Kiongoxi wa chama dola ataka kuendelea kuweka rekodi yake mwenyewe toka aliposhika madaraka. Alipata 100% alipothibitishwa kuwa Mwenyekiti Taifa na Mkutano Mkuu wa chama chake. Wote tu mashahidi kuwa chama chake kiliibuka na ushindi mnono wa zaidi ya 99% ktk uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wa mwaka 2019, na kuviacha hoi vyama vya upinzani.
Tumeshuhudia tena hapo juzi akichaguliwa tena Mkutano Mkuu wa chama chake kupeperusha tena bendera kwa kinyang'anyiro cha uraisi na kupata 100% kwa mara nyingine tena. Hakuna wa kumzuia kuzidi kuitunza hii rekodi inayoandikwa kwa wino wa kijani. NEC imejaa makada wa chama chake, vyombo vya dola vyote vinambeba kwa mbeleko, pengine wananchi wahamasike, waache uoga palec wanapoona haki yao ikipokwa kwa nguvu na waamke na kumzuia kufanya hivyo.