Aliyekuwa mke wa MC Pilipili, aibua gumzo Mtandaoni baada ya kuonekana na Ujauzito

Aliyekuwa mke wa MC Pilipili, aibua gumzo Mtandaoni baada ya kuonekana na Ujauzito

Aliyekuwa mke wa mchekeshaji maarufu Emmanuel Mathias (MC Pilipili), Nicole Florence 'Qute Mena', amezua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akiwa na ujauzito wa siku nyingi.

Gumzo hilo limeanza rasmi hivi karibuni kufuatia mrembo huyo kuchapisha mfululizo wa picha na video kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, zikimuonyesha akiwa na tumbo kubwa la uzazi huku akionekana mwenye furaha tele.

Taarifa hizo zimeibua hisia mseto na maswali mengi kutoka kwa mashabiki na wafuasi wake. Wengi wao wamekuwa wakijiuliza kuhusu umri wa ujauzito huo pamoja na utambulisho wa baba wa mtoto tarajiwa, huku wengine wakichukua fursa hiyo kumtumia ujumbe wa pongezi na kumtakia heri katika hatua hiyo mpya ya maisha yake.

Hadi sasa, Qute Mena hajatoa ufafanuzi wa kina au kuweka wazi maelezo ya ziada kuhusu baba wa mtoto huyo wala umri kamili wa mimba hiyo, hali inayozidi kuongeza udaku na mjadala mpana mtandaoni.


Hivi upelelezi wa kifo cha mume wake uliishia wapi? Ila TZ
 
Back
Top Bottom