TANZIA Aliyekuwa Mtangazaji wa RFA, Juma Ahmed Baragaza afariki Dunia

TANZIA Aliyekuwa Mtangazaji wa RFA, Juma Ahmed Baragaza afariki Dunia

ٱلَّذِينَ إِذَآ أَصَٰبَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوٓا۟ إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّآ إِلَيْهِ رَٰجِعُونَ

Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.
 
Mtangazaji maarufu wa Radio free Afrika na Star Tv, Juma Ahmed Baragaza amefariki dunia leo Agosti 7. Atakumbukwa zaidi katika vipindi mbali mbali alivyojipatia umaarufu ikiwemo Mambo Mambo na RFA pamoja na Asili ya Mtanzania kupitia Star Tv.

View attachment 1884193
RIP nilipenda utangazaji wake sijui alikuwa anaumwaa!
 
Ulifundishwa vle kuwajua walioathirika? Utakufa wewe ukiwaamini kwa macho, na watu Kama nyie ndo wepesi wa kutangaza watu kuwa wamewaka kwa macho[emoji848][emoji848]
Hamjui Mungu huyo akiamua lake anatenda, kuna mkaka alikuwa anamuuguza ndugu yake kilichofuata kaumwa yeye malaria siku yakwanza yapili kaondoka kaacha mgonjwa hata ndugu walijua mgonjwa wazani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtangazaji maarufu wa Radio free Afrika na Star Tv, Juma Ahmed Baragaza amefariki dunia leo Agosti 7. Atakumbukwa zaidi katika vipindi mbali mbali alivyojipatia umaarufu ikiwemo Mambo Mambo na RFA pamoja na Asili ya Mtanzania kupitia Star Tv.

View attachment 1884193
Daah amefanya nimkumbuke Zuberi Msabaha wa Bolingo time, Kwa heri malegend wa ukweli
 
Umegeuza, Alianza Baragaza wakifanya kwa kupokezana na Fredwaa na ndipo akaja Wambura Mtani ambaye anaendelea nacho mipindi hicho cha JE, HUU ni UUNGWANA, kesho jumapili Mungu akipenda utaweza kumsikia akiendesha kipindi hicho.

Baragaza alikuwa akitangaza kipindi cha Mambo Mambo na Sweet Menthol (SM) kinachoruka hewani kuanzia saa 10:15 jioni mpaka saa 12:00 jioni jumatatu hadi ijumaa na baadae kikabadilika jina na kunaitwa Mambo Mambo. Pia alikuwa anatangaza kipindi cha lugha gongana. Baadae alikuwa Meneja wa vipindi RFA kama Sikosei

Apumzike kwa Amani.
Ahsante mkuu...enzi hizo hiki kipindi kilikuwa kinanichelewesha hata kanisani...ibada inaanza saa nne kipindi kinaanza saa tatu na nusu. Nilikuwa nazuga hadi kiishe ndio niondoke sema wakati ule nilikuwa mdogo sikuwa nakariri majina ya watangazaji
 
Back
Top Bottom