TANZIA Aliyekuwa Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Sir Andy Chande afariki dunia

TANZIA Aliyekuwa Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Sir Andy Chande afariki dunia

Bila shaka wewe ni Sabbath, uko sawa.... Ni mtu aliye hai tu ndiye anayejua kuwa kuna siku atakufa, lakini aliyekufa hajui tena jambo lolote.....kama ilivyoandikwa baada ya kifo ni hukumu.......! Lakini sisi tulio hai leo ndio tunamuombea kwa Mungu wetu ampunzishe ndugu yetu kwa amani, Mungu alisema ombeni chochote mtapewa, God is never such a cruel, and we lose nothing kwa kumtakia ndugu yetu heri, we are brothers, lazima tuguswe na kifo kama binadamu wa kawaida, kuhusu namna aliyaishi maisha yake hiyo ni juu yake na Mungu wake!!!!!
usipotoshe maandiko ulipoambiwa Ombeni chochote uliambiwa maana yake uwaombee hadi wafu?? We unaumwa siyo mzima,MTU asipotubu mwenyewe kabla ya kifo na kujikabidhi mwenyewe upande wa Kristo Hakuna yeyote anayeweza kumuombea heri au kubadilisha hukumu kama ni Jehanamu ni jehanam 2 kama ni uzima wa milele ni uzima wa milele tu hivyo tunapasawa kuishi maisha matakatifu na kutubu dhamabu zetu kabla mauti hayajatufika Hakuna cha RIP au mdogo wake RIP kama Chande Alimrudia MUNGU na kutubu dhambi zake ataurithi uzima wa milele kama ni kinyume na hivyo ni Moto
 
Hiyo national milling ndo ipi? au Ile ya iringa

National Milling Corporation au NMC kwa kifupi kilikuwa ni kiwanda kikubwa cha kutengeneza bidhaa za nafaka, ikiwa ni pamoja na unga wa mahindi, unga wa ngano na mikate maarufu kwa jina la siha.. Wanaokumbuka mikate ya siha watakubaliana na mie ile ilikuwa ni mikate mizuri mno..

Makao makuu ya kiwanda cha NMC kiliuwa pale Tazara ambapo sasa hivi panamilikiwa na Azam.. Mikoani nadhani walikuwa na depots za kuhifadhia bidhaa toka kiwandani Dar es Salaam..
 
Wabonyeaji wa misosi misibani utawagunduwa tu hapa, maana msiba huu hakuna wanawake kupikapika ni bufee ya catering tu, ni lazima muhamie mpaka siku ya maziko.
We waache tu wakale nyama za wafu wao
 
Sasa mali zote alizozitafit then leo anakufa kuna faid gani
Alan+temba+20170304_230917.jpg
 
Ni heri mara 1000 uwe member wa Freemasonry kuliko kuwa member wa wale wanaoona ni Sunna /thawabu kumuua mtu wa dini nyingine kisa eti ni kaffir, ajabu zaidi mpaka watu wa dini hiyohiyo wanawaua kisa tu dhehebu tofauti. Very stupid
 
Apumzike kwa amani. Ufafanuzi: kitabu cha Sir Andy kinaitwa A Knight in Africa na siyo Night in Africa. Na maana yake siyo Usiku katika Afrika. Knighthood ni tuzo zinazotolewa na Malkia wa Uingereza kuwaenzi wale waliofanya mambo mema au utumishi uliotukuka serikalini au katika jamii. Waliopata tuzo hiyo ndiyo majina yao yanatanguliwa na kisifa cha Sir kama ilivyokuwa kwa Sir Andy.
 
usipotoshe maandiko ulipoambiwa Ombeni chochote uliambiwa maana yake uwaombee hadi wafu?? We unaumwa siyo mzima,MTU asipotubu mwenyewe kabla ya kifo na kujikabidhi mwenyewe upande wa Kristo Hakuna yeyote anayeweza kumuombea heri au kubadilisha hukumu kama ni Jehanamu ni jehanam 2 kama ni uzima wa milele ni uzima wa milele tu hivyo tunapasawa kuishi maisha matakatifu na kutubu dhamabu zetu kabla mauti hayajatufika Hakuna cha RIP au mdogo wake RIP kama Chande Alimrudia MUNGU na kutubu dhambi zake ataurithi uzima wa milele kama ni kinyume na hivyo ni Moto
Sawa kwahiyo ataenda motoni according to you?? Rest In Peace inamaana ya PUMZIKA KWA AMANI, sijaona popote biblia inapokataza kutamka hivyo. Labda unipe andiko mkuu......
 
ha
Sasa mali zote alizozitafit then leo anakufa kuna faid gani


Ujue jinsi gani Mungu alivyo ananguvu, licha ya yooote wafanyayo ila kuzuia kifo imewashinda...laiti wangeweza kuna watu wasingekufa ambao ni hao.

Hawa masonic ndio wanapanga mauwaji ya kila sehemu za dunia kisirisiri wakitumia migongo ya dini.
 
Mwandishi anafanya makosa anaandika "Night in Africa" badala ya "Knight in Africa: Journey from Bukene"

Well, Kiranga angekuwepo angeongea mengi kuhusu JK Chande.

Round Tabler, Rotarian,
Knight of the British Empire.

Rest in perfect peace.
 
Aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji 'Andy' Chande afariki Dunia.

Sir Andy amekuwa mwanachama wa Freemasons kwa takribani miongo 6 tangu ajiunge.

Alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7 1928 ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene Mjini, Mkoani Tabora (Tanzania).

- Historia yake zaidi, tazama video hii;


-----------

Sir Andy Chande akiwa na watu mashuhuri enzi za uhai wake..

View attachment 491754

Akiwa na JK Nyerere

View attachment 491753

Akiwa na A.H. Mwinyi

View attachment 491752
Akiwa na BW Mkapa

View attachment 491751
Akiwa na JM Kikwete

View attachment 491750
Akiwa na Diamond Platnumz

View attachment 491755
Akiwa na Wanajumuiya wenzake wa Freemasonry


======

SIR ANDY CHANDE NA FREEMASONS
Freemasons wamekuwa wakitajwa kwenye kila aina ya minong’ono. Tumeona matangazo yakialika watu kujiunga nao kama wanataka kupata utajiri na kuwa watu wenye nguvu. Lakini bado Freemason, imebaki kuwa kitendawili miongoni mwa Watanzania wengi.

Leo tunakuletea habari kuhusu Mtanzania maarufu aliyefungua kinywa na kueleza namna alivyojiunga na Freemasons, kundi lililo kongwe duniani.

Tayari watu mbalimbali watu wenye hamu ya kupata utajiri wamekuwa wakitoa ushuhuda kuhusu kundi hilo na kusikika kwenye vyombo vya habari, hasa baada ya kifo cha mwingizaji nyota, Stephen Kanumba, mwaka 2012.

Siyo hivyo tu, bali kumeibuka pia matangazo yenye namba za simu yanayoshuhudiwa kwenye nguzo za simu mitaani hadi vichochoroni yakiwataka watu wanaotaka kujiunga na Freemason kupiga simu ili wapewe utaratibu wa namna ya kujiunga kwenye ‘kisima hicho cha mafanikio’.

Baadhi ya watu tayari wameshanaswa na mtego huo, huku wengine wakiendelea kujaribu bahati yao kujipatia utajiri kwa njia ya ‘nguvu za giza’.

Hata hivyo Jayantilal Keshavji Chande, maarufu zaidi nchini kwa jina Sir Andy Chande, aliyejiunga na Freemason Oktoba 25, 1954 baada ya kupita kwenye usaili mzito, anaeleza namna alivyoibuka kutoka familia ya kawaida hadi kuwa kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.

Sir Andy Chande, ambaye amekuwa mwanachama wa kundi hili kwa karibu miongo sita sasa, anaeleza namna alivyosajiliwa na kufikia hatua ya juu ndani ya kundi hilo.

Chande alizaliwa Mombasa Kenya, Mei 7, 1928, ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene mjini, mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania.

Katika kufafanua utaratibu mzima wa Freemason, Chande ameandika kitabu alichokiita; ‘A night in Africa-a journey from Bukene’ (Usiku wa Afrika-Safari kutoka Bukene), pengine akitaka kuweka sawa dhana na kuondoa tofauti ili misingi inayoendesha Freemason ifahamike.

Imani ya kimaadili na thamani ya kundi hilo ilianza wakati wa mazungumzo yake na Messrs Campbell Ritchie na McLean mwanzoni mwa miaka ya 1950.

“Katika kipindi kile nilianza kutambua kuwa Freemason ipo katika msingi wake. Ni sayansi ya maisha ambayo malengo yake ni kumbadilisha mtu kiimani na kumfanya awe anavyopaswa kuwa. Ni mabadiliko ya mtu binafsi,” Sir Andy Chande ameandika katika kitabu chake chenye kurasa 207.

Anasema kuwa malengo ya Freemason yamefunikwa na mafumbo, ambayo pengine ndiyo yanayoeleza utamaduni uliojificha katika utendaji kazi wake.

Chande anabainisha kuwa kanuni kubwa tatu za Freemason ziliandikwa kwenye kitabu kimoja nchini Canada, kilichochapishwa na Kampuni ya Penumbra Press.

Anaandika: “Kwa hiyo, ukiwa kwenye ngazi ya kwanza (first degree), kanuni inayoongoza, inamtaka mtu awe mkweli na mwenye maadili ambayo hasa Freemason inalenga kuyaweka kwenye akili, ili mwanachama awe mzuri.

Ngazi ya pili ya utaratibu inatilia mkazo kwenye vipaji na akili kupitia sanaa na sayansi, ili kutoa mchango mzuri iwezekanavyo kwenye maisha.”

Anafafanua kuwa ngazi ya tatu inampa mtu nafasi ya kutafakari uwepo wake kwa kina na kwamba kanuni zote tatu zinafahamika kama upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli.

“Kwa njia hizi inamaanisha, unafundishwa namna ya kuyafurahia maisha kwa kiwango chake cha juu. Kwa kufuata hizo kanuni tatu za upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli, wakati huohuo ukijitambua na kuanza kujiandaa na kutokwepeka kwa kifo,” anaandika Chande.

Anaongeza kuwa, wakati kanuni hizo tatu zinapoondolewa kwenye alama ya sanaa inayofunika imani ya Freemason, ambazo zilimpa udadisi wa kupata taarifa kuhusu utaratibu huo wa kale.

Sir Andy Chande ni Kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.

Kanuni za Freemason zinafundisha nini?

Katika ratiba ya Freemason, anaandika Chande akieleza kuwa, kanuni ya upendo wa kindugu inawafundisha ndugu wote kuwachukulia wanadamu wote kama familia moja iliyoumbwa na nafsi moja kuu.

“Kujiweka huru, vilevile, inaleta ujumbe nilioupata kutoka kwa baba yangu, aliyesema ni kuwekwa huru kwa mtu mwenye msongo. Kama ni kuwekwa huru kutoka kwenye umaskini, matatizo au akili isiyo na furaha,” anaandika Chande katika kitabu hicho.

Anafafanua kuwa ngazi ya tatu ambayo ni ukweli na pengine ndiyo muhimu zaidi ni mchango wa kimungu kwa mwanachama wa Freemason.

Anabainisha kuwa kipindi hicho ndicho kinachoheshimika kama njia ya matazamio na marekebisho na kama inawezekana, kurudiwa kwa kanuni hizo kama msingi wa kuelekea kanuni kuu nne alizozitaja kuwa ni; udhibiti binafsi, nguvu, umakini na haki.

Chande anaeleza kuwa Freemason siyo kifaa cha dini, pia siyo mpinzani wa dini, lakini inakaribisha watu wote bila kujali dini zao na haijaribu kubadilisha imani zao au kushawishi kuabudu kwao.

“Inajaribu tu kuwafanya watu kuwa wema,” anaandika Sir Chande akifafanua:

“Hii ndiyo dunia niliyoingizwa mwaka 1954, imekuwa na mchango mkubwa katika maisha yangu tangu wakati huo…: Roho yangu, akili yangu na nafsi yangu, vimetajirishwa na kushiriki kwangu Freemason.

Chanzo: Mwananchi

Natamani kama angerudi atuambie kuwa alienda upande gani maana alivyokuwa akijisifia kama ashafika mbinguni kumbe alipigwa upofu na mali za Dunia
 
Back
Top Bottom