EZZ CHEZZ
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 1,230
- 1,352
Tatizo tulipowaambia wakati ule mlituona mataahira. Chama chenu kina udhaifu mkubwa kwenye ku-monitor viongozi wake walio watumishi wa umma. Yaani mbunge anaweza hata kutohudhudhuria bungeni kwa vikao vya kipindi cha miezi hat tisa bila ruhusa ya maandishi kutoka ofisi ya spika kama taratibu zinavyosema.Sasa ndio nimeamini, kumbe ile strategy yake ya kuwa mtoro bungeni ilikuwa "project" waliyoitengeneza ili akimbie Chadema.
Nilidhani kajamaa kameishia tu kuwa na sura ya kitoto, kumbe mpaka akili, binafsi nilimshangaa sana kwa lile kosa la kitoto alilofanya wakati ule, kumbe alitumwa.
Unaweza dhani chama kinaendeshwa na wendawazimu. Inakuwaje chama chenye lundo la wanasheria kuanzia mashinani mpaka makao makuu huku kikiwa na wanasheria wa chama kama akina Peter Kibatala wabunge wake wawe hawahudhurii bungeni bila ruhusa? Hawajui kanuni za bunge? Hawajui kuwa siku hizi mbunge ni taasisi! Ina ofisi rasmi yenye katibu anayelipwa na serikali? Kwamba hata mbunge akisafiri nje ya nchi kwa kipindi kirefu basi katibu wake anaweza kuwasiliana na taasisi nyingine kama bunge (ofisi ya spika).
Hiki chama hovyo kweli.