Aliyekuwa mbabe wa kivita wa Liberia Prince Johnson, ambaye alisimamia mauaji ya kikatili ya aliyekuwa Rais Samuel Doe wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotikisa nchi hiyo, kabla ya kuwa Seneta na Mfalme wa kisiasa, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 72.
Msemaji wa familia Wilfred Bangura amethibitisha kuwa Johnson, alikuwa na shinikizo la damu kabla ya kufariki Dunia.
Zaidi ya watu 200,000 waliuawa, maelfu zaidi wakipata ulemavu na kubakwa na zaidi ya Milioni Moja walikimbia makazi yao wakati wa vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia kati ya 1989 na 2003, ambapo Johnson alihusika.
Johnson alipata umaarufu baada ya watu wake kumkamata, kumtesa, na kumkata viungo vya mwili Rais wa zamani Doe kabla ya kumuua.
#KitengeUpdates