Aliyekaa mahabusu miaka 7 kwa kukisababishia Chuo Kikuu Huria hasara, ahukumiwa

Aliyekaa mahabusu miaka 7 kwa kukisababishia Chuo Kikuu Huria hasara, ahukumiwa

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu, Marietha Milinga kulipa fidia ya Sh12.9 milioni na kifungo cha nje cha miezi sita baada ya kukutwa na hatia ya kukisababishia hasara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Milinga, amehukumiwa baada ya kukiri kosa. Alifanikiwa kulipa kiasi hicho cha fedha na atatumikia kifungo hicho cha nje.

Alikiri shtaka la kusababishia hasara katika makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi mwandamizi, Agustine Rwezile amesema mshtakiwa ametiwa hatiani, anatakiwa kuilipa Serikali Sh 12.9 milioni.

“Mbali na kulipa fidia hiyo, pia mshtakiwa atatumikia kifungo cha nje cha miezi sita,” amesema Hakimu Rwezile.

Amebainisha kuwa ametoa hukumu hiyo kwa kuzingatia maombi ya mshtakiwa kuwa ana mtoto mgonjwa na ni kosa lake la kwanza.

Awali, mshtakiwa huyo aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka 69 yakiwemo ya utakatishaji fedha baada ya kufanya makubaliano na DPP alisomewa shtaka moja la kukisababishia hasara chuo hicho.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, wakili wa Serikali, Jackline Nyantori ameiomba mahakama kutoa adhabu kwa mshtakiwa na kuzingatia makubaliano waliyoingia na DPP.

“Naomba mahakama itoe adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyu ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hii pamoja na kulipa fidia ya hasara aliyoisababishia Serikali,” amesema wakili Nyantori.

Katika utetezi wake, mshtakiwa huyo aliyekaa mahabusu miaka saba, aliiomba mahakama isimpe adhabu kubwa kutokana na kukaa mahabusu muda mrefu na ana mtoto mdogo mwenye maradhi ya saratani.

Katika kesi hiyo, Marietha na wenzake wanadaiwa kati ya Julai 2009 hadi Aprili 2011 walikisababishia hasara chuo hicho zaidi ya Sh. 500 milioni.
 
Mahakama inajali siku hizi, kupitia kwa DPP mshitakiwa unabaki huru.
 
Mahabusu miaka saba! Kuna haja ya kubadili mfumo wa upelelezi katika nchi yetu haiwezekani unapeleleza miaka saba huku mtuhumiwa akiwa Mfungwa wa Mahabusu bila kuthibitishwa hatia yake
Wapi umesoma kuwa alikaa miaka 7 kwa kuwa "upelelezi haujakamilika"?

Nilichoona mimi alikuwa na kosa la "utakatishaji fedha" ambalo, nijuavyo, halina dhamana
 
Wapi umesoma kuwa alikaa miaka 7 kwa kuwa "upelelezi haujakamilika"?

Nilichoona mimi alikuwa na kosa la "uhujumu uchumi" ambalo, nijuavyo, halina dhamana
Aliyekaa miaka 7 mahabusu kwa kukisababishia chuo hasara ahukumiwa. Kesi ilikuwa haijaanza vinginevyo isingekwenda kwa DPP.
Hicho ndicho kichwa cha habari.
 
Aliyekaa miaka 7 mahabusu kwa kukisababishia chuo hasara ahukumiwa.
Hicho ndicho kichwa cha habari.
Kichwa cha habari kipo vizuri. Kakaa kweli mahabusu miaka saba. Kwa kosa lipi?

Jibu unalipata kwenye utumbo wa habari.

Huwa sikisii, kumbuka hilo.
 
Wapi umesoma kuwa alikaa miaka 7 kwa kuwa "upelelezi haujakamilika"?

Nilichoona mimi alikuwa na kosa la "utakatishaji fedha" ambalo, nijuavyo, halina dhamana
Pamoja na hayo Mama yngu sheria zetu zina makosa hv kuna aja gani ya kumshitaki mtu kwa kosa ambalo alina dhamana wakt ushahidi bado aujakamilika ndugu zetu wengi sna wanaumia magerezani Uhamsho mwaka wa 5 na zaidi nina Jamaa yngu apoteza zaidi ya miaka 6 nae juzi kati ameachia kwa kesi kukosa ushahidi kweli jamani...
 
Wapi umesoma kuwa alikaa miaka 7 kwa kuwa "upelelezi haujakamilika"?

Nilichoona mimi alikuwa na kosa la "utakatishaji fedha" ambalo, nijuavyo, halina dhamana
...Mkuu, kwani wewe hujaisoma vizuri Post hii kwa kuanzia na Kichwa cha habari???
 
Wataalamu wa Sheria naomba kusaidiwa, ikiwa umekaa mahabusu miaka saba kisha ukahukumiwa miaka mitano. Adhabu itaanzia siku umehukumiwa au siku ulizokaa ndani bila dhamana nazo zitakuwa zinajumuishwa katika adhabu yako ya kifungo?
 
Kwakuwa ana mtoto mdogo anaemumwa saratani na ameshakaa miaka 7 gerezani nadhani angeachwa tu hiyo pesa aende akamuuguze mwanawe, tuwe na utu kidogo, ameshakiri na kujutia, aachwe tu.
_______________________________________
IG: @marble_na_granite
 
Katika utetezi wake, mshtakiwa huyo aliyekaa mahabusu miaka saba, aliiomba mahakama isimpe adhabu kubwa kutokana na kukaa mahabusu muda mrefu na ana mtoto mdogo mwenye maradhi ya saratani.
Aliyekaa mahabusu miaka 7 kwa kukisababishia Chuo Huria hasara, ahukumiwa

 
Back
Top Bottom