Pre GE2025 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Msigwa ni mwakirishi wa matapeli wa Iringa,wanaiba Mali za watu wanatapeli.maheka na maheka ya mashamba ya miti na pia kuchoma misitu ya Sao Hill ili watoboe,nitakuwa wa mwisho kuipenda Iringa.Nimewaona sio watu poa na msigwa aende na opotee mazima
Atagombea Iringa wacha tuone yeye na Jesca Mtavangu
 
Je Mchungaji Msigwa aliipuzwa madai yake?! Hapa Mnyika anatakiwa atueleze kinaga ubaga.
 
Hakika wanasiasa siyo wa kuwaamn huyu SI ndyo alikataa sijuh ni pesa za rambi rambi au za nn nimesahau,alizopewa na the late Mr president (RIP DDADY)

Mwanasiasa akikuambia sasahv ni usiku,aisee Bora utoke nje ukahakikishe.! Na Leo nimeamn hawa watu wanapambania matumbo yao
 
Tatizo siyo vyama, ni watu.
Itikadi na Katiba za vyama zipo pale pale.
Kutokutimia kwa malengo binafsi, kuyumba kiuchumi na kijamii (kutokuelewana na washirika, wanachama na viongozi wenzake), humlazimisha mhamaji ili kutafuta hifadhi.
 
huwa nawashangaa sana watu wanaompapatikia tundu lisu, hakuna mtu corrupt kama tundu lisu chadema, hata yeye (tundu lusu) is next kwenda ccm utasikia tu muda si mrefu, matter of fact chadema yote ni controlled opposition …
Lusu Alikimbia mkutano kufanya na mbowe
Alichukua pesa za wazungu aliposikia kwa Mbowe kuwa kampeni Karatu watatumia Helikopta akajua hapa ulaji upo

Akajiasemea nitasema nilikodi helicopter kwenye kwa mikutano na kuwa akawachomoa pesa wazungu za Helicopter atakayokodi

Kufika karate akakutana na maajabu ya dunia Mbowe kapaka helicopter rangi ya bendera ya Chadema na kaweka picha yake kama ndie mfanya mikutano hiyo mikubwa sio Tundu Lisu sababu ile helicopter ilirushwa vyombo vya kimataifa wakiwemo wafadhili ikionyesha Mbowe ndie mwenyewe siasa za upinzani Tanzania ana hadi Helicopter ya kampeni

Lisu akaona hapa biashara haitanilipa namtangaza Mbowe kimataifa tu akazira akaamua kuacha mkutano na kutimkia ubelgiji kwa hasira kwa visingio vya uongo pamoja na kuwa aliahidi mikutano yote atakuwepo

Alijifanya mjanja kakutana na mtoto mjanja zaidi wa mjini Mbowe Helicopter kaweka picha yake

Akipigwa picha Mbowe anahutubia na Helicopter inaonyeshwa ya mwanasiasa mahiri yenye picha yake.mheshimiwa mwanasiasa mahiri Mbowe
 
Aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa , Mchungaji Peter Msigwa amejiondoa kutoka chama hicho na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo Jumapili, Juni 30, 2024, jijini Dar Es Salaam.

Msigwa amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona Chadema kimepoteza uhalali wa kuwa mkosoaji wa CCM, lakini pia kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayofanya ya kuiongoza nchi na kuwatumikia Watanzania. Pia baada ya kuchoshwa na siasa za uongo, unafiki na kiulaghai zinazofanywa na Chadema.
 

Attachments

  • IMG-20240630-WA0130.jpg
    332.3 KB · Views: 1
  • IMG-20240630-WA0128.jpg
    553.8 KB · Views: 1
  • IMG-20240630-WA0126.jpg
    151.4 KB · Views: 1
  • IMG-20240630-WA0125.jpg
    361.4 KB · Views: 1
  • IMG-20240630-WA0123.jpg
    596.4 KB · Views: 1
Sijashindwa kujua maana yake kwa sababu ni neno la kimombo la! Nimetaka nijue umelitumia kwa muhtadha gani kwa sababu swali lako hali-make sense kwenye kuhoji maelezo niliyotoa. Bado niko pale pale. Wewe unasumbulia na ufinyu wa mawazo kuhusu siasa kwa ujumla. Bado unadhani siasa iko kwa ajili ya wanasiasa tu na wananchi wengine wanatakiwa kukaa kimya. Halafu ''nitashabikia siasa kama tutaruhusu mawazo....''. Dear, unasubiri nani akuruhusu? Unadhani kuna siku utakuja kuletewa haki yako kwenye kisahani? Nakuhakikishia kuwa mambo yanazidi kuwa magumu na siku si nyingi wewe au mtu wako wa karibu ataathirika (kama haijawa hivyo tayari).
 
Tundu Lisu njoo huku unafanya nini ubelgiji ? Habari za mjini ziko huku Tanzania

Acha kusikiliza BBC na CNN

Breaking news ziko Tanzania

Your comments please hili la Msigwa swahiba wako kukutoroka unasemaje?
Naye yuko njiani, ni swala la muda tu! Ila hii ni haki yake Msigwa kufanya akipendacho!
 
Hili nililijua mdaa mrefuu ,kutokana na mienendo yakee,

Na CHADEMA wenyewe walimshtukia kitamboo,ndio maana hata MKiti aliwachia kina martin Maranja washulike nayee .
And honnest Chadema wanahitaji pongezi kwa hili la kumzui huyu jamaa kuwa mwenyekiti wa Kanda huko kusini
 
Nasubiri huo muda.

Kanuni ni mbili tu weka akilini kwako na uishi nazo maisha yako ya hapa duniani

1. AKIPINGA = HAJAGAIWA
2. AKIPIGANIA (AKILINDA)= AMEGAIWA
 
Better be kuliko kutumika kufaidisha watu

Mnamchangia mtu V8 hata Raum huna?
Wengine wanapeana hadi sumu alaf wanapewa elfu 7 ya bando wakiahidiwa watapewa UDED
Huo ubinafsi ndio umelifikisha hapa lilipo taifa

Unaonekana nawe ukapata nafasi ya juu ya uongozi TANZANIA utaanza na huo ubinafsi wako kwa kufanya kile ambacho kina masilahi nawe

Badilika ndugu ubinafsi haufai kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…