KKK (T) inachekesha sana hapa duniani.
Maswali wasiyoweza kujibu:
1. Wakfu huwa ni wa binadamu au MUNGU?
2. Kwanini Kanisa lina madeni yasiyolipika kama ya HIPC?
3. Kwanini Maaskofu hawawezi kuhamishwa Dayosisi? (Wako autonomous)
4. Kwanini Watumishi wanakosaga mishahara wakati fulani na mara nyingi?
5. Kwanini Maaskofu wengine wana muda maalum wa kutumika na wengine wanakaa hadi kustaafu kwa Kanisa hilo hilo moja?
6. Kama Kanisa limewekeza kwenye elimu kuanzia shule za awali hadi vyuo vikuu kwanini watoto wa watumishi wanafukuzwa shule kwa kukosa ada? Utumishi wa wazazi wao hautoshi kuwa dhamana ya kusoma bila ada? (kwanini wasipewe scholarship?)
7. Kama Kanisa limewekeza kwenye afya kuanzia afya ya msingi hadi ya umma (Primary to Public Health) kwa maana ya zahanati, vituo vya afya, hospitali, hospitali teule, hospitali za rufaa, hospitali za umahiri (consultant hospitals) kwanini watumishi na familia zao wafe kwa kukosa ela za medical evacuation kwenda ughaibuni? Kwanini wanakuwa ombaomba kwa ndugu, jamaa, marafiki, majirani, waumini ndiyo wawachangie?
8. Kwanini watumishi wanaoondolewa wakfu wakienda wakaanzisha Makanisa yao au Huduma zao wanafanikiwa sana? Wakfu huwa ni wa binadamu au MUNGU? Angalia Mwingira alikuwa Mwinjilisti wa KKKT, angalia Fernandes alikuwa Mchungaji wa Pentecost, angalia Moses Kulola alitimuliwa TAG akaanzisha EAGT, Gamanywa aliondoka Pentecost nk nk.
9. Kwanini asilimia 90 ya watumishi kwenye Makanisa haya ya Kimagharibi wanafanikiwa kiuchumi nje ya mfumo wanaouhubiri? Wakianzisha na kusimama kwenye Makanisa yao au Huduma zao ndipo wanapopata mafanikio makubwa na kuwa Mamilionea. Mwingira aliitangulia KKKT kuanzisha benki, Tv, Kilimo na Ufugaji Katavi, Sacoss, mgodi Arusha nk. Fernandes pia aliitangulia Pentecost kuanzisha Tv, Gamanywa naye aliitangulia Pentecost kuanzisha media..
10. Kwanini watumishi wanaotumika kwenye vituo vya Dayosisi (siyo Dayosisi kwenyewe) baadhi yao wana ugomvi wa sadaka na waumini?
11. Kwanini KKKT, Moravian (version zote mbili) na Anglikana Mchungaji au Askofu anaweza kupigwa na waumini au kufukuzwa?
Hapo juu namba 4, 6, 7, 9 na 10 wahanga wake ni watumishi walio chini kwenye vituo vya Dayosisi, siyo walio makao makuu ya Dayosisi.