Du hata picha huoni.
Feisal anao mkataba hai hadi May 2024. Hivyo sio free agent ni mali ya Yanga.
Pili Feisal au Yanga wanayo haki ya kuvunja mkataba. Na utaratibu wa kuvunja ni lazima mdaliane na kufikia muafaka wa kuvunja.
Tatu, timu yeyote inaweza kumnunua mchazaji yeyote ikiwa timu hiyo itafikia makubaliano na timu inayommiliki mchezaji huyo. Kwa mchezaji ambaye mkataba wake umeisha(bado timu inawajibika kutoa taarifa ya nia ya kumchukua)
Mchezaji anayetaka kuvunja mkataba lazima wakubaliane pande zote mbili(fuatilia Ronaldo na Man United hivi karibuni). Klabu yake ikishatangaza wazi wamevunja mkataba na mchezaji baada ya mashauriano. Kama hakukua na timu iliyomuhitaji kabla ya kuvunja mkataba basi mchezaji atahesabika kuwa yupo huru. Lakini bado timu itakayomtaka italazimika kutoa taarifa kwa timu yake ya zamani.
Dogo Feisal anatamani kupata mshiko mkubwa ila uelewa mdogo wa maswala ya mkataba.
Azamu wanamtaka kwa hudi na uvumba na wamemchanganya kwa kutumia nguvu ya hela pasipo kufuata taratibu na sheria
Yanga bado wanamhitaji Feisal lakini pia wapo tayari kumuuza ila sio kwa 112.0m maana Feisal ni mtaji mkubwa.
Solution
Feisal akae na yanga wakubaliane kuvunja mkataba.
Azamu wakubaliane na Yanga kiasi wanachotaka kumnunua Feisal. Hapo transfer zitafanyikapasipo na kelele.