Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Wapo watu wanaamini Nasary ameongwa, nataka kuwafahamisha kwamba rushwa ya Nassary haitofautiana ya ya Kitila Mkumbo na Dr Slaa.
Nassary alikuwa kijana mtiifu kwa Dr Slaa, na Dr. Moja ya Jambo analoomba usiku na mchana Ni kuona chadema inakufa, nikuona Mbowe anaangamia kisiasa. Moja ya Jambo alilofanya Dr. Nikwenda na deal kwa watawala waliopo Sasa. Kwamba namleta flani lakini apangiwe kazi aweze kuishi na akipata kuishi wengine pia watakuja.
Nassary baada ya kubainika anashirikiana na mzee kukiua chama walimwacha na hata kipindi Cha kuvuliwa ubunge Lema hakusema chochote kwa sababu alishamkataza mara nyingi asiendekeze tumbo kuliko wanadamu waliomthamini akiwa na njaa.
Nassary alitambua kwamba rushwa ya madaraka itamtesa ila hakujipa muda wa kuona itamtesa kiasi gani. Leo katamka wazi kwamba anajua watu watamchukia na kumtukana, hakumaanisha wanachadema Bali anafahamu kwamba si chadema waliompa Ubunge Bali Ni wananchi.
Kwa jina na ukubwa wake kisiasa si mtu wakupokelewa na akina Sabaya, si mtu alipaswa kuuza utu wake kwa ajili ya madaraka. Si mtu aliyetakiwa kupewa ubunge na tume Bali alipaswa kusubiri Ubunge wa wananchi
Ameahidiwa uwaziri, ataupata ila hata angefanikiwa kuwa Waziri mkuu usaliti hautamwacha atembee kifua mbele.
Naamini leo Ni siku ya uzuni kwake kuliko siku nyingine zote, ila pia naamini ataishi mpweke zaidi ya Waitara.
Dr. Slaa, upinzani siyo Nassary Tena upinzani upo miyoyoni mwa kizazi kipya, wazee wazalendo wamepotea acheni kuaribu future za vijana wapeni ushauri sahihi. Leo mtoto akubaliki upinzani wala CCM anasubiri kuishi kwa kudra za mwenyekiti.
Sio lazima uwe umesema ukweli kwa asilimia mia moja, lakini nanusa harufu ya mwelekeo wa ukweli. Hilo la kwamba Slaa anataka cdm ife kwa sababu ya tofauti yake na Mbowe, pia liko wazi. Ngoja tunywe mtori nyama tutazikuta chini. Sasa nimejua kwanini hata mbunge wa Karatu kaondoka cdm.