Familia ya rais Mobutu yalilia haki ya nyumba yao kwa miaka 14, mtoto wa Marshal Mobutu azungumzia ugumu baada ya baba yao kuondoka madarakani ..
View: https://m.youtube.com/watch?v=eU3YCimpl3A
Bana ba Kongo waliokuwapo enzi za utawala wa rais Mobutu wanamkumbuka kuwa Mobutu alikuwa ni muunganishi maana enzi zake unaweza kusafiri mikoa yote 11 ya Zaire bila tatizo hasa ukijua Lingala vizuri ....
Na utawala wa sheria ulikuwapo tofauti na sasa baadhi ya mikoa ina majeshi ya mgambo yasiyo rasmi ambayo hayatii amri za kutoka Kinshasa...
Maoni mengine ya wanawaKongo wanasema sakata la watoto wa rais wa zamani Mobutu ni somo zuri la kuwapata kwa wanasiasa wetu wa Kiafrika, ambao ni wabinafsi sana, hawafikirii vizazi vijavyo kama leo tunaona mtoto wake akililia haki. Ndugu zako wakubwa wametesa watu wengi, hata watu wote wakatetemeka enzi za utawala wa Mobutu baba yenu na ,aliacha makovu mengi.
Asante leo tunakuona mtoto wa Mobutu ukiwa na unyenyekevu kama Mama Marie Antoinette roho yake ipumzike kwa amani.
Bwana Mobutu mtoto, unalalamika nini leo hii kupoteza nyumba yako, kwa kuteseka kwa miaka 14? Lakini sisi na familia zetu tumeteseka tangu rais Mobutu aingie madarakani. Mateso haya yaliongezeka hata maradufu kwa Uzairi (Congo Zaire), maana ulipokula kwenye masinia ya dhahabu na kuteremsha matonge ya mlo kwa maziwa, tulikunywa machozi yetu huku tukila pumba za mahindi! Na leo, hatuna chochote cha kuponea, kama wewe, kwa sababu hatukuwahi kuwa na chochote...