Tetesi: Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Serikali ya Awamu ya Tano Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga

Tetesi: Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Serikali ya Awamu ya Tano Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga

Akiteuliwa familia za waluouawa wote na wasiojulikana awamu ya 5 walipwe bilioni moja. Wakati ule kuna msiba nilienda wa katibu wa vijana wilaya flani wa chadema alicharangwa mapanga nilijionea jinsi zile familia zilivyoachwa na madonda na makovu yasiyokoma.

Kama ni kigezo cha maridhiano.. Akiteuliwa na hao wahanga wote. wapewe bilioni moja moja in exchange na huyo makonda.

Ila hata ivyo najua hatafika mbali.
 
Mama Samia hawezi asilani kufanya uteuzi wa kumdhalilisha Rais mwenyewe, Rais Samia sio mtu wa kufanya teuzi za ajabu hivyo na kamwe haiwezi tokea kwa Mama yetu, Mama Samia kajenga Imani na upendo mkubwa kwa wananchi tayari kwa muda mfupi sana, alafu alete mtu wa hovyo hovyo kama Makonda, hilo halipo na watanzania tunaona hilo halipo. Muda wa watu wa hovyo ushapita
Nakwambia akifanya ivyo amejimaliza. Ni nani hakuathiriwa na jeuri ya huyo dogo? Watu wanategemea ashitakiwe then awe RC?
 
Acha wivu wewe kama unamchukia kwa chuki binafsi ni wewe

Makonda ndie mtu pekee anayeweza kuhimili moto wawapinzani wanaokwenda kuuwasha
Wana moto gani? Ni upuuzi mtupu. Wananchi wametoka kwenye dhiki waje wakahangaike na vurugu za za upinzani?.

Je unajua kwanini hata tozo na gharama kupanda sababu ya kuyumba uchumi wa dunia na hali ya hewa na corona wananchi hawakureact? Ni sababu tulitoka kwenye dhiki kuu ya miaka 6. Hakuna mtu ana hamu na wapinzani wasio na nia ya dhati na wanayosema.
 
Hii ni habar mpya kabisa kijana mchapakazi paul makonda kwa taarifa zilizopo huenda akawa RC mkoa wa shinyanga, nadhani kijana huyu huenda anateuliwa kwa kuwa kunamaridhiano ya siasa na siasa za upinzani anazimudu ni kiongozi anayejuwa jinsi ya kucheza mpira na wapinzani.

Kama ni kweli namtakia kila la heri katika utumishi wake.
KWA CCM inawezekana hata STEVE NYERERE anaweza pia akawa Mkuu wa Mkoa
 
Wana moto gani? Ni upuuzi mtupu. Wananchi wametoka kwenye dhiki waje wakahangaike na vurugu za za upinzani?.

Je unajua kwanini hata tozo na gharama kupanda sababu ya kuyumba uchumi wa dunia na hali ya hewa na corona wananchi hawakureact? Ni sababu tulitoka kwenye dhiki kuu ya miaka 6. Hakuna mtu ana hamu na wapinzani wasio na nia ya dhati na wanayosema.
21 sio mbali mkuu ...hautaamini na macho Yako .... Ni wajinga na wapumbavu wachache wenye mawazo kama yako

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni habar mpya kabisa kijana mchapakazi paul makonda kwa taarifa zilizopo huenda akawa RC mkoa wa shinyanga, nadhani kijana huyu huenda anateuliwa kwa kuwa kunamaridhiano ya siasa na siasa za upinzani anazimudu ni kiongozi anayejuwa jinsi ya kucheza mpira na wapinzani.

Kama ni kweli namtakia kila la heri katika utumishi wake.
Makonda yupo chini ya uchunguzi. Kwanza alimteka Mo, aliua na kujeruhi vipi awe kwenye cheo? Subiri kidogo utamuona pale Kisutu na makesi kibao. Tena yakiongozwa na Jamhuri
 
Kina Cha maji hakipimwi kwa kuingiza miguu, tutavuka mto tukiufikia, kwa Sasa hatutoi panga zetu kwenye ala.

Itakuwa blunder kubwa sana ambayo itaandamana na political risks, na sioni wa kubeba hilo zigo la misumari, walau kwa wakati huu.

Ni huyu mtu ambaye anatajwa kuwa Dodoma wakati Lissu akinyeshewa mvua ya risasi. Na ni mtu huyu, tangu nchi hii iumbwe, Yuko blacklisted asikanyage U.S.A kwa kudhulumu haki ya kuishi. Kudhulumu haki ya kuishi ni kwamba kwa mkono wake au Kwa maelekezo yake, aliuwa watanzania wenzetu iwe kwa mapanga, kwa risasi, au kuwanyonga, inawezekana walimlilia sana awaache au awasamehe, lakini akahakikisha wanakufa kifo Cha kikatili, bila fursa ya kuaga wapendwa wao, Wala kujulikana walipozikwa.

Ameshaonja damu ya binadamu, bila shaka atakuwa na kiu ya damu nyingine, ni ya nani Kati ya wa Tizee milioni 61?
tatizo Tanzania hii watu wenye akili timamu wanaendeshwa na hisia umememuona nani aliyeuwawa na makonda? mahakama ipi iliyothibitisha makonda kauwa? , kiufupi tafuta hela makasiriko uliyonayo kwa watu usiowajua ni kwasababu haupo busy kutafuta Hela , kiufupi usijifunge na kamba usiyoijua .
 
Bila shaka wewe ni moja ya wale mabodigadi wake mlilokuwa mnapepea Makonda na Lemutuz ili wasipate joto.

Kibarua kimekufa hicho, na hakitarudi
 
Wewe acha uchawa!
Mama anataka mikopo, hivyo lazima akuze demokrasia na utawala wa Sheria.
Sasa huyo Makonda wako anadhani Mama ameshasahau tamko la Mike Pompeo la kunyima watu wengine haki za kuishi ( yaani Muuaji)?!
Atasubiri sana! Hivi bado ana ile Chura yake!?
 
Back
Top Bottom