Aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli azikwa Chato mkoani Geita

Ulikuja chanika juzi imenyesha sanaa tu

Ili iwe ajabu unyeshe eneo la tukio tu
 
Nakumbuka 2012 huko Mbarali Mbeya alififariki nguli mmoja Na mchawi mkubwa wa usangu nzima. Ilikuwa ni mwezi wa 8 kipindi cha kiangazi. Muda wa kumzika mida ya saa 8 mchana ilinyesha mvua isio ya kawaida. Toka nizaliwe sikuwahi kuona mvua ikinyesha msimu kama ule.
 
Habari za muda huu.Kwanza nitoe pole kwa msiba huu mzito uliotukumba taifa letu na mpaka sasa tupo katika hatua za mwisho za kumpumzisha mpendwa wetu JPM katika makazi yake ya milele....
Tuendelee mkuu kumshukuru Mh. Hayati Rais wetu mpendwa kwa kutuletea hali ya mawingu na mvua. Daima tutaendelea kumkumbuka.
 
Hahaa hii ndiyo mtakuja Street jf. Karibu saana baby ntakutafuta baada ya maziko maana nimwkuona uko unachat
Dah unafanya tucheke kwenye msiba.🤣🤣🤣🤣

Mtu ashatwishwa na cheo cha baby fasta
 
Ibada za wafu, hizo sifa zoe angepewa tu Mungu na si mwanadamu.
Kuna watu wanamsifia na kumtukuza kuliko wamsifiavyo Mungu na wake zao.
 
BURIANI MAGUFULI: Ibada bado inaendelea uwanja wa Magufuli, Chato ambako kuna Kanisa la muda lililoandaaliwa kwaajili ya ibada ya mwisho ya Hayati Dkt. John Magufuli


Baadhi ya waombolezaji waliopo hapa uwanja wa Magufuli, Chato ambapo itafanyika ibada ya mwisho ya kuaga mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli.
Tayari viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wameshawasili katika eneo hili.



 
Aidha pia alisuggest mwili wa JPM usizikwe Bali ukaushwe na kwekwa kumbukumbu kwa vizazi vijavyo. Amesema siku ya maziko kutanyesha mvua kubwa sana iliyoambatana na radi nchi nzima ikiwa watamzika.

Na hiyo ni ishara ya ardhi kulaaniwa kwani jpm hajafa kifo naturally kama inavyosemekana Bali kuna watu wamehusika.
Pia kutatokea misiba mfululizo ikiwa wafanya hivo

Moderator msiifute hii thread.let's keep it tuone.huwezi jua.
Pasipo maono taifa huangamia.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…