Aliyekuwa Mrakibu wa Polisi, Kinondoni akata rufaa dhidi ya hukumu yake ya kunyongwa hadi kufa

Aliyekuwa Mrakibu wa Polisi, Kinondoni akata rufaa dhidi ya hukumu yake ya kunyongwa hadi kufa

Kwahiyo Mkuu, Unapendekezeje? Je Alichokifangaya, Aachiwe Tu Huru Aendelee Ilihali Wafiwa Huwez Jua Ni Magumu Na Maumivu Kias Gani Wamekutana Nayo Kwa Kuondokewa Na Wapendwa Wao?.
ninatanguliza pole zangu kwa ndugu na familia za wafanya biashara hao waliopoteza maisha yao kinyama mno ,familia hizi zinaishi bila wapendwa wao na bread winners wao its tough life;ILA kwa upande wa pili wa adhabu hii ya KIFO,hivi ikitekelezwa itaifanya familia za waliouawa kuwa happy?,je utarudisha uhai wa ndugu zao?,je na familia za waliohukumiwa kifo zitakuwa ni familia bora zaidi?je kunyongwa hadi kufa kwa mtuhumiwa kutaleta better closure kwa wanandugu waliopoteza ndugu zao?,binafsi ninachukia adhabu hii ya kifo,ni adhabu inayoonyesha kuwa bado tunaishi maisha very primitive,na adhabu hii sio kuwa unafanya watu waogope kutenda kosa la kuuwa eti na wao watauliwa.ni wakati sasa Tanzania ifute hii adhabu ya kifo maana haina faida yeyote kwa jamii.
 
Alafu Huyu Jamaa Mbona Kama Anakula Bata Tu![emoji1][emoji1]
View attachment 1111303

Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Mrakibu wa Polisi (SP), Christopher Bageni, aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kuwaua wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro, amepinga adhabu hiyo katika Mahakama Rufaa jijini Dar es Salaam.

SP Bageni amewasilisha maombi ya mapitio Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ambayo yamepangwa kusikikizwa Juni 16, mwaka huu mbele ya jopo la majaji watatu, Stellah Mugasha, Ferdinand Wambali na Rehema Kerefu.

Katika maombi yake ya mapitio, Bageni amewasilisha sababu mbalimbali za kupinga adhabu hiyo ikiwamo kwamba jopo la majaji lilifanya makosa ya dhahiri katika muonekano na hivyo kusababisha haki kutozingatiwa katika kutoa hukumu hiyo.

SP Bageni alihukumiwa adhabu hiyo Septemba 16 mwaka 2016 na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania mbele ya jopo la majaji watatu, Jaji Benard Luanda, Sauda Mjasiri na Semistocles Kaijage.

Mahakama ya Rufaa ilitoa hukumu hiyo baada ya kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) akipinga aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi, Abdallah Zombe na maofisa wenzake watatu akiwemo Bageni kuachiwa huru na Mahakama Kuu mwaka 2009.

Hukumu hiyo ilisomwa na aliyekuwa Msajili wa Mahakama ya Rufaa wakati huo, Jaji John Kahyoza. Aliwataja wajibu rufani kuwa ni Zombe, SP Bageni, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.

Katika kesi hiyo, wafanyabiashara wa madini waliouwawa ni Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva taksi, mkazi wa Manzese Dar es Salaam, Juma Ndugu.

Walidaiwa kutenda makosa hayo Januari 14, mwaka 2006, katika Msitu wa Pande, uliopo wilayani Kinondoni baada ya kuwakamata wafanyabiashara hao Sinza, walipokuja Dar es Salaam kuuza madini.

Mtanzania
 
Kwahiyo Mkuu, Unapendekezeje? Je Alichokifangaya, Aachiwe Tu Huru Aendelee Ilihali Wafiwa Huwez Jua Ni Magumu Na Maumivu Kias Gani Wamekutana Nayo Kwa Kuondokewa Na Wapendwa Wao?.
no mkuu jitahidi usome vema kabla ya kujibu,hakuna sehemu niliyoandika kuwa aachiwe huru,nilichokiandika mimi suing mkono death sentence kwa sababu hazisaidii kurekebisha chochote kwenye jamii,bado nchi yetu tunashuhudia watu wakiua huku wakielewa kuwa tuna death sentence ndani ya nchi yetu,kinachotakiwa ni kuwa na adhabu mbadala kwa serious offences kama za murder,rapping,drugs etc etc,kama life sentences.nimekujibu ili next time usijibu kama hivi hii ni sawa na kuniwekea maneno kwenye kinywa change wakati mimi mwenyewe nina uwezo huo,always read to understand.
 
Ni muhimu iwepo ilikupunguza rate ya watu kufanya makosa,imagine leo hii itangazwe haipo usalama utapungua sana.Hata hivyo wanaonyongwa ni wachache sana wengi wapo gerezani tu
yaaa,lakini adhabu hii haionyeshi kuwa inaleta uoga kwa watu kuuwa,few weeks ago tumeshuhudia mauaji mengi tu ,kuanzia visasi,wivu wa kimapenzi,maiti za kwenye viroba,maiti za pale mto Ruvu etc etc watu bado wanaua,ni wakati sasa tuachane na death sentence na tuangalie adhabu mbadala.
 
ninatanguliza pole zangu kwa ndugu na familia za wafanya biashara hao waliopoteza maisha yao kinyama mno ,familia hizi zinaishi bila wapendwa wao na bread winners wao its tough life;ILA kwa upande wa pili wa adhabu hii ya KIFO,hivi ikitekelezwa itaifanya familia za waliouawa kuwa happy?,je utarudisha uhai wa ndugu zao?,je na familia za waliohukumiwa kifo zitakuwa ni familia bora zaidi?je kunyongwa hadi kufa kwa mtuhumiwa kutaleta better closure kwa wanandugu waliopoteza ndugu zao?,binafsi ninachukia adhabu hii ya kifo,ni adhabu inayoonyesha kuwa bado tunaishi maisha very primitive,na adhabu hii sio kuwa unafanya watu waogope kutenda kosa la kuuwa eti na wao watauliwa.ni wakati sasa Tanzania ifute hii adhabu ya kifo maana haina faida yeyote kwa jamii.

Faida ipo humuoni huyo aliyehukumiwa anapata mateso makali? Ndio anaonja ladha ya kutenda uhalifu, unataka aachwe tu astarehe?
 
Akili ndogo wewe!
lengo la mada ni kujadili,na tuna haki ya kutofautiana ndio mjadala,hatuwezi wote kuongea kitu kimoja otherwise hatuhitaji mjadala,ninakuona ni mtu mwenye hasira ambaye hata familia yako unailea kwa hasira na bila shaka ni mmoja wa watu wanaochangia nchi yetu kuanza kuwa na watu wenye hasira.,akili ninazo na nimeenda shule wakati nchi ina heshima na adabu,nikafundisha ,nikasafiri mno duniani and iam enjoying my life na nimeishi maisha yangu bora and I work to my ass
 
Ni kweli, si adhabu nzuri kabisa kwa binadamu.Lakini, ili kuifeel vizuri, ufanyiwe unyama wa aina hiyo ,yani mtu awaue watu wako wa karibu,hapo ndipo utaweza kutoa maoni sahihi.kuhusu adhabu hii.

Haya mambo yapo tata sana
nimekuelewa mkuu wote sisi ni binadamu ila kutekelezwa kwa adhabu hii hakutarudisha mpendwa wako uhai wake,na sidhani utapata any closure,na haisaidii chochote maana mauaji bado ni mengi mno na ndio yanazidi.
 
Kumuua BAGENI hakutarudisha uhai wa kina Chigumbi ila itakua fundisho kwa polisi wengine wanao ua watu wasio na hatia na kuwaibia. Vile vile kutaonyeaha kwamba institutions za serikali hii ziko hai na serikali inasimamia haki sio serikali ya wacha wapigwe tu kama untouchable mmoja alivyosemaga. Binafsi najua Bageni alihusika kuwaua wale watu huku akijua ni kosa mbele ya binadamu na dhambi mbele za Mungu.
Otherwise atuambie walikufaje au nani aliwau?
Sijui kwanini huwa naamini Bageni hakufanya kosa lolote na namuonaga Zombe akiwa mtuhumiwa No 1,ni kwa vile tu kwenye jeshi unapokea order ya mkubwa but to me Zombe ana hatia!
 
Subiri na wewe uuawe kwanza ndio utajua kama hukumu hiyo inafaa au haifai [emoji3]
no mkuu this debate kuhusu hii mada tuna haki ya kutofautiana,ila tuijadili kwa facts sio hasira na dharau,sio lazima wote tukubaliane,na kwa taarifa yako hii death sentence ni adhabu ambayo haijapunguza watu kutokuuwa,mauaji yanaongezeka mno na kwa sasa wivu wa kimapenzi watu wanaamua kuuwa.
 
Faida ipo humuoni huyo aliyehukumiwa anapata mateso makali? Ndio anaonja ladha ya kutenda uhalifu, unataka aachwe tu astarehe?
NOOOOOO sijasema aachiwe huru why wakati kushapatikana na hatia?ni lazima ahukumiwe swali je death sentence aliyopewa ataleta closure kwa waliofiwa?je atafanya watu wengine to think twice kabla ya kuuwa?majibu hapa ni NO,HII ADHABU HAISAIDI JAMII YETU.
 
Kwani,jamaa waligeukwa.CCM,sio ya kuaminka.mnapewa kazi,baadae mnageukwa
 
lengo la mada ni kujadili,na tuna haki ya kutofautiana ndio mjadala,hatuwezi wote kuongea kitu kimoja otherwise hatuhitaji mjadala,ninakuona ni mtu mwenye hasira ambaye hata familia yako unailea kwa hasira na bila shaka ni mmoja wa watu wanaochangia nchi yetu kuanza kuwa na watu wenye hasira.,akili ninazo na nimeenda shule wakati nchi ina heshima na adabu,nikafundisha ,nikasafiri mno duniani and iam enjoying my life na nimeishi maisha yangu bora and I work to my ass
Wewe haustahili kufanya mjadala na yeyote! Don't infect people with your DISEASE!
 
NOOOOOO sijasema aachiwe huru why wakati kushapatikana na hatia?ni lazima ahukumiwe swali je death sentence aliyopewa ataleta closure kwa waliofiwa?je atafanya watu wengine to think twice kabla ya kuuwa?majibu hapa ni NO,HII ADHABU HAISAIDI JAMII YETU.

Inasaidia kusudu la kumnyonga ni kutoa funzo kama wewe funzo halikufikii bac pole yako ila aliyeua nae auwawe
 
Katika hii kesi kuna dogo mmoja polisi ambae alikufa katika mazingira ya kutatanisha. Alieleza ukweli kabla hajafia gerezani. Dogo mmoja mchagga nasahau jina. Naona nafsi na imani yake ya kidini vilikua vinamsuta
Alieleza nn
 
no mkuu this debate kuhusu hii mada tuna haki ya kutofautiana,ila tuijadili kwa facts sio hasira na dharau,sio lazima wote tukubaliane,na kwa taarifa yako hii death sentence ni adhabu ambayo haijapunguza watu kutokuuwa,mauaji yanaongezeka mno na kwa sasa wivu wa kimapenzi watu wanaamua kuuwa.
Ok. Tufanye kama debate basi, wewe unapendekeza iwe hukumu gani mbadala?

Labda nikuulize, kwanini kwanza huwa kuna sheria? Na ikivunjwa kwanini kuna kuwa na kesi? Na kwanini maamuzi yanayotokana na kesi yaitwe hukumu? Lengo la hukumu ni nini? Kisha tuambie mtu aliyeua kwa makusudi afanywe nini?

Mimi sina hasira, ingawa kwenye mijadala kama hii inayogusa hisia za watu ni ngumu kutenganisha hisia na uhalisia, wewe mwenyewe hapo unasukumwa na hisia kwamba adhabu ya kunyonga haifai ingawa unaamini hutumii hisia ila uhalisia. Na ukichomoka hapo itabidi tuje kwenye mjadala mwingine hisia ni nini.

Ni sawa na wanaosema hawapendi au hawafuatilii mambo ya siasa wakati huohuo ana lalamikia baadhi ya mambo yanayokera au kukwamisha jamii...bila siasa hamna kitu kitafanyika. Tatizo ni aina gani ya siasa inatumika.
 
Naomba ni-declare interest kwamba niliwahi kufanya kazi Jeshi la Polisi tena Kikosi hicho hicho cha kupambana na majambazi na mpaka naacha kazi nilikuwa hapo hapo Oysterbay,na askari wote waliokumbwa na kesi ninawafahamu maana nilifanya nao kazi,hukumu ya Jaji Kipenka ya kuwaachia huru watuhumiwa wote ilikuwa sahihi maana askari aliyewafyatulia wale marehemu hakuwahi kukamatwa mpaka leo!! wengine wote walirudisha silaha zao Armory zikiwa na risasi kamili kama walivyochukua isipokuwa huyo mmoja,ndio maana Jaji Kipenka wakati anawaachia huru watuhumiwa alisema kabisa "MLETENI MTUHUMIWA ALIYEUA MAANA YEYE NDIE ALIRUDISHA SILAHA IKIWA HAINA RISASI"kwa hiyo naamini hili Jopo la Majaji wa Mahakamani ya Rufaa nitamuachia huru Christopher Bageni maana hakufyatua risasi hata moja kuua marehemu
Katika maisha yangu,wazazi wangu walinilea na kunieleza kuwa kwa kazi yoyote ambayo nitakayoifanya inabidi kuwaheshimu watu wengine na kumtanguliza Mungu siku zote kwa kufata amri zote kumi za mwenyezi Mungu.Kinachokosekana kwa watu wengi wa kisasa ni hekima,ambayo hupelekea kukosa kiasi na utu katka maisha au hata kazi zao za kila siku.
 
Back
Top Bottom