Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chadema, Joshua Nassari na mbunge wa sasa wa Karatu,
Willy Qulwi Qambalo wameondoka rasmi ndani ya chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wamepokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa pamoja na viongozi wengine wa Chama mkoa wa Arusha.
Amesema kuwa haikuwa kazi rahisi hata kidogo kufanya hayo maamuzi na akasema kuwa amekwenda Chama Cha Mapinduzi mchana kweupena si usiku kwa sababu moja tu, anachokifanya na alichokuwa anafanya ni swala lililowazi lenye mwanga na la kuelekeza.
Amesema kuwa hakwenda kuzunguza na wao kwa kuwa wamevaa kijani labda kuna kitu anataka hapana ila ni kwa sababu anaipenda nchi yake amesema angeamua kubaki huko duniani atengeneze pesa au kuitunza familia yake na afanye kazi akiwa huko duniani, wamsome kwenye magezati ya kimaaifa akiwa huko angeweza.
Nasari amekishukuru CHADEMA kwa kumlea tangia akiwa mdogo na sasa ameamua kutumikia nchi yake na sina nia ya kugombea nafasi yoyote, kilichopo mbele yake ni kumsaidia Rais John Magufuli.