais Magufuli na chama chake, ni wakati wa kuungana kumkataa kwenye sanduku la kura!

Hofu kubwa waliyonayo wananchi ni kuporwa kwa matokeo na tume ya uchaguzi ambayo kwa mazingira ya uwepo wake na utendaji wake kwenye chaguzi zilizopita, ni wazi kuwa huamrishwa imtangaze nani, na nani isimtangaze!

Kama wananchi tunajua kura ni mali yetu ya thamani tutailinda! Ulinzi wa mali na maisha yetu ni jukumu la kila mzalendo wa kweli!

Wananchi tukapige kura kwa wingi na tulinde kura yetu ihesabiwe na itangazwe kama tulivyochagua!

Wezi wa kura tunawajue tujipange kuwadhibiti kwa mbinu na gharama yoyote, tumechoka na dharau za wezi hawa!
 
Umesema kweli kabisa, ila yatupasa kujua si rahisi kuiondoa ccm madarakani kwa sanduku la kura/makaratasi.

SIRI: Maana ya ccm ni CHAMA CHA MAPINDUZI. Si rahisi kukiondoa chama /serikali iliyoingia madarakani kwa mapinduzi kwa kutumia karatasi, SERIKALI AU CHAMA KILICHOINGIA MADARAKANI KWA MAPINDUZI, KINAONDOLEWA KWA MAPINDUZI.
 
Tuwe wakweli Watanzania wanahitaji heshima na kuthaminiwa.Haya mambo ya dharau na kiburi watawala yanachosha. Neno " Hamtashinda" baya sana halifai kwa taifa la kidemocrasia.
 
Sahihi kabisa!

Na hii ndo agenda kuu mwaka huu. Tunapiga kura kwa wingi, tunasimamia uhesabuji wa kura zetu na kuzilinda. Na mwisho tunahakikisha hatutoki vituoni hadi matokeo yatangazwe kama tulivyopiga kura.
Mwaka huu ndo mwisho wa kuvumilia ujinga. Wakitaka watuuwe sote ila vizazi miaka elfu vitatukumbuka.
 
Wezi wa kura tunawajue tujipange kuwadhibiti kwa mbinu na gharama yoyote, tumechoka na dharau za wezi hawa!
Kitu wanachopashwa kukielewa wananchi ni kwamba 'KURA' yao inathamani kubwa sana katika uhai wao na ufanisi wa taifa lao.

Mtu yeyote anayenajisi kura hiyo ni adui mkubwa anayetakiwa kushughulikiwa ipasavyo mahali popote atakapokuwa.

Wananchi wanatakiwa kuelimishwa tu kuhusu haya, hasa kuhusu kunyimwa haki yao ya msingi kabisa, ya kuwapata viongozi wanaowataka wao kwa kura zao kuvurugwa.

Hawa wanaovuruga kura vituoni ni lazima wadhibitiwe huko huko vituoni, wasiachwe kwa kufanya uharifu huo. Mtu anayevuruga kura ni lazima alipie huko huko alikovurugia hizo kura.

Ni lazima ieleweke hivyo kwa kila anayepanga kuharibu kura za wananchi.
 
Sahihi kabisa!

Na hii ndo agenda kuu mwaka huu. Tunapiga kura kwa wingi, tunasimamia uhesabuji wa kura zetu na kuzilinda. Na mwisho tunahakikisha hatutoki vituoni hadi matokeo yatangazwe kama tulivyopiga kura.
Mwaka huu ndo mwisho wa kuvumilia ujinga. Wakitaka watuuwe sote ila vizazi miaka elfu vitatukumbuka.
Nitakaa jirani na Dudley Mbowe kwenye Kituo Cha kupiga Kura tuzilinde!
 
Kiongoxi wa chama dola ataka kuendelea kuweka rekodi yake mwenyewe toka aliposhika madaraka. Alipata 100% alipothibitishwa kuwa Mwenyekiti Taifa na Mkutano Mkuu wa chama chake. Wote tu mashahidi kuwa chama chake kiliibuka na ushindi mnono wa zaidi ya 99% ktk uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wa mwaka 2019, na kuviacha hoi vyama vya upinzani.

Tumeshuhudia tena hapo juzi akichaguliwa tena Mkutano Mkuu wa chama chake kupeperusha tena bendera kwa kinyang'anyiro cha uraisi na kupata 100% kwa mara nyingine tena. Hakuna wa kumzuia kuzidi kuitunza hii rekodi inayoandikwa kwa wino wa kijani. NEC imejaa makada wa chama chake, vyombo vya dola vyote vinambeba kwa mbeleko, pengine wananchi wahamasike, waache uoga palec wanapoona haki yao ikipokwa kwa nguvu na waamke na kumzuia kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom