Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na Willy Qulwi Qambalo wa Karatu wajiunga CCM na kupokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa

Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na Willy Qulwi Qambalo wa Karatu wajiunga CCM na kupokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa

Sasa ndio nimeamini, kumbe ile strategy yake ya kuwa mtoro bungeni ilikuwa "project" waliyoitengeneza ili akimbie Chadema.

Nilidhani kajamaa kameishia tu kuwa na sura ya kitoto, kumbe mpaka akili, binafsi nilimshangaa sana kwa lile kosa la kitoto alilofanya wakati ule, kumbe alitumwa.
Tatizo tulipowaambia wakati ule mlituona mataahira. Chama chenu kina udhaifu mkubwa kwenye ku-monitor viongozi wake walio watumishi wa umma. Yaani mbunge anaweza hata kutohudhudhuria bungeni kwa vikao vya kipindi cha miezi hat tisa bila ruhusa ya maandishi kutoka ofisi ya spika kama taratibu zinavyosema.

Unaweza dhani chama kinaendeshwa na wendawazimu. Inakuwaje chama chenye lundo la wanasheria kuanzia mashinani mpaka makao makuu huku kikiwa na wanasheria wa chama kama akina Peter Kibatala wabunge wake wawe hawahudhurii bungeni bila ruhusa? Hawajui kanuni za bunge? Hawajui kuwa siku hizi mbunge ni taasisi! Ina ofisi rasmi yenye katibu anayelipwa na serikali? Kwamba hata mbunge akisafiri nje ya nchi kwa kipindi kirefu basi katibu wake anaweza kuwasiliana na taasisi nyingine kama bunge (ofisi ya spika).

Hiki chama hovyo kweli.
 
kawa mstaarabu kiasi

it is better

nampongeza kwa hilo

Ni haki yake kikatiba so far, hatuwezi jua yanayoendelea chadema pia maana siasa za Africa zmekaa kipuuzi sana

Anyway Nasari ni smart boy sana atumike vizuri sio mapambio

Naona akiteuliwa kuwa mbunge ...
 
Wapo watu wanaamini Nasary ameongwa, nataka kuwafahamisha kwamba rushwa ya Nassary haitofautiana ya ya Kitila Mkumbo na Dr Slaa.

Nassary alikuwa kijana mtiifu kwa Dr Slaa, na Dr. Moja ya Jambo analoomba usiku na mchana Ni kuona chadema inakufa, nikuona Mbowe anaangamia kisiasa. Moja ya Jambo alilofanya Dr. Nikwenda na deal kwa watawala waliopo Sasa. Kwamba namleta flani lakini apangiwe kazi aweze kuishi na akipata kuishi wengine pia watakuja.

Nassary baada ya kubainika anashirikiana na mzee kukiua chama walimwacha na hata kipindi Cha kuvuliwa ubunge Lema hakusema chochote kwa sababu alishamkataza mara nyingi asiendekeze tumbo kuliko wanadamu waliomthamini akiwa na njaa.

Nassary alitambua kwamba rushwa ya madaraka itamtesa ila hakujipa muda wa kuona itamtesa kiasi gani. Leo katamka wazi kwamba anajua watu watamchukia na kumtukana, hakumaanisha wanachadema Bali anafahamu kwamba si chadema waliompa Ubunge Bali Ni wananchi.

Kwa jina na ukubwa wake kisiasa si mtu wakupokelewa na akina Sabaya, si mtu alipaswa kuuza utu wake kwa ajili ya madaraka. Si mtu aliyetakiwa kupewa ubunge na tume Bali alipaswa kusubiri Ubunge wa wananchi
Ameahidiwa uwaziri, ataupata ila hata angefanikiwa kuwa Waziri mkuu usaliti hautamwacha atembee kifua mbele.

Naamini leo Ni siku ya uzuni kwake kuliko siku nyingine zote, ila pia naamini ataishi mpweke zaidi ya Waitara.

Dr. Slaa, upinzani siyo Nassary Tena upinzani upo miyoyoni mwa kizazi kipya, wazee wazalendo wamepotea acheni kuaribu future za vijana wapeni ushauri sahihi. Leo mtoto akubaliki upinzani wala CCM anasubiri kuishi kwa kudra za mwenyekiti.
 
Nasari alipandwa bei na CCM ila akawapanga kuwa yuko tayari kuhama ila anaogopa Wameru watamuua, ndiyo akaomba afanye danganya toto ya kufukuzwa ubunge alafu atajoin baadaye na ndiyo hichi alichofanya.

Na leo angekataa kwenda kuzalilishwa kwa kupokelewa na mwenyekiti wa uvccm wangemdai chenchi yao.
 
Umeuliza jibu mbona.Ukuona majuzi alikuwa na DC wa Hai.Alishaunga juhudi kiaina akazugia kwenda mahakamani,kumbe alishavuta advance.
Hehehe kama Nyalandu Na Lowassa walivyotoa advance kwa Mboweee
 
Kwa maneno ya baba wa taifa, " Ni Tabia ya kimalaya malaya tu, ananunulika tu" sijui anawafundusha nini vijana wenzake.


Vipi mtakapo mpokea membe nayo itakuwa ni tabia ya kimalaya malaya ya siasa?
Na juzi amesema mwenyewe keshawaroga huko sasa mtajuwa mmerogwaje hilo sijui.
 
Vipi mtakapo mpokea membe nayo itakuwa ni tabia ya kimalaya malaya ya siasa?
Na juzi amesema mwenyewe keshawaroga huko sasa mtajuwa mmerogwaje hilo sijui.

kuhama hama- iwe kwa membe au Nassari -ni umalaya Malaya tu kwa kisingizio cha katiba kuwaruhusu- sijui siku hizi umalaya umalaya umehararishwa na vifungu gani ili hali polisi kila kukicha hufanya Msako wa Malaya . Sijui hawa Malaya wa kisiasa huwa mpaka wamulikwe na tochi?
 
kwa trend hii chadema hakina makosa, ni suala la mtu binafsi na kusaliti. wasomi wengi ni wapuuzi kabisa, tulitegemea kama kina nassari type ndo wangekuwa future opposition leader kumbe ugolo wa tumbaku mfu (isiyo active), kumbe kizazi cha zamani walikuwa na vision kuliko 4G, tanzania itahangaika sana kupata definetly desired leader kama akina madiba, lumumba,kambarage, nkurumah na wengine. viongozi hawa walikuwa commited kuwakabili wakoloni na vibaraka wao! leo hii the eldest ruling party in tanzania ccm ndo kinabebwa na mahakama, tume ya uchaguzi, vyombo vya ulinzi na usalama, msajiri wa vyama, bunge, eti mnawapa vijana wasomi nafasi za uwakilishi wakawasemee wanainchi ndo wanakuwa wakupewa vipande 30!! wananchi wakiletwa kwenu kuwahadaa wapigeni chini wakiwahonga chukueni ila piga chini,,,
 
Hi nchi kusupport upinzani ni kujitaftia presha,bora tuu ubaki na presha zako za kushabikia Yanga.Nikikumbuka mwaka 2015 nilivyomuunga mkono mamvi akahamia CHADEMA nikahama nae alaf akaja kurudi matopeni,Siwezi kuwaamini wanasiasa tena,huyu Nassari anasubiri uteuzi na atateuliwa pumbav zake.
 
Back
Top Bottom