Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa Tabora Mjini apinga kustaafishwa

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa Tabora Mjini apinga kustaafishwa

Kuna watu Wana dharau za wazi wazi.

Unafikiri Enzi Cha bwana mkubwa angethubutu hata kujipost huyo ,?? Achilia mbali kuenda mahakamani
Mama haogopwi si unaona hata wasaidizi wake hasa mawaziri wanavyojimwambafai sasa hv...pia wanatupiga sana ila mama yupo kimyaa hana shida na mtu ndio kwaanza kawaomba wale lakini wasivimbiwe!.
 
Wakati mwingine TZ ni shida. Wakiwa majukaani, wanahubiri kujiajili, Sasa zamu Yao ikifika, anaenda mahakamani Kugomea kujiajili kama walivyokuwa wanahubirii[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Vita vya uraiani sii mchezo

Ova
 
Anadai arudishwe kazini PSSSF (Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma) alipotolewa kupelekwa kamati maalum ya CCM kuhakiki mali kisha kuteuliwa na Rais wa awamu ya 5 JPM kuwa mkuu wa wilaya halafu baadaye kutenguliwa ukuu wa wilaya na rais wa awamu ya sita.

Habari Toka maktaba :
Wenzie watumishi wa umma kule chama cha walimu CWT walikataa teuzi za U-DC



🤣🤣Alikuwa bwege kweli,unaacha cheo chenye pension afu unakubal cheo Cha kisiasa usichojua hatima yake,si uzuzu huo?
 
Ana hoja ya msingi.

Fikiria, mtu yawezekana ana ajira sehemu fulani. Halafu anateuliwa kuwa DC au RC. Anaacha kazi yake ya mwanzo. Anaenda kwenye uteuzi. Baada ya mwaka mmoja anafutwa kazi, haambiwi hata sababu. Kazi yake ya mwanzo amepoteza, na huku amefutwa kazi. Huyu tayari ameharibiwa mpangilio wa maisha.

Suluhisho la jaya yote ni KATIBA.

Katiba ipunguze idadi ya wateuliwa wa Rais. Nafasi nyingi ziwe ni ajira ya kawaida, na wahusika walindwe kwa sheria ya ajira.

Rais abakiziwe teuzi za nafasi za kisiasa tu, na zenyewe, Rais asiwe final. Kuwepo chombo cha kuidhinisha. Wanapotolewa kabla ya muda uliotarajiwa, zitolewe sababu kwa chombo kilichoidhinisha teuzi zao.
 
Toka Maktaba :

29 December 2017

Ikulu, jijini Dar es Salaam

'Kamati ya Dk. Bashiru'

Wajumbe wa Kamati ya Kuhakiki Mali zote za CCM

Kamati hiyo ina wajumbe wana CCM tisa, wakiongozwa na Dk. Bashiru, iliundwa na mwenyekiti wa CCM taifa mheshimiwa Rais John Pombe Joseph Magufuli, Desemba 20, mwaka 2017 mjini Dodoma.

Wajumbe hao ni Walter Msigwa, Albert Msando, Galala Wabanhu, Albert Chalamila, William Sarakikya, Komanya Erick Kitwala, Dk. Fenella Mukangara na Mariam Mungula.



Katika Mazungumzo hayo Mhe. Rais Magufuli amewataka wajumbe wa kamati hiyo kufuatilia na kuhakiki mali zote za chama, kumhoji mtu yeyote ambaye atahitajika kutoa taarifa juu mali za chama na kubaini thamani ya mali, mahali zilipo, makusanyo ya mapato na wanaozishikilia ama kutumia mali hizo.

Mhe. Rais Magufuli pia ametoa wito kwa wanachama wa CCM na wananchi wengine kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zote zinazohusu mali za chama kwa kamati hiyo, na watakaoitwa kuhojiwa waitikie wito huo.
View attachment 2644124
“Nataka mali za chama zikinufaishe chama, nataka mkamhoji mtu yeyote, awe kiongozi, awe mwanachama, awe mfanyabiashara, mtu yeyote. Mkazihakiki mali zote ili chama kipate haki yake” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Kwamba mzee alikua sukuma gang[emoji28]
 
Ana hoja ya msingi.

Fikiria, mtu yawezekana ana ajira sehemu fulani. Halafu anateuliwa kuwa DC au RC. Anaacha kazi yake ya mwanzo. Anaenda kwenye uteuzi. Baada ya mwaka mmoja anafutwa kazi, haambiwi hata sababu. Kazi yake ya mwanzo amepoteza, na huku amefutwa kazi. Huyu tayari ameharibiwa mpangilio wa maisha.

Suluhisho la jaya yote ni KATIBA.

Katiba ipunguze idadi ya wateuliwa wa Rais. Nafasi nyingi ziwe ni ajira ya kawaida, na wahusika walindwe kwa sheria ya ajira.

Rais abakiziwe teuzi za nafasi za kisiasa tu, na zenyewe, Rais asiwe final. Kuwepo chombo cha kuidhinisha. Wanapotolewa kabla ya muda uliotarajiwa, zitolewe sababu kwa chombo kilichoidhinishwa.
Ndio maana kuna waalimu walikuwa wanakutana teuzi za ukuu wa wilaya kumbe waliyaona haya.
 
Tumshauri akapate notisi kwa Ally Hapi
We mjinga Jamaa ana hoja za msingi sana, shida nchi imejaaa wajinga plus Waoga, Ogopa sana nchi inakuwa na watu wajinga na waoga bora hata juwa njinga then usiwe nuoga shida ya Tanzania watu ni wajinga jumlisha waoga
 
Kwani huyo jamaa kabla ya kuteuliwa kuwa DC aliwahi kutuma maombi kwa nani?

Kama alipewa kwa hisani, basi pia ajue anaweza kuipoteza bila kupewa sababu zozote.

Rais amepewa mamlaka ya kuteua na kutengua kwenye nafasi zilizo chini yake bila kutoa sababu yoyote, ningemuona mjanja kama angeshinikiza hiyo sheria ibadilishwe, kwa kumtaka Rais atoe sababu pale atakapomteua fulani, au kumtengua.

Anachokifanya huyo jamaa kwa sasa ni sawa na kulilia arudishiwe kitu alichonyan'ganywa wakati hakuwahi kukiomba, kama alikuwa tayari kukipokea bila kuulizia sababu ya kupewa kwake, basi kikichukuliwa asiulize sababu pia.
We mjinga jamaa ana hoja ya msingi sana, shida kuu nchi imejaa wajinga sana
 
Huyu Jamaa hajakataa kutenguliwa u-DC bali anataka arudi kwa mwajiri wake wa zamani PSSSF baada ya kutenguliwa u-DC. Hii ni haki yake hata kama HAMUMPENDI, haina kupepesa macho

Ilibidi kwanza arejeshwe kwenye kazi yake ya PSSSF, then ndipo "kumstaafisha kwa manufaa ya umma" kufuate.

Hayo "manufaa ya umma", yanahusiana na nafasi ya u-DC ambayo aliteuliwa na Rais na siyo kazi yake ya awali ya PSSSF.

Pengine kama Rais asingemteua kuwa DC asingenge commit hiyo offence inayoathiri "manufaa ya umma".

Mamlaka ya Rais yana mpaka kwa wateule wake, hayako kama "blank cheque".

Na hii haitakuwa kesi ya kwanza kwa Mahakama kuwarudisha wafanyakazi waliotenguliwa na Rais. Kumbukeni wale Maadisa 5 wa Polisi (Man, Lymo, Walele et al) waliotenguliwa na B W Mkapa mwaka 1996.
Jamaaa ana hoja sana tena ya msingi mno, shida ni kwamba hii nchi imejaaa raia wapumbavu sana jumlisja waoga sana. Ndio maana huwa tunaweza hata chuchumaishwa ndani ya mabasi na tukaona sawa tu
 
Kuna watu Wana dharau za wazi wazi.

Unafikiri Enzi Cha bwana mkubwa angethubutu hata kujipost huyo ,?? Achilia mbali kuenda mahakamani
Sema muoga plus mjinga, Nchi imejaaa vilaza sana hii si bure Wazungu, Wakenya wanajichumia tu, kwa akili kama hizi zako unafikiria nini?
 
Wakati mwingine TZ ni shida. Wakiwa majukaani, wanahubiri kujiajili, Sasa zamu Yao ikifika, anaenda mahakamani Kugomea kujiajili kama walivyokuwa wanahubirii[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Yeye kafungua kesi na ni haki yake kikatiba, ndio maana kukawa na mahakama, kwani ulitakaje? Kuna sheria kavunja kufungua kesi? Itajulikana mahakamani
 
Back
Top Bottom