Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro ameripoti kwenye kituo chake kipya cha kazi Shinyanga

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro ameripoti kwenye kituo chake kipya cha kazi Shinyanga

Nina Uhakika ulikuwa na Kipimo chako cha ubora Kichwani. Niambie wewe saizi na hicho Kichwa chako unasomeka pande zipi.
Ni Muhimu kuwaheshimu Watu hasa ullosoma nao maana inakuletea Faraja kuwa Mungu Darasa lenu ameliona. Sasa Wewe Badala ya Kumshukuru Mungu kwa hillo wewe unaleta porojo.
Hawa ndo wale unakuta wachimba chumvi tu
 
Karibu kwenye madini ujiokotee
Watanzania wengi Bado geographia ya Nchi yetu hatuijui,Yaani Kuna watu Bado wanafokiri Madini Yako Shinyanga tu.Huko alikotoka Kuna Madini sana.Tunduru ndiko Kuna ruby,Suphire, Alexander n.k Kwa ufupi huyo alishamlizana kabisa huko anakuja kujazia.Hii Nchi imebarikiwa imetapakaa Madini sema Wananchi wake tu hawana Akili timamu.
 
Huyu mwamba hakuna anachojua ni mweupe sana kichwani. Nimesoma naye udsm 2007 namjua sana.
Mbona alikuwa waziri mkuu udsm.
Wao na akina Silinde na odong odwar plus Bush ndio walileta migomo na changes kwenye bodi ya mikopo ya sasa

Mkuu sio kila mtu haifahamu udsm,

Ondoa ujinga wako hapa
 
Jamaa alikuwa wa Moto sana alipokuwa DARUSO. Baada ya hapo amekuwa wa kawaida kabisa. SERIKALI zinatakiwa kuwakuza vijana katika mwelekeo sahihi kipindi wanapoonyesha juhudi, sio Iwatumia wakati wanapokuwa wakawaida. Kwa uwezo ule na utisho aliokuwa nao huyu Mh alitaliwa leo awe PM.
 
MTATIRO AKABIDHIWA MIKOBA SHINYANGA
View attachment 2932823
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Wakili Julius Mtatiro ameripoti kwenye kituo chake kipya cha kazi ili kuanza majukumu ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga.

Katika kikao kifupi cha makabidhiano ya ofisi, kilichohudhuriwa na Kamati ya Usalama ya Wilaya hiyo na Wakurugenzi 2; Manispaa na Shinyanga Vijijini, DC Mtatiro amekabidhiwa nyaraka mbalimbali, zikiwemo Taarifa ya Wilaya, Katiba ya Tanzania, Ilani ya CCM 2020 - 2025.
View attachment 2932824
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza Bi. Johari Samizi ambaye amehudumu kama DC Shinyanga kwa kipindi cha mwaka mmoja, ndiye amemkabidhi ofisi na mamlaka kwa DC Mtatiro.

DC Mtatiro amesema ameridhishwa na kasi ya maendeleo inayoendelea wilayani Shinyanga na kwamba anajipanga kushirikiana kwa dhati na viongozi, wadau na wananchi wote ili kazi ya Mkuu wa Mkoa na Rais Samia iwe nyepesi.
View attachment 2932825
Mtatiro ameahidi kuja na mpango kazi kabambe ambao utaendelea kuipaisha Wilaya ya Shinyanga na wananchi wake kiuchumi huku akisisitiza kuwa kipaumbele chake ni "haki" za wananchi.
View attachment 2932826
Mara baada ya makabidhiano hayo, DC Mtatiro ameanza safari kuelekea Tunduru mkoani Ruvuma ili kukabidhi Ofisi ya DC Tunduru kwa Mkuu wa Wilaya hiyo wa sasa, Simon Chacha, ambaye kabla alikuwa DC Sikonge, mkoani Tabora.

Faraja Stanley,
Shinyanga,
12.03.2024.
Makurya on the top
 
CCM killed the young man charisma and talent. Lipumba na Maalim ndio waliiona tunu na kipaji cha huyu bwana mdogo, mimi nilishuhudia maana akikuwa mbele yangu hapo Mlimani.
Kile kipaji cha kujenga hoja na kuzitetea, uwezo mkubwa wa kuhoji na kutetea hoja siouni tena kwa huyu jamaa. Kweli hakuna mkate mgumu mbele ya chai.
Magu ndio ka injinia kuua kipawa chake
 
Nina Uhakika ulikuwa na Kipimo chako cha ubora Kichwani. Niambie wewe saizi na hicho Kichwa chako unasomeka pande zipi.
Ni Muhimu kuwaheshimu Watu hasa ullosoma nao maana inakuletea Faraja kuwa Mungu Darasa lenu ameliona. Sasa Wewe Badala ya Kumshukuru Mungu kwa hillo wewe unaleta porojo.
Kbsaaa
 
Mtatilo ana uwezo wa kufanya kama dc na ded at the sametime. This man will be able to be the country president
Kwa English hiyo uliyomalizia kwenye post yako, sishangqi kwa nini unamuona Mtatiro ni genius. Kwenye kundi la vipofu, mwenye chongo ndiyo mfalme wao
 
Jamaa alikuwa wa Moto sana alipokuwa DARUSO. Baada ya hapo amekuwa wa kawaida kabisa. SERIKALI zinatakiwa kuwakuza vijana katika mwelekeo sahihi kipindi wanapoonyesha juhudi, sio Iwatumia wakati wanapokuwa wakawaida. Kwa uwezo ule na utisho aliokuwa nao huyu Mh alitaliwa leo awe PM.
Hivi akili zenu zina kazi gani? Akiwa DARUSO alikuwa mwanafunzi na kiongizi. Alitekeleza majukumu yake kwa wakati huo.

Sasa ni DC Shinyanga, bado unataka a behave kama mwanafunzi kiongozi wa DARUSO
 
Back
Top Bottom