Nimekushangaa sana. Kwamba, adhabu ya kifo ni kukiuka utu wa mtu, pia inamnyima fursa muuaji kupata kujifunza na kujutia makosa yake,,,na haisaidii kumfurahisha marehemu aliyekatishwa uhai wake.
Unasahau kuwa adhabu yoyote inasaidia kuleta amani na mshikamano (peace & stability) katika jamii, pamoja na kushawishi jamii kufuata mkondo wa sheria. Ina maana haya matukio ya wananchi wenye hasira kali kujichukulia sheria mkononi huyaoni? Unafikiri ndugu/jamaa na marafiki wa marehemu, watamuonaje na kuishije na huyo muuaji akiwa amerudi uraiani, mf. mjane/mgane anamuona mtu aliyemuua mwenzi wake au kijana aliye katika hali ngumu ya kimaisha anaoneshwa mtu aliyemuua baba yake...nini kitafuata?
Nakutaarifu kuwa maoni yako na hao wenzio yamenikera