Aliyekuwa askofu Konde aondolewa wakfu. Fimbo, msalaba na pete yake vyaondolewa wakfu pia. Sasa atabakia kuwa muumini wa kawaida

Aliyekuwa askofu Konde aondolewa wakfu. Fimbo, msalaba na pete yake vyaondolewa wakfu pia. Sasa atabakia kuwa muumini wa kawaida

Ni nini wameamua kumdhihaki hivi.

Wameshindwa kumstahi hata kidogo mpaka wanamdhalilisha hivi.

Hivi vitu unaweza ona ni kawaida ila vinaumiza moyo.

Wao wana uhakika upi kuwa ni watumishi halali wa Bwana.
Ukitaka kulielewa hili vizuri ni kama Magufuli alivyomuondowa CAG Profesa Assad wakati hakuwa na mamlaka hayo kikatiba.

Hivyo basi Askofu wa mnyororo akishawekwa wakfu hakuna mwenye uwezo wa kumvuwa huo Uaskofu hilo halipo.

Kinachowezekana ni kumvuwa tu madaraka ya Kiaskofu kwenye dayosisi na mfano mzuri ni Askofu Mokiwa wa Anglican alivuliwa madaraka tu lakini bado ni Askofu.

Huwezi kumvuwa Jaji title yake, huwezi kumvuwa mwalimu tittle yake, kinachoendelea Konde ni bangi tu kuzidi kutuamsha kwamba dini ni biashara na hii ni vita ya kimaslahi.
 
Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde leo imetangaza kumwondolea wakfu wa Uaskofu aliyekuwa askofu wa Dayosisi hiyo, Dk. Edward Mwaikali.

Pia imeviondolea wakfu vifaa vya Kiaskofu alivyokuwa anatumia kama pete, msalaba pamoja na fimbo ambavyo alikabidhiwa tarehe 18 Januari 2018 alipowekwa wakfu kuiongoza Dayosisi ya Konde.

Uamuzi huo umefanyika leo Jumapili Juni 5, 2022 wakati wa lbada ya kumweka wakfu mrithi wake, Dk. Geofrey Mwakihaba.

Wamefikia hatua hiyo baada ya Dk. Mwaikali kugoma kuvirejesha ili vitumike kwa mrithi wake kwa mujibu wa taratibu za kanisa hilo.

Dk. Mwaikali aliondolewa madarakani tarehe 22 Machi 2022 na Mkutano Mkuu Maalum wa KKKT Dayosisi hiyo kwa kile kilichoelezwa kushindwa kuiongoza vyema.

Vitu vingine ambavyo amegoma kuvirejesha ni kiti cha uaskofu na mavazi ambavyo navyo vimeondolewa wakfu.

View attachment 2251168

Kuwa askofu tunakoelekea watu wafanye interview kuondoa upendeleo na malalamiko kwenye makanisa​

Hivyo basi Askofu wa mnyororo akishawekwa wakfu hakuna mwenye uwezo wa kumvuwa huo Uaskofu hilo halipo.
Lutheran lipo madhehebu hayalingani taratibu

Kuhusu title ya jaji unaweza vuliwa pia Tanzania pia iliwahi mvua mtu ujaji ila process yake kali inahusisha joo.la msjaji toka ndani na nje ya nchi

Alikutwa na makosa mazito akavuliwa title
Kuvuliwa hata degree waweza vuliwa zote.Mugabe alivuliwa digrii zake
 
Ukitaka kulielewa hili vizuri ni kama Magufuli alivyomuondowa CAG Profesa Assad wakati hakuwa na mamlaka hayo kikatiba.

Hivyo basi Askofu wa mnyororo akishawekwa wakfu hakuna mwenye uwezo wa kumvuwa huo Uaskofu hilo halipo.

Kinachowezekana ni kumvuwa tu madaraka ya Kiaskofu kwenye dayosisi na mfano mzuri ni Askofu Mokiwa wa Anglican alivuliwa madaraka tu lakini bado ni Akofu.

Huwezi kumvuwa Jaji title yake, huwezi kumvuwa mwalimu tittle yake, kinachoendelea Konde ni bangi tu kuzidi kutuamsha kwamba dini ni biashara na hii ni vita ya kimaslahi.
Kabisa tena bangi linavutwa hadharani na boss wao Shoo! mambo ya ajabu kabisa
 
Ndio kingereza linaitwa Lutheran

Kiswahili linaitwa KKKT yaani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
Safi San Mkuu kwa maelezo mazuri,pia ni moja kati ya makanisa yanaunda Christian Council of Tanzania yaani CCT, ambayo ni KKKT, Moravian,Babtist na mengineyo.Ila Roman Catholic ipo chini ya TEC,Walokole yaani TAG,EAGT nk nao wana Umoja wao kama sikosei unaitwa EACT
 
Wakati Paulo akilitesa kanisa hakuwa Mkristo alipobadilika kuwa Mkristo ndio akawa vizuri sana

Mwaikali katesa kanisa akiwa Mkristo
Usimlinganishe na Paulo!!
Roho wa Mungu anayefanyakazi ndani ya Mwaikali kwa kumpa Uaskofu na aliyempa Paulo Utume alikuwepo hata kabla ya Ukristo. Matendo ya Paulo (akiwa Sauli) yalikuwa mafu kuliko ya Mwaikali.
 
Roho wa Mungu anayefanyakazi ndani ya Mwaikali kwa kumpa Uaskofu na aliyempa Paulo Utume alikuwepo hata kabla ya Ukristo. Matendo ya Paulo (akiwa Sauli) yalikuwa mafu kuliko ya Mwaikali.
Tatizo la Mwaikali ni moja tu hakutengeneza base nzito ya watu wa kula nao sadaka za kondoo wa bwana.

Unapokaa kwenye ulaji mkubwa ni lazima uwe na chawa wa kutosha tu wanaishi kwenye payroll yako, hii ndio kanuni ya kudumu kwenye ulaji.
 
Mwaikali na Shoo walianza ugomvi wao tangu wakiwa chuoni kugombania wanawake.
 
Ni nini wameamua kumdhihaki hivi.

Wameshindwa kumstahi hata kidogo mpaka wanamdhalilisha hivi.

Hivi vitu unaweza ona ni kawaida ila vinaumiza moyo.

Wao wana uhakika upi kuwa ni watumishi halali wa Bwana.
Atakuwa ana maneno ya SHOMBO Sana huyu Mwaikali!
Mnyaki atakuwa alitoa maneno Ka ya Mwakyembe hadi wajumbe, wakaona isiwe taabu, wakamchinjia baharini!
 
Wewe mburula, hizo ni taarifa zinapatikana kwenye public domains. Wengine sisi ni wanasheria tumehusika kwenye cases nyingi ya taasisi mbalimbali zikiwemo za dini hivyo tunajua.

Una akili ndogo sio rahisi kuelewa mambo mengi kwa wakati mmoja.
Mwanasheria wewe principle iliopo kwenye kesi ya Donogue vs Stevenson..yenyewe inatambua uwepo wa Mungu..wewe unajifanya nani kunifanya hautambui uwepo wa Mungu...🤣🤣🤣🤣
 
Huu mgogoro ni kituko kitupu, aibu kubwa sana hii
 
Tumemaliza kazi sisi KKKT

KWA UTARATIBUU Kabisa wa Kanisa letu.

Nakushauri Ndugu Mwaikali omba msamahaa la sivyo mwisho wako sio mzuri
Pamoja na kujifanya mnamiliki Imani na bado mnamtishia maisha yake.

Hakika CHUKIZO LA UHARIBIFU LIMESIMAMA MADHABAHUNI leo
 
Mwanasheria wewe principle iliopo kwenye kesi ya Donogue vs Stevenson..yenyewe inatambua uwepo wa Mungu..wewe unajifanya nani kunifanya hautambui uwepo wa Mungu...🤣🤣🤣🤣
Kesi kutambua uwepo wa mungu hiyo ni facts ama opinion ya Judges?

Kuna Judges opinion na facts, facts hua zinaletwa mahakamani kama exhibits ama evidences, mungu alietwa mahakamani?
 
KKK (T) inachekesha sana hapa duniani.

Maswali wasiyoweza kujibu:

1. Wakfu huwa ni wa binadamu au MUNGU?

2. Kwanini Kanisa lina madeni yasiyolipika kama ya HIPC?

3. Kwanini Maaskofu hawawezi kuhamishwa Dayosisi? (Wako autonomous)

4. Kwanini Watumishi wanakosaga mishahara wakati fulani na mara nyingi?

5. Kwanini Maaskofu wengine wana muda maalum wa kutumika na wengine wanakaa hadi kustaafu kwa Kanisa hilo hilo moja?

6. Kama Kanisa limewekeza kwenye elimu kuanzia shule za awali hadi vyuo vikuu kwanini watoto wa watumishi wanafukuzwa shule kwa kukosa ada? Utumishi wa wazazi wao hautoshi kuwa dhamana ya kusoma bila ada? (kwanini wasipewe scholarship?)

7. Kama Kanisa limewekeza kwenye afya kuanzia afya ya msingi hadi ya umma (Primary to Public Health) kwa maana ya zahanati, vituo vya afya, hospitali, hospitali teule, hospitali za rufaa, hospitali za umahiri (consultant hospitals) kwanini watumishi na familia zao wafe kwa kukosa ela za medical evacuation kwenda ughaibuni? Kwanini wanakuwa ombaomba kwa ndugu, jamaa, marafiki, majirani, waumini ndiyo wawachangie?

8. Kwanini watumishi wanaoondolewa wakfu wakienda wakaanzisha Makanisa yao au Huduma zao wanafanikiwa sana? Wakfu huwa ni wa binadamu au MUNGU? Angalia Mwingira alikuwa Mwinjilisti wa KKKT, angalia Fernandes alikuwa Mchungaji wa Pentecost, angalia Moses Kulola alitimuliwa TAG akaanzisha EAGT, Gamanywa aliondoka Pentecost nk nk.

9. Kwanini asilimia 90 ya watumishi kwenye Makanisa haya ya Kimagharibi wanafanikiwa kiuchumi nje ya mfumo wanaouhubiri? Wakianzisha na kusimama kwenye Makanisa yao au Huduma zao ndipo wanapopata mafanikio makubwa na kuwa Mamilionea. Mwingira aliitangulia KKKT kuanzisha benki, Tv, Kilimo na Ufugaji Katavi, Sacoss, mgodi Arusha nk. Fernandes pia aliitangulia Pentecost kuanzisha Tv, Gamanywa naye aliitangulia Pentecost kuanzisha media..

10. Kwanini watumishi wanaotumika kwenye vituo vya Dayosisi (siyo Dayosisi kwenyewe) baadhi yao wana ugomvi wa sadaka na waumini?

11. Kwanini KKKT, Moravian (version zote mbili) na Anglikana Mchungaji au Askofu anaweza kupigwa na waumini au kufukuzwa?

Hapo juu namba 4, 6, 7, 9 na 10 wahanga wake ni watumishi walio chini kwenye vituo vya Dayosisi, siyo walio makao makuu ya Dayosisi.
Unawauliza watu wa mwilini kuhusu Ufalme wa Mungu?
 
Hawa RC sio kama hawana mauozo yao kama hawa wengine ni vile tu wao hawajaruhusu demokrasia (unasali unasepa zako hakuna maswali sijui sadaka au uongozi unafanya nini sijui) ndomaana uezi kusikia chochote lakini ukitaka kujua wakoje ww kaa na watu wa uko ndani malalamiko yapo kibao tu ila ndoivo yanaenda kichinichini hutayasikia kamwe
Jibu rahisi tu watu ni walewale sema rc padre ana ndoa Wala kuwa mtoto hivyo ni ngumu kutokea unadhizilifu wa Mali za kanisa maana viingozi wamejifungamanisha na kanisa cyo familia zao
 
Back
Top Bottom