SaidAlly
JF-Expert Member
- Jan 22, 2011
- 2,328
- 2,228
Kuna kitu nakiona kwenye hoja yako.Adhabu hii ya kunyonga hadi kufa ni kiashiria kingine cha kupuuza utu wa mtu wala si kwamba inawafanya wahukumiwa kujutia makosa yao au waliobaki kuogopa kutenda makosa kama hayo.... Na ndiyo maana bado tunaendelea kusikia visa vya mtu kutekeleza mauaji ya watu kadhaa kwa sababu za kipumbavu kabisa kisha naye kujiua. Yaani ni kama inaonekana muuaji anaogopa yale maumivu ya kimwili na kisaikolojia atakayoyapata wakati wa kuendesha kesi na wakati wa kusubiria utekelezaji wa hukumu kuliko hukumu yenyewe, Pengine ndiyo maana haoni taabu kujiua mara tu! baada ya kuwa amekamilisha uharifu wake wa Mauaji.
Itoshe tu kusema kuwa Adhabu ya kunyongwa hadi kufa haitoi nafasi ya muhusika kujirekebisha wala muathirika kufurahia haki aliyopatiwa na mahakama iliyotoa adhabu hiyo bali ni MAUJI KAMA MAUAJI MENGINE. #NIMEWAZA KWA SAUTI
Na je, ni sahihi mtu huyu akahukumiwa kifungo cha maisha kisha akapangiwa kazi ya uzalishaji kama kulima mashambani ili walau apate uchungu wa kufanyakazi nzito alafu haambulii chochote??