Southern Highland
JF-Expert Member
- Mar 22, 2017
- 14,938
- 25,405
Mkuu kuna kitu unakisahau japokua umeandika maelezo mengi. Katika ile barua ya Yangu ilichapishwa imeeleza kuna sheria na taratibu za FIFA na TFF zimekiukwa.Huyu mkurugenzi wa sheria asiyejua sheria anashangaza, unasema vipi suala la mkataba ni la kukaa pamoja walimalize wakati kuna kipengele kwenye mkataba kilimruhusu mchezaji kuvunja mkataba kama akiweka kiasi fulani cha pesa kwenye akaunti ya klabu?
Zaidi, anaposema mchezaji anapovunja mkataba hakai peke yake, lazima akae na klabu yake, napo anakosea, akumbuke pande zote kwenye mkataba kisheria huwa zipo sawa, hapa asilete ukubwa wa klabu akadhani ndio advantage kwa Yanga SC, hapa Yanga SC walijichanganya wenyewe kuweka kipengele kilichowabana kwenye mkataba.
Pia, klabu inayomhitaji mchezaji sio lazima iandike barua ikimhitaji mchezaji husika, kuna.mazingira yanayolazimisha kufanya hivyo hasa ikiwa mchezaji bado ana mkataba na timu yake, na mkataba wake unambana kwenda timu nyingine bila makubaliano ya timu mbili.
Lakini kwa Fei Toto hali haiko hivyo, yeye habanwi na mkataba kwasababu ameshatimiza takwa la kimkataba lililomtaka anunue sehemu ya mkataba wake kama akitaka kuondoka akiwa huru, huyu mwanasheria anaonekana mchanga halafu amekariri mambo ya usajili, hajui kutofautisha mazingira.
Yes amevunja mkataba lakini kwa taratibu za FIFA ilipaswa timu inayomtaka hasa wakati wa dirisha ionane na timu inayommliki mchezaji wajadiliane kuvunja mkataba. Feisal amekidhi vigezo kuvunja mkataba na Yanga ila hajakidhi kulungana na taratibu za baba wa mpira wetu na ndicho anachozungumza huyo mwanasheria.
Tusikurupuke jamani tunaishia kujiaibisha kuandika vitu tusivyo na uelewa navyo