Aliyekuwa Mkurugenzi wa Sheria TFF amaliza utata: Asema Fei Toto amekosea, mkataba hauvunjwi kienyeji vile

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Sheria TFF amaliza utata: Asema Fei Toto amekosea, mkataba hauvunjwi kienyeji vile

Husizani rahisi kama ndio hata Madrid wangefanya uhuni huo kwa Ronaldo na wasingeshindwa.

Wakati unapoingia mkataba zinazo husika pande mbili na wakati wa kuuvunjwa unavunjwa na pande mbili, sio kwa sababu unahela unavunja.Kuna sheria zina mlinda mchezaji na club inayo msajili.
Hawawezi kukuelewa.. Rage apewe pgd ya heshima kwa kweli
 
Du hata picha huoni.

Feisal anao mkataba hai hadi May 2024. Hivyo sio free agent ni mali ya Yanga.

Pili Feisal au Yanga wanayo haki ya kuvunja mkataba. Na utaratibu wa kuvunja ni lazima mdaliane na kufikia muafaka wa kuvunja.

Tatu, timu yeyote inaweza kumnunua mchazaji yeyote ikiwa timu hiyo itafikia makubaliano na timu inayommiliki mchezaji huyo. Kwa mchezaji ambaye mkataba wake umeisha(bado timu inawajibika kutoa taarifa ya nia ya kumchukua)

Mchezaji anayetaka kuvunja mkataba lazima wakubaliane pande zote mbili(fuatilia Ronaldo na Man United hivi karibuni). Klabu yake ikishatangaza wazi wamevunja mkataba na mchezaji baada ya mashauriano. Kama hakukua na timu iliyomuhitaji kabla ya kuvunja mkataba basi mchezaji atahesabika kuwa yupo huru. Lakini bado timu itakayomtaka italazimika kutoa taarifa kwa timu yake ya zamani.

Dogo Feisal anatamani kupata mshiko mkubwa ila uelewa mdogo wa maswala ya mkataba.
Azamu wanamtaka kwa hudi na uvumba na wamemchanganya kwa kutumia nguvu ya hela pasipo kufuata taratibu na sheria

Yanga bado wanamhitaji Feisal lakini pia wapo tayari kumuuza ila sio kwa 112.0m maana Feisal ni mtaji mkubwa.

Solution
Feisal akae na yanga wakubaliane kuvunja mkataba.

Azamu wakubaliane na Yanga kiasi wanachotaka kumnunua Feisal. Hapo transfer zitafanyikapasipo na kelele.
Kwani lazima kukaa na Yanga? Kwenye mkataba kuna kipengele kimesema lazima wakae chini?
 
Kwani lazima kukaa na Yanga? Kwenye mkataba kuna kipengele kimesema lazima wakae chini?
Kwani mkataba huo ambao yy anataka kuulipia alisainishwa na nani?

Kama walikaa chini kisaini basi wakae chini kuuvunja. Uzuri kuna sheria zinazo mlinda mchezaji na club anayo ichezea.
 
Mkuu kuna kitu unakisahau japokua umeandika maelezo mengi. Katika ile barua ya Yangu ilichapishwa imeeleza kuna sheria na taratibu za FIFA na TFF zimekiukwa.

Yes amevunja mkataba lakini kwa taratibu za FIFA ilipaswa timu inayomtaka hasa wakati wa dirisha ionane na timu inayommliki mchezaji wajadiliane kuvunja mkataba. Feisal amekidhi vigezo kuvunja mkataba na Yanga ila hajakidhi kulungana na taratibu za baba wa mpira wetu na ndicho anachozungumza huyo mwanasheria.

Tusikurupuke jamani tunaishia kujiaibisha kuandika vitu tusivyo na uelewa navyo
Kweli Mkuu. Tukumbuke Feisal kavunja contract na Yanga sio kwamba anaenda masomoni ulaya bali amevunja ili kwenda kucheza mpira timu nyingine.
 
Free Agent mwaka 1 mmoja na nusu? Mkataba unaingiwa na pande mbili na hata ukivinjwa lazima pande mbili zikae chini bila kusahau third party ambayo inataka kuvunja huo mkataba.
Zilizoingia mkataba ni pande mbili, Feisal na Yanga. Feisal ameununua mkataba kama vifungu vinavyoeleza. Wala hajasema anataka kwenda Azam au Simba! Yeye anataka kuwa huru
 
Zilizoingia mkataba ni pande mbili, Feisal na Yanga. Feisal ameununua mkataba kama vifungu vinavyoeleza. Wala hajasema anataka kwenda Azam au Simba! Yeye anataka kuwa huru
Ameununua mkataba kwa makubaliano na nani?
 
Ya mkataba upi?
img-20221225-wa0005-jpg.2457519
 
Mi nilitaka kushangaa kwamba inakuwaje mtu unakaa zako magomeni mapipa unakula tambi zako na juice ya embe unaamua kuvunja mkataba kiwepesi hivi!!
 
Back
Top Bottom