Aliyekuwa Mkurugenzi wa Sheria TFF amaliza utata: Asema Fei Toto amekosea, mkataba hauvunjwi kienyeji vile

Duh we jamaa huna akili
 
Aiseeee hii ni hatara kwa Fei, unaweza tuwekee hiko kipande tupate uhakika zaidi?
 
Kama katika mkataba wake kuna kipengele cha release clause, mchezaji anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu itakayolipa kiasi kilichomo kwenye hiyo clause bila kuhusisha klabu yake. Ila hataruhusiwa kuhama mpaka msimu wa uhamaji unapokuja. Klabu iliyo na release clause inatakiwa kuanza mazungumzo na mchezaji ambae wanaona thamani yake imepanda ili kuongeza kiasi kilichomo na wakati huo huo kumuongezea maslahi yake binafsi. Wasipofanya hivyo, ruksa kwa klabu nyingine kuingia MOU na huyo mchezaji mara watakapolipa lile dau. Na hiyo klabu mpya inaweza kumuuza tena kwa bei ya juu zaidi bila ya klabu ya awali kupata chochote.

Aidha, kama kuna buyout clause, mchezaji anaweza kulipa kiasi kilichopo na kuingia mkataba mpya na klabu nyingine msimu unaofuata. Tatizo la buyout clause ni kuwa mara nyingi hizi pesa mchezaji anapewa na klabu inayomtaka na hivyo inaweza kuwaingiza katika matatizo ya kodi ( ametoa wapi hizo pesa?) na hoja kuwa alianza mazungumzo na klabu nyingine kabla ya kuifyatua hiyo clause, kitu ambacho hakiruhusiwi.

Amandla...
 
hii sio vita ya yanga na fei, bali ni vita ya wanasheria tupu..ili wajipigie hela zao maana tunagawana kidogo kidogo hapa nchini, matatizo ya mwengine ni fursa ya mtu. lazima wanasheria wa yanga waoizonge timu ili wafungue kesi..nako kwa fei watajitokeza mawakili wasomi kumtetea fei😛😀. najilaumu kwanini sikusoma sheria ningekuwa mchonganishi hasa ili nijipatie madili kila mara..uzuri serikali haiajiri ningejiajiri niwanyooshe wasiojua sheria jamaniii..wanasheria wanafaidi kwakweli..nawaonea wivu😎😛😛😛
 
Huyo kilaza kakurupuka na usimba wake.
Muacheni kijana atengeneze maisha yake, tukumbuke umri unakwenda kama Azam watampa mshahara mara nne ya ule wa Yanga asubiri nini! Maisha yake ni sasa hakuna wakati mwingine!! Ila tu nimshauri Fei kama akipata timu nje itakua vizuri zaidi sio hapa Bongo!!
 
Ni kweli, Hiyo clause imempa mchezaji haki ya kuvunja Mkataba, lakini the issue ni kwamba ukitaka kuvunja Mkataba hakuna formality za kufuata ambazo ni za kitaasisi?, i.e kukaa chini na Kuandika barua Kwa Klabu, nk
Formality yenyewe ndio hiyo , hata kama ipo nyingine haithari chochote as long as cost zimelipwa

Unaweza soma namba 14 kipengele cha kwanza hapo , hata FIFA hawatak jichosha, wewe lipa sepa
 
Mimi sio mwanasheria ila baada ya kuusoma huo mkataba kwenye picha sijaona Feisal alipokosea..
 
Hapa hakuna mwanasheria, ni kanjanja tu. Hajui hata zinazungumzia nini.

Kwa mfano.
Azam wanahusikaje katika hili la Feisal? Mpaka sasa hakuna mahali Feisal amesema anahamia Azam, na Azam wamekanusha kuhusika na chochote kuhusu Feisal. Sasa mwanasheria unajengaje hoja katika hilo?

Mchezaji akiwa huru (hana tena mkataba na klabu yake ya awali), ni vipi tena klabu zingine zikitaka kumsajili ziende kujadiliana na klabu yake ya awali?

Kama mkataba wa Feisal na Yanga unatoa nafasi kwa Feisal kuweza kuuvunja muda wowote kiwa atalipa fidia za kimkataba na Feisali anaona okay, nini mantiki ya kusema Feisal anapaswa kwanza kufanya majadiliano na Yanga? Ili iweje?
 
Huna hoja za msingi na kinachowauma ni Yanga kuendelea kuongoza ligi na ndio maana mnatetea ujinga kwa hoja nyepesi.
Hee, kumbe bado upo?!

Kama wewe ulikuwa na hoja za msingi kwanini usingeandika hapo tuzione badala ya kupoteza muda na kukimbilia habari ya makolo!

Wacha usanii.
 
Kuna nyongeza hapo chini yake na ndo hawamtaki kujiweka Ili kuficha dogo Fei alipoingia mkenge.
Issue ya Fei kuondoka ina zaid ya miez minne , sio jambl la jana na juz

Hiyo ilikua kilele tu
 
Mkuu, ukisitisha mkataba unakuwa free, hakuna haja ya mazungumzo tena. Sasa kama ni mali ya Yanga siku zote hata baada ya kufanya termination, hicho kipengele kina maana gani hapo?
Mkataba hausitishwi kihuni hivyo lazima mwajiri wako wa kwanza umjulishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…